Maslahi binafsi yanayohujumu harakati na maisha ya vijana

Bob Manson

JF-Expert Member
May 16, 2021
3,928
7,251
Huwenda nimechelewa kufahamu hili kwasababu ya umri wangu na uzoefu wangu, nimegundua Tanzania hakuna upinzani wa kweli.

Vijana wanapoteza maisha yao, wanaumizwa hata kupotezwa, yote ni kwasababu ya kupigania haki sambamba na kuwa upande wa upinzani, ajabu viongozi wao wanafanya mambo kwa maslahi yao binafsi.

Nimeshtuka japo nimechelewa, labda siku atokee kiongozi mwengine mfano wa TAL, lakini kwa sasa nawasihi vijana wenzangu kupambania ndoto zao, wasidanganyike na mienendo ya kisiasa hasa hasa upinzani.

Upinzani ambao umedhihirika kwamba hauna lengo la kweli bali kutetea matumbo yao na familia zao.
 
Mara nyingi watu unaowapenda ni kwasababu upo nao mbali .

Hata office uliyokuwa unatamani kuajiriwa siku umeingia unakuta wafanyakazi wanalalamika kuwa hawapo comfortable

Siasa ni Kama ilivyo maeneo mengine wapo ambao hufanya vizuri Sana na wapo ambao hawafanyi vizuri.

Upinzani wa kweli upo mkuu isipokuwa ambacho hakipo ni Vyama vya upinzani vya kweli.

Hata Ccm wakibaki peke yao lazima yataibuka makundi na kuanza kupingana hivyo upinzani wa kweli Tz UPO.

Kuhusu vijana kutumika na wanasiasa kwanza ni vijana wachache wenye uchungu na hii nchi wengi unaowaona kuna malengo nyuma yao wanayapambania.
 
ukiwa na ndoto, kusanya wajinga wakuunge mkono na kuwaaminisha unawapigania, kisha watumie kutimiza ndoto zako. Ndicho kinachoendelea sana afrika.
 
Dr habari mkuu...
Nje ya mada mkuu..
Siku hizi umekua adimu sana dactari...
 
Sahihi mkuu, ndyomaana nimesema labda atokee kiongozi mfano wa TAL, au hata yeye pia.

Lakini tofauti na hapo sioni kiongozi wa upinzani mwenye nia na lengo la kweli, nimegundua wengi ni mapandikizi ya watawala, hawaumii wala kujali wakiona vijana wanapoteza maisha yao kwa sababu yao.
 
Acha kuzunguka ww sema wazi mbowe katuangusha
 
Na hao wanaotekeleza hayo mauwaji bila hatia wao ni watakatifu au sio.
 
Hata huyo TAL ni kwakuwa upo nae mbali, hivyo kiti kabla haujakikalia na baada ya kukikalia ni tofauti
 
Kipimo cha kugundua TAL ni mtu sahihi ni vita anayopigwa na watawala.
Anafanya Kazi nzuri Sana na ana mawazo mazuri Sana .

Kitu anachohitaji Kwa sasa ni platform (jukwaa) ambalo yeye atalitumia kufanyia shughuli za kisiasa.

Na kuhusu kupigwa vita - TAL hapigwi vita na wazalendo anapigwa vita na wezi (mafisadi) .


Mbowe is a good guy Ila nafasi ya uenyekiti haimfai maana ni mfanya Biashara ambaye lazima awe interest fulani na watu weserikali ili mambo yamnyokee

Ila TAL hana cha kupoteza ni mtu ambaye ameweka maslahi ya Taifa mbele kuliko Maslahi yake.

Sio tu TAL anafaa kuwa mwenyekiti pia anafaa kuwa Rais wa nchi Kutokana na ukubwa wa potential yake.
 
Waache wawe busy na siasa kuja kushtuka miaka 47 hii hapa hakuna alochofanya
 
.

Sio tu TAL anafaa kuwa mwenyekiti pia anafaa kuwa Rais wa nchi Kutokana na ukubwa wa potential yake.
Mkuu naomba nikuulize, tofauti na TL ni kiongozi gani mwingine wa upinzani unadhani anafaa na kuwa na muelekeo kama alionao TL?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…