gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 2,315
- 3,940
Ni uhuni,kisa mtu kakunyima mafuta yake unaanza fitna na kubaka mali zake,hiyo ndege ilinunuliwa lini,kabla au baada ya vikwazo!?..wakabariki malipo na wala si kwamba hawakujua,wamepora mali na hatch za wafanybiashara wa urusi,pesa za urusi wamepora,abramovic kaporwa chelsea kisa anajuana na putin na alipiga nae picha,huu wote ni uhuni, mamlaka simaanishi idhini ya mihimili yao ya uongozi,un ilipiga marufuku vita iraq, marekani akaanzisha vita iraq vilivyoivuruga dunia baadaeMsio na akili kila wakati mnakimbilia kutukana.
Tatizo uwezo wenu ni duni halafu mnaamini kuwa mna uelewa.
Huwezi kuiambia nchi yoyote ile kuwa eti haina mamlaka ya kuiwekea vikwazo nchi fulani kama kama ina sababu za msingi kufuatana na yale ambayo Taifa linayasimamia. Marekani imeweka vikwazo kwa nchi ya Venezuela kuwa hakuna kampuni, au mtu yeyote katika nchi yake anayeruhusiwa kufanya biashara na Venezuela, wewe unasema, haina mamlaka. Halafu bado unaamini una uelewa!! Kama Marekani ingeiambia Tanzania au Urusi isifanye biashara na Venezuela, hapo ungekuwa na hoja. Japo ina uwezo wa kusema kuwa nchi yoyote itakayofanya biashara na Venezuela, Marekani itaiwekea vikwazo. Maana yake itazuia makampuni ya nchini mwake kufanya biashara na nchi inayofanya biashara na Venezuela. Japo hilo halifanyiki mara nyingi.
Hata Tanzania, kama kuna sababu za msingi, kwa mfano wakati ule Malawi inaleta chokochoko dhidi ya nchi yetu, ingeweza kupitisha maamuzi kuwa tunaiwekea vikwazo Malawi. Maana yake hatununui na wala hatuuzi chochote Malawi. Na wala usingeweza kusema kuwa eti hatuna mamlaka ya kuiwekea vikwazo Malawi. Ukumbuke kuwa kwa nchi yenye mifumo ya utawala shirikishi, maamuzi hayo huwa ni maamuzi yaliyoridhiwa na mihimili ya utawala wa nchi kwa kuzingatia maslahi na tunu za Taifa.
Mtu wao kashindwa uchaguzi venezuela ndiyo wanapora mali