Mapendekezo: Serikali ipitie upya Sheria ya Usalama wa Taifa na TISS iundwe upya kwa maslahi ya taifa

Nisiingie ndani sana lakini kipindi cha kuanzia 2015 kulifanyika maboresho mengi japo yamepata upinzani mkubwa kutoka kwa "wakongwe"(hawa ndo walikuwa wavujisha siri) lakini nia ilikuwa kuimarisha taasisi.

Mf.
Taasisi ilijaa undugu(kama baba ni TISS basi watoto na ndugu ndo watapata nafasi)

Ilifikia hatua walikuwa hawako kwa kificho tena .wakienda sehemu za starehe walikuwa wanajinadi na silaha zao za moto.

Kwenye awamu ya 5, ndio kipindi ambapo taarifa zao zilikuwa zikifanyiwa kazi kuliko kipindi chochote kile.
Huo ni uongo kabisa wakati katika awamu ya tano ndo Mambo ya kuchukua taarifa za watu na kuwapa wakuu mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, mawaziri na wajinga wajinga wengine wavimbe nazo kwenye majukwaa ya siasa au mtandaoni......huyo Magufuli nae hata usimsifie vipi alikuwa hana lolotee
 
Shida ya hii nchi ni imperial presidency, na haikuanza leo bali ilianza tangu zama za Mwalimu Nyerere.

Imperial Presidency imevifanya vyombo vyote vya serikali, ikiwemo TISS, viwajibike zaidi kwa maslahi ya Rais kuliko kulinda maslahi mapana ya taifa. Mbaya zaidi, hata Bunge na Judiciary navyo vinaitumikia executive. Rejea kisa cha Job Ndugai kuachia uspika kilivyoanza hadi kufanikishwa.

Vilevile, Katiba yetu ndio iliyomfanya Rais kuwa imperial na asiyeweza kushitakiwa kwa lolote lile. Rais ni kama mungu-mtu hapa Tanzania coz hakuna effective mechanism ya kumwajibisha hata akikosea.

Hitimisho langu ni kwamba, TISS haiwezi kuboreshwa na kuwa bora, hadi tutakapoamua kuweka Katiba na Sheria zinazomlazimisha Rais kuwajibika kwa Wananchi kimatendo. Mfano, sasa hivi DG-TISS ni direct appointee wa Rais bila kupitia vetting mahsusi ya kibunge. Hii ina maana kwamba, hata akiteuliwa mwingine bado atamtumikia Rais kwanza, then nchi baadae.
 
Who do you trust kufanya hilo? Ndio mambo ya katiba, wanaopiga kelele za katiba wote wana ajenda binafsi si za wananchi. Ulimwengu huu unayoona kwa macho sio uhalisia behind the scene.

But I believe one day, watu wenye hofu halisi ya Mungu watasimama na kuirudisha nchi kwenye mstari. Tumuombee mama avae ujasiri wa Bikira Maria na atamke "mimi ni mtumishi wa Bwana nitendewe kama ulivyonena" na asiwe Eva aliyetwaa tunda akala akampa na Adam mission ya Lucifer ikawa accomplished na kutwaa madaraka yao na vizazi vyao.

Yes of Mary to God ( through Gabriel) ndicho mbingu na malaika zake walisubiri kwa hamu for the mission of salvation to start and refute Yes of Eve to Lucifer.

Watch and pray
 
Who do you trust kufanya hilo? Ndio mambo ya katiba, wanaopiga kelele za katiba wote wana ajenda binafsi si za wananchi. Ulimwengu huu unayoona kwa macho sio uhalisia behind the scene.

But I believe one day, watu wenye hofu halisi ya Mungu watasimama na kuirudisha nchi kwenye mstari. Tumuombee mama avae ujasiri wa Bikira Maria na atamke "mimi ni mtumishi wa Bwana nitendewe kama ulivyonena" na asiwe Eva aliyetwaa tunda akala akampa na Adam mission ya Lucifer ikawa accomplished na kutwaa madaraka yao na vizazi vyao.

Yes of Mary to God ( through Gabriel) ndicho mbingu na malaika zake walisubiri kwa hamu for the mission of salvation to start and refute Yes of Eve to Lucifer.

Watch and pray
Hadithi hizo za watch and pray inabidi ukawahadithie ndugu na jamaa zako wa karibu
 
Kinachoniuma Ni sisi vijana wazalendo tumesoma na tunasifa za kuwa katika hizo taasisi na tunania ya thati Ila hatupewi nafasi,kila ukijaribu kuhangaikia hupati,au kwa vile sisi tunatoka familia nasikia.
Kama muhusika utasoma hii jumbe nahitaji msaada wako,sifa ninazo na uwezo ninao,nimejaribu kusoma article za idara za usalama za
Russia
Rwanda
Uganda
USA
Na usalama wa ndani wa jwtz nimeona Nina baathi ya sifa hizo.tusaidiane sio kila siku muchukue watoto wenu tu na sisi masikini tubebeni,wengine sio fedha tu Ila Ni wazalendo wa kweli,yapo mengi nimeyaona na yanaumiza sana lakin no way out.
Umejuaje kama una sifa za kuwa huko, au uliona wapi sifa za mtu kuwa huko mpaka ukadhani na wewe ni miongoni mwa watanzania wanaotakiwa kuwa huko. Yani kusoma vipeperushi uchwara ushajiona una sifa mkuu??!!!
 
Umejuaje kama una sifa za kuwa huko, au uliona wapi sifa za mtu kuwa huko mpaka ukadhani na wewe ni miongoni mwa watanzania wanaotakiwa kuwa huko. Yani kusoma vipeperushi uchwara ushajiona una sifa mkuu??!!!
Hana nimekuambia nikicompare na article nilizosoma
 
Usalama, amani, maendeleo na ustawi wa nchi yoyote hutegemea sana utendaji wa idara ya usalama wa Taifa.

Idara hii ndiyo yenye dhamana ya kukusanya na kuchambua taarifa zote za kiitelejensia zinazohusu siasa, uchumi, ulinzi na usalama na kisha kuishauri serikali hatua za kuchukua na au kupanga mikakati yake

Ukifuatilia historia ya vyombo vya usalama duniani utatambua kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizokuwa zikisifika barani Afrika kwa kuwa na idara bora ya usalama wa Taifa, Ubora huo ulijidhihirisha wakati wa vita vya ukombozi wa kusini mwa Afrika, katika vita vya Kagera vilivyomtoa nduli Idd Amin, na katika ukombozi na ulinzi wa Congo DRC, na visiwa vya Shelisheli.

Katika kipindi cha utawala wa hayati rais John Pombe Magufuli idara ya usalama wa Taifa (TISS) chini ya DG Diwani A. Msuya ilionesha kulegalega katika utendaji wake, kushindwa kuishauri vema serikali, na hasa mheshimiwa rais katika masuala muhimu ya kiuchumi, sheria, diplomasia, na usalama kwa ujumla.

Tukirudi nyuma TISS chini ya Diwani Athumani Msuya ilifanya maamuzi ya kufikirisha sana ambapo angekuwa katika mataifa yanayotambua jukumu la taasisi hii katika nchi basi alipaswa kujiuzulu ama kubadilishwa mapema sana kuinusuru idara hii nyeti;

Kwanza; Taarifa nyeti zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kila siku, ilikuwa ni udhaifu mkubwa mno kwa idara hii nyeti kwa taifa.

- Kimsingi (TISS) ndiyo inayopaswa kuhakikisha siri za serikali hazivujishwi hovyo, nyaraka za serikali zinatunzwa ipasavyo, na watendaji wanafanya kazi zao kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za nchi. Kinyume chake TISS ilionesha udhaifu mkubwa katika kutunza na kudhibiti siri za serikali, na hata kuwadhibiti maafisa wake, achilia mbali watumishi wengine wa umma.

- Ingawa tatizo hili (la uvujishaji siri) kwa watu wa kawaida linaweza kuonekana dogo, madhara yake ni makubwa mno. Kwa ujumla, hiki ni kiashiria tosha kuwa ndani ya idara kuna maafisa wasio waaminifu, na walio tayari kutumika kwa namna moja au nyingine. Afisa aliye tayari kutoa taarifa isiyo na uzito mkubwa bure, kwa sababu yoyote ile, hawezi kusita kutoa siri kuu kama akiahidiwa kulipwa donge nono.

Pili; Udhaifu wa idara pia ulijidhihirisha wakati aliyekuwa rais wa JMT hayati John Pombe Magufuli alipoanza kuugua na kutokuonekana hadharani kwa takribani wiki nzima.

- Katika hali isiyo ya kawaida taarifa za ugonjwa wake zilisambazwa katika mitandao ya kijamii (kwa namna isiyofaa) kana kwamba kiongozi huyo hakuwa kiongozi wa kitaifa. Hata rais Magufuli alipofariki, dunia nzima ilijua siku kadhaa kabla serikali ya Tanzania kutangaza taarifa rasmi, jambo ambalo ni aibu kwa taifa.

Tatu; Idara pia inalaumiwa kwa kumshauri rais Magufuli vibaya, na mara nyingine kumuacha atoe taarifa za upotoshaji kwa malengo binafsi au ya kisiasa kitu ambacho ni kinyume na utendaji wa idara hii inayoaminiwa na serikali.

- Mfano ulikuwepo ushahidi wa kutosha kuwa baadhi ya mitambo ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na TANESCO iko katika hali mbaya mno kutokana na kutofanyiwa matengenezo (service) kwa muda mrefu kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Na endapo mitambo hiyo haitashughulikiwa mapema TANESCO inaweza kulazimika kuizima ili kunusuru isiungue, na hivyo kusababisha kuwepo kwa mgao wa umeme katika baadhi ya mikoa, au nchi nzima.

- Hadi sasa tunavyoshuhudia mgawo wa umeme katika baadhi ya maeneo nchini haya yote yametokana na ushauri mbovu uliotolewa na TISS kwa rais Magufuli kiasi cha kumsukuma kuvuruga mipango ya shirika hilo kwa manufaa ya kisiasa.

- Idara pia imeshindwa kumshauri rais wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan katika teuzi zake, ama kufanya upekuzi sahihi (vetting) za wateule ambao rais alitaka kuwapa madaraka “ tukumbuke uteuzi na utenguzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) bwana, Thobias Richard ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu kuteuliwa kwake” na baadhi ya teuzi ambazo zimekuwa na makosa mbalimbali.

- Pia udhaifu huo umesababisha watu wasio na sifa stahiki, na hata matapeli na mafisadi waliowahi kufikishwa mahakamani (kwa utapeli) kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa serikalini hasa awamu hii ya sita.

Maoni na ushauri;

1. Kwa vile uongozi wa TISS uliopo madarakani umeonesha udhaifu katika utendaji kazi, ingefaa mheshimiwa rais (kama itampendeza) kufanya mabadiliko ya uongozi. Mabadiliko hayo yanafaa kuanzia kwa kuteua mkurugenzi mkuu (DGIS) mwingine toka ndani ya idara.

- TISS ina hazina kubwa ya maafisa wenye weledi na uwezo wa hali ya juu wapo maafisa kama Suleiman Abubakar Mombo aliyekuwa nje katika moja ya balozi zetu, Huyu ana uwezo mkubwa wa uongozi na utendaji kazi na kama si majungu ya idara na mitaani huwenda angeteuliwa kuwa DGIS miaka mingi iliyopita.

- Pia kuna Makungu Msalika aliyekuwa naibu DGIS lakini akaondolewa kutokana na mvutano kati yake na aliyekuwa DGIS kipindi cha nyuma mchungaji Modestus Kipilimba na kupelekwa kuwa RAS katika moja wapo wa mkoa hapa Tanzania.

- Pia kulikuwa na James Kaji aliyewahi kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais, na Kamishna wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya, huyu alikuwa ni afisa mwenye uwezo na weledi wa kuweza kuiongoza TISS kwa mafanikio makubwa, ila majungu na fitina zilimuondosha Idarani.

- Hawa pamoja na wengine wengi walio ndani ya idara wana uwezo wa kuiongoza idara kwa weledi na kuondoa madhaifu yaliyopo.

2. Mfumo wa utendaji kazi wa idara hiyo ufumuliwe na kujengwa upya. Idara ipewe nguvu na iwezo wa kufanya kazi yake kwa uhuru pasipo kuburuzwa narais au viongozi wengine waliopo madarakani.

- Ingawa TISS inapaswa kuonesha utii kwa rais kama ilivyo kwa vyombo vingine vya dola, ipewe wigo mpana wa kufanya majukumu yake kwa kufuata sheria na malengo yake, badala ya kutumika kama chombo cha rais kwa manufaa ya rais.

- Kwa kifupi Idara iwe mlinzi wa katiba na si mtu binafsi au watu.

3. Idara iboreshe utaratibu wa kuwafanyia upekuzi (vetting) watu inaotaka kuwaajiri katika ofisi zake, na idara nyingine za serikali. Watu wanaopungukiwa sifa za kuwa maafisa wa idara wasipewe nafasi hata kama ni watoto au ndugu wa vigogo au maafisa wa idara.

- Sambamba na hili idara iwapatie mafunzo ya ziada (re-flesher course) maafisa waliopata mafunzo ya mkurulo (Voda Faster) na wale waliokaa kazini miaka mingi bila kupatiwa mafunzo mengine. Hii itasaidia kuboresha utendaji wa maafisa wa idara na kuliondolea taifa aibu iliyopo sasa.

Wako katika ujenzi wa taifa;
…..
TISS ya wapi? Tz hakuna TISS, kuna vijana wa timu msoga tu.
 
Back
Top Bottom