Wewe unaongea hujui madhara ya kuondoka matajiri katika nchi, mpaka leo Uganda inabembeleza wafanyabiashara wake waliohama kwenda Uingereza na Canada enzi ya Raisi Iddi Amin lakini wapi, wameondoka na nguo zao lakini kwa sasa wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa katika nchi hizo. Wafanyabiashara, wawekezaji na hata wananchi wanapenda nchi salama na inaendeshwa katika misingi ya haki na sheria. Tizama mfano wa nchi iliyo karibu ya zimbabwe wananchi wake wengi wamekuwa wakimbizi Afrika ya kusini.Waende tu, tuzalisha matajiri wengine.