Masikini Ze Comedy Imekosa Legal Advice

Hatuna cha kuwasaidia..hii sheria imewakalia pabaya..inawakata shingo hawa moja kwa moja. Ila wanavuna walichopanda.
Si vyote uvunavyo katika maisha ulipanda .Wacha hizo.Vijana hawa ni wadogo wanahitaji msaada wako na wangu na wengine.
 
mimi naona hakuna kilichoharibika juu ya hilo jina the comedy majina yapo mengi waombe msaada tutawasaidia kuwapa majina, muhimu wahusika niwalewale tutazoea na hilo litakalokuja pia. tatizo lipo pale ambapo Manji anataka kuaproove kila shoo kabla ya kuonyeshwa ninavyojua mimi hii inafanyika kila mahali lakini shida ni huyu Manji atakosoa na kufuta chochote kitakachohusisha ufisadi na chochote juu chama tawala kwani ni jamaa zake wa karibu sana.
 
Maskini kina Masanja na wenziwe, hawa hawakujua sheria! walidhani umaarufu wao utabaki pale pale. Lakini hata kwa watu wanaofurahisha kama walivyokuwa wao mambo mara nyingine hubadirika. Si unakumbuka wale wakina Bishanga enzi zao? walibeba umaarufu sana wale. Lakini leo wako wapi?
Kila mahali unapokuwa katika kazi panakupa umaarufu wa aina fulani na nakwambia unaweza kutoka kwa kudhani umaarufu ule ule uliokuwa nao, utakuwa nao kumbe ndio kabisa kila kitu kikaisha.
Kama walivyodokeza wengi, nina mashaka kama hawa vijana wapya wa Manji ambao kisheria hatutakiwi kuwaita tena ze comedy wataendelea kufanya vitu vyao kwa uhuru ule ule waliokuwa nao. Maana nakumbuka hata Mengi alilalamikiwa na hawa mafisadi kwamba awazuie vijana hawa kufanya waliyokuwa wanafanya na akakataa. Sasa leo wako katika mikono yake si hapo ndio wamekwisha?
Mi nakwambia hakuna atakayeendelea kuangali upuuzi kama hawataendelea ku mantain trend ile ile waliyokuwa nayo walipokuwa EATV. Kama watabadilika kidogo na kudhani watu watafurahia kila kitu, wajue wamejimaliza wenyewe.
Tunataka kama wataendelea na ujasiri huo huo wamuigize huyo Manji kama fisadi namba mojana huyo Tido wao kama kibaraka wa JK na hapo tutawaaminia!
 
..sina sympath nao kabisa na acha wasote maana wakati mafisadi wanatumaliza wao ndio walikuwa PR machine yao!
 
Back
Top Bottom