Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 600
- 1,508
Ni wazi kuwa Tanzania ipo katika msimu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandaa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi. Hii itafanywa kwa kushirikiana na vyama vya siasa, ikizingatia marekebisho yaliyofanywa Februari 2024 kuhusu ukatili wa kijinsia katika sheria za uchaguzi, yana lengo la kukabiliana na changamoto hizi kwa kuongeza ulinzi na usalama wa wagombea, hususan wanawake.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Ummy Nderiananga, alitoa maelezo katika Mkutano wa Bunge jijini Dodoma, akijibu swali la Mbunge Neema Lugangira kuhusu mchakato wa kanuni hizo. Alifafanua kuwa, Kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi kinataka Tume itoe kanuni hizo, na kwamba maadili ya uchaguzi yatatumika katika Uchaguzi Mkuu na chaguzi ndogo.
Tujadiliane hapa wadau.
Hatua hii itaboresha vipi mazingira ya uchaguzi?
Tujadiliane hapa wadau.
Hatua hii itaboresha vipi mazingira ya uchaguzi?