Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 26,432
- 19,236
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa Anaendelea kukonga na kukosha mioyo ya watu mbalimbali na mataifa mbalimbali, kutokana na uchapakazi wake pamoja na mapinduzi na mabadiliko mbalimbali ambayo amayaleta katika Secta na maeneo mbalimbali,ambapo yameleta nuru na mwanga katika Taifa letu.
Hii leo Marekani kupitia balozi wake hapa Nchini Balozi Michael Battle amemmiminia sifa na pongezi nzito sana Rais mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutoa na kuhamasisha vyombo vya habari kufanya uchunguzi na kutoa taarifa na ripoti ya Vitendo vya rushwa katika chaguzi zijazo.
Ambapo Balozi huyo wa Marekani Nchini amesema ya kuwa nguvu na uwajibikaji au wajibu wa vyombo vya habari katika kuwahabarisha wananchi ni nguzo au kichocheo cha kukua au kuimarika kwa demokrasia Nchini.
Ikumbukwe wakati huu wa Rais Samia vyombo vya habari vimekuwa huru sana katika kufanya shughuli zake,ikiwa ni pamoja na kuchunguza,kuandika ,kuchapisha na kusambaza habari pasipo vikwazo wala vitisho wala tishio la usalama kwa waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari.
Ndio maana huoni wala kusikia habari za waandishi kupigwa,kuteswa ,kuvunjiwa au kunyang'anywa vifaa vyao vya kazi,kufungiwa ,kulipishwa faini,kufungwa au kuwekwa mahabusu bila sababu. Waandishi wa habari wanafanya kazi zao katika mazingira ya kuheshimiwa na kutambuliwa sana,wanafanya kazi pasipo kuingiliwa wala kutishiwa uhai wao.
Ndio maana umma wa watanzania umekuwa ukipata habari mbalimbali zinazojiri hapa nchini kila siku,zilizo na uchambuzi wa kina na ufafanuzi wa masuala mbalimbali.Hii yote inatokana na dhamira njema ya Daktari wetu Samia Suluhu Hasssan kuweka dhamira ya dhati katika kuipa nguvu Secta ya habari kutekeleza na kutimiza Majukumu yake kwa uhuru kama sehemu ya kioo chake cha kujitizamia. Rais Samia na mama yetu mpendwa hataki kuendeshea serikali yake gizani,ndio maana amekuwa rafiki mkubwa sana na kipenzi cha wanahabari hapa Nchini.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.