mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 389
- 378
Kila tokeo la kimwili bila kujali kama ni chanya ama hasi asili yake ni roho ama rohoni... Hakuna kitu kisicho asili na roho ama nguvu isiyoonekana.... Hata huyu Mungu mkuu anayebishaniwa kila siku uwepo wake ni kinyume cha miungu ile ya kuchonga ile inayoonekana kwa macho..... Hata haya macho na masikio na sauti zetu... Kuna macho na masikio ya kuonekana, kuna sauti za kusikika na kuna macho masikio na sauti vya rohoni.... Havionekani havisikiki lakini vipo na ndio asili na chanzo cha ulimwengu unaoonekana
Maslahi ya kiroho ninini? Ni yapi?
Maslahi ya kiroho ni ukamilifu wa jambo lolote baya ama zuri kwenye ulimwengu wa nyama, ulimwengu unaoonekana kwa macho ya kawaida
Kutokamilika kwa jambo husika, maslahi ya kiroho huwa shakani na katika mtanziko mkubwa kutokana na kushindwa kufanya ukamilifu... Hapa sasa chanzo na sababu za kushindwa hutafutwa!!!!
Kila kitu, kila jambo huanza na wazo, wazo halionekani, halishikiki halisikiki.. Hiki linaishi rohoni.. Ndio penye chanzo chake... Wazo huzaliwa na kupangwa kati ya mtu na mwenyewe ndani ya nafsi zake tatu kabla ya kushirikisha nafsi ya nje, nafsi ya nne...
Wazo hata bila kupangwa ndani ya mwenyewe linaweza kuwasilishwa nje ya nafsi kwa njia ya sauti, michoro, maandishi na hata vitendo.... Baraza la nafsi lenye wajumbe nafsi tatu ndio huamua aina ya uwakilishi husika
Baraza nafsi tatu ndani ya nafsi ni lipi?
Nafsi ya kwanza ni nafsi roho... Mwenyekiti
Nafsi ya pili ni nafsi ufahamu... Katibu
Nafsi ya tatu ni nafsi wajumbe/hadhira... Muunganiko wa nafsi roho na nafsi ufahamu vinavyozaa utambulisho....
Asili ya wazo hutoka kwa wote katika muunganiko wa umoja, nafsi ufahamu akiwa ndio mzizi...
Hapa wazo hufanyiwa kazi na kukubaliwa na baraza la nafsi kwa sauti moja.... Kama kukiwa kuna kusitasita basi tambua kwenye kikao cha baraza la nafsi kuna mmoja hajakubaliana na wazo... Na shida itaanzia hapa kama kutakuwa na kufeli baada ya matokeo ya kimwili kuwa tasa au kuharibika....
Unapopanga jambo lakini ukawa kila wakati uko kwenye mtanziko wa kulifanya ama kutolifanya tambua baraza lako la ufahamu halijakubaliana kwa sauti moja....
Maslahi ya kiroho daima huzingatia na hudai mrejesho kwa kila tendo lililokamilika kwenye matokeo ya kimwili
Kama matokeo ni chanya baraza hushangilia na kupata faraja.... Lakini kama matokeo ni hasi basi lazima kitafutwe chanzo ama sababu yake....
Hapa kuna sababu nje ya baraza... Hizi si muhimu sana na maslahi ya kiroho huwa hayazingatiii sana.. Sababu ya kushindwa kama inatokana na maamuzi ndani ya baraza la nafsi, ama maamuzi yaliyokuwa yanakinzana ama kupishana hapa hali huwa mbaya na maslahi ya kiroho ndani ya mamlaka ya baraza la nafsi huamua kujiadhibu....
Ni adhabu gani hizo basi....
Majuto yenye kukosesha furaha na amani
Vilio mfululizo
Mawazo mpaka kuugua ama kushindwa kula nk
Kujidhuru mwili kwa vileo, madawa nk
Hisia za kutaka kulisambaratisha baraza na mamlaka yake kwa kuamua kujitoa uhai..
Nknk
Tuna tabia ya kuwacheka wengine wanaopitia hizi hali bila kutambua kuwa sio wao bali ni matokeo ya kushindwa kimwili yale yote yaliyopangwa na maslahi ya kiroho kupitia baraza la nafsi.....
Nimeeleweka?
Jr
Kuna kitabu kipo humu kwa sura kadhaa...
Kinaweza kupendeza hapa.
===
Sura 8
Masomo ya Elihu. Uumoja wa Maisha yote. Nafsi Mbili. Ibilisi. Upendo mwokozi wa wanadamu. Daudi wa nuru.Goliati wa giza.
TENA Elihu alikutana na wanafunzi wake katika ua takatifu na kusema, 2 Hakuna mtu ajiishiaye kwake yeye mwenyewe; kwa kuwa kila kitu hufungwa mpaka na kamba kwa kila kingine kiishicho. 3 Wamebarikiwa sana ni wale wenye kuwa na moyo safi; kwa kuwa wao watapenda na bila kulazimu upendo kurejeshwa. 4 Wao hawatowatendea wengine vile ambavyo wasingalivipenda wao kutendewa na wengine. 5 Kuna nafsi mbili; ya Juu na ya Chini. 6 Nafsi ya Juu ni roho ya mwanadamu iliyovikwa kwa Sonafi, iliyofanyika katika namna ya Mungu. 7 Nafsi ya chini, nafsi ya kimwili, mwili wa matamani, ni mwakisiko wa nafsi ya juu, iliyotengukika sura kwa etha za mfano wa maji yaliyoingia vumbi la tope la mwili wa nyama. 8 Nafsi ya chini ni onekano la machoni na hali lisilo la kweli ndani yake, na litapita zake; nafsi ya juu ni Mungu katika mtu, na haitapita zake. 9 Nafsi ya juu ni utwaaji mwili wa kweli iliyogeuzwa, na hivyo ni mdhahiriko wa usikweli. 10 Nafsi ya juu ni hali ya kuwa na haki, rehema, upendo na usahihi kwa katikati; nafsi ya chini i si kama vile ilivyo kwa nafsi ya juu. 11 Nafsi ya chini huzaa chuki, usaliti, ukosefu wa maadili, mauaji, wizi, na kila kitu chenye kudhuru; Nafsi ya juu ni mama wa karama(mapaji*) zote na utulivu wa kwenda na hali sawa na sambamba wa maisha yote. 12 Nafsi ya chini ni yenye utajiri wa ahadi, lakini i maskini katika ubarikika na amani; hutangaza kuzawadia starehe, furaha na mapato ya kujiridhishia; lakini hutoa kutokutulia na mataabiko na kifo. 13 Huwapa wanadamu matunda[apples] yenye sura ya kupendeza machoni na yenye kuwa na harufu kuvutia; na viini vyake vya ndani vimejaa uchungu na nyongo. 14 Ikiwa mngaliniuliza kipi cha kuchunguza ili kukisoma ningalisema ninyi wenyewe; na mtapokuwa mmesoma, na halafu tena mngaliniuliza kipi cha kufuatia kusoma, ningalijibu, ninyi wenyewe. 15 Yeye mwenye kujuvua vema nafsi yake ya chini, yuajua madanganyo ya sura ya ulimwengu, avijua vile vyenye kupita zake; na yeye mwenye kujua nafsi yake ya juu, yuajua Mungu; ajua vema vile vitu visivyoweza kupita kwenda zake. 16 Amebarikiwa mara tatu ni yule mtu aliyevifanya usafi na upendo wa moyo kuwa ni vyake hasa; amelipiwa deni la uhuru wake kutoka katika makucha ya nafsi yake ya chini na yeye mwenyewe ni nafsi yake ya juu. 17 Wanadamu watafuta wokovu toka kwenye uovu ambao wanauchukulia kuona ni dubwana lenye kuishi huko chini kuliko laaniwa; na wana miungu ambayo si kingine ile mapepo katika sura ya kujificha; yenye nguvu tele, na wakati yamejaa wivu tele na chuki na matamanio; 18 Ambayo fadhila zake ni lazima kununuliwa kwa kafara zenye kugharimu za matunda, na za maisha ya ndege, na wanyama, na binadamu. 19 Na wakati miungu hawa hawana kwao masikio kusikia, hakuna macho kuona, na wala moyo wa kuelewa hisia, hakuna nguvu kuokoa. 20 Uovu huu ni hadithi za kubuni; miungu hawa wamefanyika kwa hewa, kuvikwa kwa kimvuli cha fikra. 21 Ibilisi pekee kutoka kwa huyo wanadamu wote yawapasa kuwa wamekombolewa ni nafsi, nafsi ya chini. Ikiwa mtu angalimpata mwokozi wake yamlazimu kutazama ndani yake; na pale nafsi pepo iondolewapo katika kiti cha kifalme mwokozi, upendo, atanyanyuliwa katika kiti cha nguvu na enzi. 23 Daudi wa nuru ni Usafi wa moyo, mwenye kumchinja Goliati imara wa giza, na kumtawaza kitini mwokozi, upendo, juu ya kiti cha enzi.
===
Sura ya 12
Masomo ya Salome. Sala. Somo la kuhitimishia la Elihu. Kujumlishia yote ya mafunzo ya miaka mitatu ya kujifunza. Wanafunzi warejea makwao.
SASA, Jua la asubuhi lilipochomoza wakuu na wanafunzi wao wote walikuwa katika ua la bustani iliyofanywa takatifu. 2 Salome alikuwa wakwanza kuzungumza, yeye akasema, Tazama Jua! Ladhihirisha sura ya nguvu ya Mungu azungumzaye kwetu kupitia Jua na Mwezi na Nyota; 3 Kupitia mlima, kilima na korongo; kupitia maua, na mmea na mti. 4 Mungu atuimbia kwa sisi kupitia ndege, kinubi, na sauti ya mwanadamu; azungumza kwetu kupitia pepo za kuvuma na mvua na mngurumo wa radi; kwa nini tusili inamie mbele na kuabudu miguuni pake? 5 Mungu azungumza na mioyo iliyo wazi; na mioyo iliyowazi na ilazimu kuzungumza naye; na hili ni sala. 6 Si sala kupaza sauti kubwa kwake Mungu, kusimama, ama kukaa, ama kupiga magoti na kumwambia yeye yote juu ya dhambi za wanadamu. 7 Si sala kumweleza Mtukufu Mmoja ni jinsi gani alivyo mkubwa, jinsi gani alivyo ni mwema, jinsi gani alivyo na nguvu na jinsi gani alivyona huruma. 8 Mungu si mtu kununulika kwa kusifu kwa mwanadamu. 9 Sala ni tamanio la mfano wa moto wenye kuwaka sana yakwamba kila njia ya maisha kuwa nuru; yakwamba kila tendo livikwe taji kwa chema; yakwamba kila kiumbe hai kineemeke kwa huduma yetu. 10 Tendo lenye sifa kuu, neno lenye kuleta msaada ni sala; yenye kuwa na hisia kali, sala yenye kuathiri matokeo. 11 Bubujikio la Sala lipo katika moyo; kwa fikara akilini, si maneno, moyo hubebwa juu kwa Mungu, inakorehemiwa, basi wacha tusali. 12 Wakasali, lakini hakuna neno lililosemwa; ila katika ule Ukimya Mtakatifu kila moyo ulirehemiwa. 13 Na halafu tena Elihu akazungumza. Alisema kwa Mariamu na Elizabeti, maneno yetu yamesemwa; hamuhitaji tena kubakia kukaa hapa zaid; wito umekuja; njia i wazi, mnaweza kurudi katika nchi mtokazo. 14 Kazi kubwa mmepewa kufanya; mtaonesha mwelekeo akili ambazo zitaonesha mwelekeo kwa ulimwengu. 15 Wana wenu wametengwa kuwaongoza wanadamu juu katika mawazo yenye haki, na maneno, na matendo; 16 Kuwafanya wanadamu kujua udhambi wa dhambi; kuwaongoza wao kutoka kwenye mahusudisho ya nafsi ya chini, na vitu vyote vidanganyifu kwa sura, na kuwafanya kuwa macho na nafsi yenye kuishi na Kristu katika Mungu. 17 Katika maandalizi ya kazi yao wana wenu yawabidi kupita katika njia nyingi za miiba. 18 Hukumu kali na majaribu na majaribu watakutana navyo, kama wanadamu wengine; mizigo yao haitakuwa ni miepesi, na watachoshwa, na kudhoofu. 19 Nao watajua madhaa [pangs] ya njaa na kiu; na bila sababu watadhihakiwa, kufungwa, kuadhibiwa kwa mijeledi. 20 Kwa nchi nyingi watakwenda, na miguuni pa watu wakuu kiroho wengi wataketi, kwa kuwa yawalazimu kujifunza kama wanadamu wengine. 21 Lakini tumesema yakutosha. Baraka za watatu na za Saba, hao wenye kusimama mbele za mahala pa enzi, kwa hakika watatulia juu yenu hata wakati wote zaidi. 22 Na hivyo ndivyo lilivyofungwa somo la Elihu na Salome. Miaka mitatu waliwafundisha wanafunzi wao katika ua la bustani iliyofanywa takatifu, na ikiwa masomo yao yote yangeandikwa kitabuni, lo, ingalikuwa ni kitabu kikubwa; ya yale waliyosema tunajumla yake. 23 Sasa, Mariamu, Yosefu na Elizabeti na Yesu na mtayarisha njia wake, wakaianza safari kuelekea njia ya nyumbani. Hawakwenda kwa karibu na Yerusalemu, kwa kuwa Arkelausi alikuwa akitawala. 24 Walisafiri kupita Bahari ya Chungu, na walipofika vilima vya Engedi walipumzika katika nyumba ya Yoshua, ndugu wa karibu; na hapa Elizabeti na Yohana waliishi kukaa. 25 Lakini Yosefu, Mariamu na wana wao wakwenda kwa njia ya Yordani, na baada ya siku kadhaa walifika nyumbani kwao katika Nazareti.
===
Sura ya 14
Masomo ya Matheno. Mafundisho ya kanuni ya sheria ya ulimwengu wote. Nguvu ya mwanadamu kuchagua na kufikia kupata. Manufaa ya hali ya kukanganya. Vitabu vya zamani vilivyofanywa vitakatifu. Nafasi ya Yohana na Yesu katika historia ya ulimwengu.
Matheno na mwanafunzi wake, Yohana, walikuwa wakiongea ya vitabu vilivyofanywa vitakatifu vya zama nzee, na ya mafunzo ya dhahabu yalivyobeba, na Yohana atamka kwa kushikwa na hamasa, 2 mafunzo haya ya dhahabu ni yenye kuinukia juu sana; tuna uhitaji gani wa vitabu vingine vitakatifu? 3 Matheno akasema, Roho wa Mtakatifu Mmoja husababisha kila kitu kuja na kwenda katika wakati ulikaa vizuri. 4 Jua lina wakati wake mwenyewe kuzama, mwezi kuinuka, mwezi kupita kuwa mkubwa na kuwa mdogo, nyota kuja na kwenda, mvua kuanguka, pepo kuvuma; 5 Nyakati za Mbegu na nyakati za mavuno kuja; mtu kuzaliwa na mtu kufa. 6 Roho hizi kubwa husababisha mataifa kuzaliwa; huyapembeleza katika kijitanda, kuyapa matunzo hadi kufikia nguvu imara na majukumu yake yanapoisha huyafungasha hayo katika mashuka yake ya kuvingirishia na kuyalaza ziarani. 7 Matukio nimengi katika maisha ya taifa, na katika maisha ya mwanadamu, ambayo si yenye kufurahisha kwa wakati; lakini katika mwisho kweli hutokea: chochote chenye kuja ni kwa lililo bora kabisa. 8 Mwanadamu aliumbwa kwa sehemu yenye sifa ya hadhi; lakini hakuweza kufanywa mtu huru aliyejaa hekima, kweli na nguvu. 9 Ikiwa angefungiwa uzio, kufungiwa nafasi katika mafinyangizo kutoka kwa hayo hawezi kufaulu, basi angalikuwa ni mfano wa mwanasesere, mashine. 10 Roho za Uumbaji zilimpa mwanadamu utashi; na hivyo ana nguvu ya kuchagua. 11 Yeye aweza kufikia kupata vimo vya juu kabisa, ama kuzama chini kabisa ya vina; kwa kuwa kile akifanyiacho nia kupata anayo nguvu ya kukipata. 12 Ikiwa atamania uimara wa ndani yeye anayo nguvu ya kupata uimara huo; 13 Hivyo, katika mzunguruko wa mkorogano wa migongano yenye pande nyingi mwanadamu kawekwa pale ambapo yampasa kujifanyia jitihada kujinasua mwenyewe. 14 Katika kila migongano mwanadamu hupata nguvu ya kusimama imara; na kwa kila kuyashinda mapigano yeye afikia vima vya juu zaidi. Na kwa kila siku hukuta majukumu mapya na matunzo mapya ya kujali. 15 Mwanadamu habebwi juu ya mashimo ya hatari, na wala kusaidiwa kuwashinda maadui wake. Yeye mwenyewe ni jeshi lake, upanga wake na ngao; na yeye ni kapteni wa umma wake. 16 Mtakatifu Mmoja hutia tu nuru njia yake. Mwanadamu hajapata kamwe kuachwa bila taa ya mwanga kuongoza. 17 Na siku zote amelikuwa na mwenge wa taa uliowashwa mikononi mwake ili aweze ona miamba ya mawe hatari, maji yenye tope na mashimo yasiyotabirika. 18 Na hivyo Wenyekuwa Watakatifu wameshafanya hukumu; wanadamu walipohitaji mwangaza ulioongezeka nafsi roho kuu imekuja duniani kutoa mwangaza. 19 Kabla ya siku za kiveda ulimwengu ulikuwa na vitabu vingi vitakatifu kutia mwangaza njia; na mwanadamu alipohitaji mwangaza mkubwa zaidi Veda, Avesta na vitabu vya Tao Kubwa vilitokea kuonesha njia kielekea vima vya juu. 20 Na katika penye kufaa Biblia ya Kiebrania, pamoja na kanuni za sheria zake, manabii wake na Zaburi zake, vilitokea kwa ajili ya utaamuliko wa mwanadamu. 21 Lakini miaka imepita na wanadamu wanalo hitaji la mwangaza mkubwa zaidi. 22 Na sasa Nyota ya Mchana kutoka kuliko ni juu yaanza kung'ara; na Yesu ni mjumbe aliyefanyika kwa nyama kuonesha ile nuru kwa wanadamu. 23 Na wewe, mwanafunzi wangu, umeteuliwa kuiandaa siku ijayo. 24 Lakini yakupasa kutunza usafi wa moyo ulio nao sasa; na yakupasa kuwasha taa yako moja kwa moja kutoka kwenye makaa yenye kuwaka kutoka kwenye altare ya Wenyekuwa Watakatifu. 25 Nayo taa yako itabadilishwa namna ya umbo na sura kuwa moto usiyokingwa na mipaka, na utakuwa ni mwenge ambao nuru yake itang'ara kokote aliko mtu. 26 Lakini katika zama bado kuja, mwanadamu atafikia vimo vya juu zaidi, na nuru iliyo ni kali zaidi itakuja. 27 Na basi, mwishowe, nafsi roho mkuu mkubwa atakuja duniani kumulika njia kuelekea mahala pa enzi pa mtu kamilifu.
===
Sura 22
Urafiki wa Yesu na Lamaasi. Yesu amuelezea Lamaasi maana ya kweli, mtu, nguvu, uelewa, hekima, wokovu na imani.
MIONGONI mwa makuhani wa Jaganati alikuwapo mmoja alimpenda kijana wa Kiyahudi. Lamaasi Bramasi lilikuwa ni jina ambalo alikuwa akijulikana nalo. 2 Siku moja Yesu na Lamasi walipokuwa wakitembea pekee yao katika njia zilizopo katika viwanja vya ndani ya Jaganati, Lamaasi akasema, Mkuu wangu wa Kiyahudi, kweli ni nini? 3 Na Yesu akasema, Kweli ni kitu pekee ambacho hakibadiliki. 4 Katika ulimwengu mzima kuna vitu viwili; kimoja ni kweli; kingine ni hali ya uongo; na kweli ni kile kilicho, na uongo kile kinachoonekana kama. 5 Na kweli si kiasi chochote, na hakina sababishwaji, na wakati i ni sababisho la kila kitu. 6 Uongo ni chochote, na wakati ni madhihiriko ya kisicho chochote sura. 7 Chochote kilichofanyika kitarudia kinyume kufanyika; nakile chenye kuanza lazima kiwe na mwisho. 8 Vitu vyote ambavyo vyaweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu ni madhihiriko ya si kiasi chochote, ni kitu chochote, na hivyo kitapita zake. 9 Vitu tuvionavyo ni tu tafsiri ya fahamu za mwili kuonekana tu, wakati etha ikitetema hivi na vile, na hali ikibadilika hivyo hupotea kuonekana. 10 Pumzi Takatifu ni kweli; ni kile ambacho kilikuwa, na ndicho, na daima kuwa; haiwezi kubadilika na wala kupita zake. 11 Lamaasi akasema, unajibu vema; sasa, nini ni mtu? 12 Na Yesu akasema, Mtu ni kweli na uongo kwa namna ya ajabu kuchanganywa. 13 Mtu ni Pumzi kufanywa nyama, kwa hivyo kweli na uongo vimeunganishwa pamoja ndani yake; vyajitahidi nguvu pamoja, na ni chochote kwenda chini na mtu kama kweli abakia kukaa zaidi. 14 Tena Lamaasi aliuliza, nini usemacho kuhusu nguvu? 15 Na Yesu akasema, ni dhahiriko; ni matokeo ya kani; hiyo ni chochote; ni sura yenye kuonekana isiyo na kuwa hasa hadi kwa ndani; hakuna zaidi. Kani haibadiliki, ila nguvu yabadilika kadri vile kwa wakati etha ikibadilika. 16 Kani ni mapenzi ya Mungu na uweza wa yote, na nguvu ni hayo mapenzi katika madhahirisho, yakiongozwa na Pumzi. 17 Kuna nguvu katika pepo za kuvuma, nguvu katika mawimbi, nguvu katika kupiga kwa radi, nguvu katika mkono wa mwanadamu, nguvu katika macho. 18 Etha husababisha humo nguvu za kujakuwa, na neno fikara la Elohim, la malaika, mtu, ama kingine chochote chenye kufikiri, huongoza kani; inapokuwa imeshaifanya kazi yake nguvu haimo tena. 19 Na tena Lamaasi akauliza, je una nini cha kusema juu ya uelewa? 20 Na Yesu akasema, ni mwamba ambao mtu hujijengea mwenyewe; ni ginosia ya kisicho kiasi chochote na ya kilicho chochote cha kuwa, ya uongo na ya kweli. 21 Ni maarifa ya nafsi ya chini; kuzihisi fahamuni nguvu za wanadamu mwenyewe. 22 Na tena Lamaasi akauliza, una nini cha kusema juu ya hekima? 23 Na yesu akasema, ni ufahamu ya kwamba mtu ni kisicho kiasi chochote; ya kwamba Mungu na mtu ni moja; 24 Kwamba ulivyo kitu ni si kitu; kwamba nguvu ni tu sura isiyo kweli; kwamba mbinguni na nchi na kuzimu haviko juu, popote mahala, chini, ila ndani; ambavyo katika nuru ya kisicho kiasi chochote huja kuwa ni kitu chochote, na Mungu ni vyote. 25 Lamaasi akauliza, Kusali, imani ni nini? 26 Na Yesu akasema, Imani ni uhakika katika kweli ya uweza yote wa Mungu na mtu; hakika kwamba mwanadamu atafikia maisha ya kideifi*. 27 Wokovu ni ngazi ya kukwea kufika toka kwenye moyo wa mwanadamu hadi moyo wa Mungu. 28 Ina hatua tatu; Usadikifu ni kwanza, na hiki ni kile mwanadamu anachofikiri, labda ni kweli, 29 Imani hufuata, na hii ni kile mwanadamu yu ajua ni kweli. 30 Utunda ni wa mwisho, na huu ni mtu mwenyewe, kweli yenyewe. 31 Usadikifu kupotelea katika imani; na katika utunda hupotea; na mwanadamu aokolewa anapofikia maisha ya kideifi; ambapo yeye na Mungu ni moja.
***