Marais wa Tanzania, kila mmoja anakuja na ajenda yake, hawana ajenda ya kuunganisha taifa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Licha ya marais wote wa Tanzania kutoka chama kimoja hakuna agenda ya jumla kila mmoja huja na gia yake na kuondoka na mdundo wake

Ukitaka kujua maendeleo endelevu ya taifa lolote, tizama ikiwa mipango ya utawala mmoja ni endelevu kwenye utawala unaofuata. Enzi za Nyerere ujamaa na kujitegemea ulishindwa akaondoka nao. Mwinyi akafanya kila kitu RUKSA akaondoka maisha ya mtanzania yakaboreka kiasi.

Mkapa akaleta ubinafsishaji holela wa mali za umma na kujilimbikizia mali akasahau hata ilani yake ya uchaguzi.

Jakaya Kikwete akaanza na kukopa hadi deni la taifa limekua mara mbili ya bajeti ya serikali.

Na huyu Magufuli naye kaja na "HAPA KAZI TU" licha ya nchi kuwa na utajiri wa rasli mali nyingi za Taifa kodi mbele kwa mbele na haimusi yoyote zaidi ila mwananchi wa kawaida ndie anayeumia zaidi licha ya kuja na kauli mbiu ya kutetea wanyonge.

Kati ya marais wote hakuna CONNECTION ya ajenda kubwa za kitaifa. Kila mmoja anaingia na gia yake na kutoka na mdundo wake.

Wananchi ni watizamaji na washangiliaji kwa makofi.
 
Mmeshabadilisha gia tena....sasa hivi ule wimbo wa CCM ni ile ile mmeukataa?
 
NI LAZIMA KATIBA IBADILISHWE HATA CCM WAZUIE KWA NAMNA GANI KWA KUHOFIA KIAMA CHAO. ILI PAWEPO NA AGENDA YA KITAIFA SIYO KILA KIONGOZI AJAYE AKILALA NA MKEWE WANASHAURIANA AU KIKUNDI FULANI.
NCHI YA KUSADIKIKA INA MAAJABU AMBAYO HAYAPO KTK SAYARI YA TATU.
 
Hakuna mabadiliko chanya tutaweza kuyapata ktk taifa hili kama hii kansa (ccm) bado itaendelea kuwepo, ccm wote pumzi imekata wanahitaji kupumzishwa ili zije akili mpya zenye kuwaza maslahi ya nchi badala ya maslahi ya kundi dogo kbs la walanguzi wa mali za umma
 
Ajenda ya sasa ni kutumia wataalamu wa IT kutoka Rwanda kwenye mifumo yetu ya kodi na fedha, hongera PK kwa kutusaida
 
Nchi haina dira, haijui kama ni ya kijamaa au ya kibepari. Viongozi hawana ilani wanachosimamia kama nchi badala yake utasikia ilani ya CCM. Hakuna ilani ya nchi?
 
Pamoja na CCM kuwa chama kikubwa ila hawajawahi kuwa na sera zinazowaunganisha.

Magufuli akiondoka hakuna atakayeikumba sera zake za viwanda.
 
Magu hajui hâta yupo mrengo gani,mara ujamaa,mara uliberali wa Chadema,mara ubepari wa viwanda
Mwigulu mjamaa,Mwijage mbepari, Lukuvj anapuyanga hovyo kunyanga'nganya watu mashambq yao sijui ni siasa za Mao Dze Dung karne ya ishirini na moja
Hakuna sera ya Taifa kila waziri anasubiri leo rais kaamkaje wamuigize
Hapa ndipo tulipofika chini ya mwaka mmoja na bado mingine minne
. Tutaisoma namba
Waulize ma DC waliotumbuliwa wanavyoisoma
 
01.Ujamaa na kujitegemea. .... 02.Ruksaaaaa...... 03.Ubinafsishaji.....04. Kilimo kwanzaaa 05. Tanzania ya viwandaaa 06. ????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…