kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,718
- 14,152
Mitaa yetu ina giza nene totoro na vibaka wengi sana, na wakati mwingine hakuna umeme kabisa.
Ni jambo jema sana biashara kariakoo masaa 24, itasaidia kuchechemua uchumi wa watu, familia, jiji na taifa kwa ujumla. Usalama Kariakoo umeimarishwa kwa kufunga taa, kamera na kuwa na walinzi wa watu na mali zao wakiwa Kariakoo. Hata hivyo kuweka usala Kariakoo tu peke yake bila kufanya hivyohivyo na kwenye mitaa wanakoishi wananchi (wanunuzi/wateja) ni kuhatarisha usalama wao na mali wazilizozinunua usiku wa manane Kariakoo. Wataporwa watakapokuwa wanarudi nazo majumbani kwao kwenye mitaa yenye giza na isiyokuwa na kamera wala ulinzi wowote.
Tuache kukopi na kupesti matukio kutoka nchi za watu bila kuchota na kupesti mazingira ya matukio hayo huko mlikoyakopi.
Tujiandae kuona watu wakiporwa na kuumizwa wakati wakitoka Kariakoo saa 9 usiku kurudi majumbani kwao.