Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,038
- 4,752
Nimefuatilia utaratibu unaotumiwa na watendaji wanaohudumu kwenye mashirika ya kimataifa na kubaini Kwa hatua za awali mambo yafuatayo;
1. Mashirika haya yanakataa kulipa watu wanaofanya nao kazi stahiki zao Kwa wakati Kwa kisingizio kwamba wakilipwa hawafanyi kazi. Hii ipo zaidi kwenye posho za safari zinazohusu Watanzania.
2. Wapo watumishi wa Serikali au binafsi wanalipwa kinyume na miongozo ya kimataifa.
3. Wapo wafanyakazi wanafanya kazi miezi kadhaa bila kupatiwa stahiki zao.
4. Walipaji wana kauli za kuwaona weusi kama masikini wenye shida na kwamba wao watumishi wa madaraja ya juu.
Haya ni baadhi ya mambo wanayofanyiwa Watanzania; nawaita watafiti tuingie kazini kwenye miradi ya mashirika ya kimataifa tuone kama Hali iliyopo inaridhisha? Lakini pia niwaite kuwahoji zaidi watumishi wa umma wanalipwa stahiki zao Kwa wakati na viwango au wanatumikishwa Kwa vigezo kwamba Serikali inawalipa Mshahara?
Pesa zao nyingi wanajidai kukata kwenye msosi na mambo kama hayo unaambulia 30 Kwa siku na unawajibika kulipa hoteli..
Tuingie kazini kufanya utafiti kujua viwango na utaratibu tukilingana na Sera za ajira za kimataifa.