Herbalist Dr MziziMkavu JF-Expert Member Feb 3, 2009 42,850 34,300 Jan 16, 2016 #1 Leo tunapika wali wa nazi, viazi vya kukaanga, mchemsho wa mboga za majani na samaki za kukaanga. Mahitaji: Mchele Tui la nazi Chumvi Viazi Kitunguu maji Zucchin karoti French beans Samaki Tangawizi Vinegar Ndimu Pilipili manga Mafuta ya kupikia. Hatua za kupika: Tuanze na wali wa nazi Tayarisha maji yenye tui la nazi na chumvi kidogo na uweke kwenye moto Osha mchele tayari kwa kupikwa Kabla maji hayajachemka, na yakiwa yamepata moto sana, ingiza mchele uliyo oshwa ndani ya sufuria Pika wali katika moto mdogo hadi uive Epua wali wako tayari kwa kuliwa. Tuje kwenye viazi vya kukaanga Menya maganda ya viazi Osha viazi tayari kwa kupikwa Weka viazi ndani ya sufuria yenye maji, chumvi kidogo na vitunguu tayari kwa kuchemshwa Chemsha viazi kiasi Epua viazi vyako na chuja maji uliyochemshia Chukua kikaangio na weka mafuta ya kupikia Kaanga viazi vyako mpaka vibadilike rangi ya brown na kuiva vyema Epua viazi vvyako tayari kwa kuliwa. Tupike mboga zetu Chukua zucchini, karoti, french beans na giligilani Katakata vipande vilivyo sawa Viweke ndani ya sufuria na maji kiasi na chumvi kiasi Chemsha kiasi na hakikisha visiive sana. Tumalizie na Samaki za kukaanga Safisha samaki vyema Katakata vitunguu swaumu na tangawizi na kisha viponde Katakata samaki kisha vichane kidogo kidogona kisu kuruhusu mchanganyiko uingie ndani ya samaki Changanya Vitunguu swaumu na tangawizi vilivyopondwa na ndimu, mafuta ya kupika, vinegar pamoja na vipande vya samaki Acha mchanganyiko huo uingie ndani ya vipande vya samaki kwa muda wa dk 30 - 45 Weka mafuta ya kupikia ndani ya kikaango na yaache yapate moto wa kutosha Ingiza vipande vya samaki ndani ya mafuta na kaanga mpaka vipate rangi ya brown na viive kabisa Epua samaki wako tayari kwa kuliwa. Mapishi ya wali wa nazi, viazi na samaki kaanga | Menu Time
Leo tunapika wali wa nazi, viazi vya kukaanga, mchemsho wa mboga za majani na samaki za kukaanga. Mahitaji: Mchele Tui la nazi Chumvi Viazi Kitunguu maji Zucchin karoti French beans Samaki Tangawizi Vinegar Ndimu Pilipili manga Mafuta ya kupikia. Hatua za kupika: Tuanze na wali wa nazi Tayarisha maji yenye tui la nazi na chumvi kidogo na uweke kwenye moto Osha mchele tayari kwa kupikwa Kabla maji hayajachemka, na yakiwa yamepata moto sana, ingiza mchele uliyo oshwa ndani ya sufuria Pika wali katika moto mdogo hadi uive Epua wali wako tayari kwa kuliwa. Tuje kwenye viazi vya kukaanga Menya maganda ya viazi Osha viazi tayari kwa kupikwa Weka viazi ndani ya sufuria yenye maji, chumvi kidogo na vitunguu tayari kwa kuchemshwa Chemsha viazi kiasi Epua viazi vyako na chuja maji uliyochemshia Chukua kikaangio na weka mafuta ya kupikia Kaanga viazi vyako mpaka vibadilike rangi ya brown na kuiva vyema Epua viazi vvyako tayari kwa kuliwa. Tupike mboga zetu Chukua zucchini, karoti, french beans na giligilani Katakata vipande vilivyo sawa Viweke ndani ya sufuria na maji kiasi na chumvi kiasi Chemsha kiasi na hakikisha visiive sana. Tumalizie na Samaki za kukaanga Safisha samaki vyema Katakata vitunguu swaumu na tangawizi na kisha viponde Katakata samaki kisha vichane kidogo kidogona kisu kuruhusu mchanganyiko uingie ndani ya samaki Changanya Vitunguu swaumu na tangawizi vilivyopondwa na ndimu, mafuta ya kupika, vinegar pamoja na vipande vya samaki Acha mchanganyiko huo uingie ndani ya vipande vya samaki kwa muda wa dk 30 - 45 Weka mafuta ya kupikia ndani ya kikaango na yaache yapate moto wa kutosha Ingiza vipande vya samaki ndani ya mafuta na kaanga mpaka vipate rangi ya brown na viive kabisa Epua samaki wako tayari kwa kuliwa. Mapishi ya wali wa nazi, viazi na samaki kaanga | Menu Time
P PhD JF-Expert Member Jul 15, 2009 4,667 3,840 Feb 24, 2016 #4 inahitaji uwe na pesa kama trump ili ule huo mlo, kwa namna magu alivyobana pesa sa hivi tunakula dagaa na bamia daily , cholestrol free
inahitaji uwe na pesa kama trump ili ule huo mlo, kwa namna magu alivyobana pesa sa hivi tunakula dagaa na bamia daily , cholestrol free