Mapendekezo kwa Serikali: Jinsi ya kuimarisha shilingi ya Tanzania

Cha msingi turekebishe sheria zetu zinazoruhusu matumizi ya dollar nchini. Sheria hizi ni za madini na utalii. Mahoteli na madini zote zitatoza shilingi hivyo kuwa highly demanded na dollar kuwa supplied. The higher the demand the higher the price na kinyume chake. Wote watakao toza dollar watashughurikiwa na kuifanya shilingi kuwa ya thamani kubwa.

Kumbuka dollar ni sarafu kubwa kuichanganya na shillingi kwenye uchumi mmoja lazima sarafu dhaifu shilingi itayumba. Mengine ya balance of trade yatakuja baadaye lakini lazima nyumba yetu iwe in order. Matumizi ya shilingi maeneo yote iwe wimbo wetu.
Baby kumbe unafanya biashara ya mikeka ntakutafuta tuongee biashara.
 
Natafuta sana mikeka ntakutafuta baby tufanye biashara.
 
Hapana maduka yawepo tu lakini hakuna manunuzi ya aina yeyote yatakayo fanyika kwa kutumia dollar. Si nyumba za kupanga, hoteli, huduna za kitaalamu nk. Ukija na dollat ili uishi badilisha kwanza ziwe shilingi. Hapo ndipo shilingi itasakwa kama lulu!!

Mkuu, umesema kuwa maduka ya kubadili fedha yaendelee kuwepo lakini @ikipendaroho ameeleza kuwa maduka ya kubadili fedha yanafanya biashara kama biashara nyingine na inakuwa governed by demand and supply policy na mwenye kuuza fedha za kigeni anaweka faida ya Tsh. 5 - 20 kwa dola au tuseme kwa kila fedha ya kigeni.

Wateja wa kununuwa wanapozidi wao hupandisha bei ya kununulia na matokeo yake bei ya kuuzia inazidi. Inapotokea wateja wa kununua kidogo na hela za kigeni anazo nyingi, anaogopa fedha za kigeni kumlalia na bei kuporomoka akala hasara. Na matokeo yake bei ya kununulia inaanguka kwa vile hana uhakika siku chache zijazo rate itaanguka au kupanda kiasi gani.

Sasa kuruhusu kuendelea kuwepo kwa maduka ya kubadili fedha huoni kuwa kunaweza kuchangia kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu ya Tanzania?
 
biashara ya kuuza change, kununua noti chakavu inashusha sana thamani ya shilingi huyu gavana amekaa picha tu hafanyi kitu
 
Mkuu, umesema kuwa maduka ya kubadili fedha yaendelee kuwepo lakini @ikipendaroho ameeleza kuwa maduka ya kubadili fedha yanafanya biashara kama biashara nyingine na inakuwa governed by demand and supply policy na mwenye kuuza fedha za kigeni anaweka faida ya Tsh. 5 - 20 kwa dola au tuseme kwa kila fedha ya kigeni.

Wateja wa kununuwa wanapozidi wao hupandisha bei ya kununulia na matokeo yake bei ya kuuzia inazidi. Inapotokea wateja wa kununua kidogo na hela za kigeni anazo nyingi, anaogopa fedha za kigeni kumlalia na bei kuporomoka akala hasara. Na matokeo yake bei ya kununulia inaanguka kwa vile hana uhakika siku chache zijazo rate itaanguka au kupanda kiasi gani.

Sasa kuruhusu kuendelea kuwepo kwa maduka ya kubadili fedha huoni kuwa kunaweza kuchangia kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu ya Tanzania?

Tunasema kuwa maduka ya pesa yaendelee tu ila humu nchini ukitaka kununua chochote kile kiwe kwa shilingi na ni kosa kubwa kutumia sarafu ya nchi nyingine. Kwa mfano umeenda kulala Serena Hotel unakuta chumba ni Tzs250,000 inabidi ulipe shilingi hiyo na fedha uliyonayo ya kigeni uibadili kulipia huduma hiyo. Iwapo hoteli itakuwa na sehemu ya kubadilishia itabidi ufanye hivyo.

Tunachopinga kwa nguvu zote ni pale ambapo niko mtaani huku Mikocheni, Mbezi Beach nk mtu anasema anapangisha kwa US$ hapa ni kosa kubwa. Ukiwa ndani ya Tanzania bei ni zote ziwe kwa shilingi. Ikiwa hii itasimamiwa utaona automatically bei ya shilingi inaanza kupanda kutoka TZS2,150 hadi tuseme TZS1,100 kwa US$.

Bureau De Change zinauza kulingana na soko la sarafu (demand and supply) hivyo zitaji adjust tu. Ukienda nchi za watu na una dollar yako hupati huduma hadi ubadili. Lakini kwetu hapa mtu anapokea na anaenda baadaye kubadili. Hii tabia iachwe mara moja na tujivunie shilingi yetu. Kwa sasa ni vingumu kwa sababu serikali inaipendelea dollar sehemu kubwa kuliko shilingi. Mbona TRA wanatoza shilingi tu iweje wizara ya Nishati na Madini na utalii wang'ang'anie pesa ya Obama badala ya kwetu?
 
Hivi karibuni tumeshuhudia shilingi yetu ya Tanzania ikishuka thamani kwa zaidi ya asilimia 20 kiwango ambacho ni kikubwa sana na mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuimarisha shilingi hiyo.

Kutokana na hali hiyo nimeona ni vyema nikaanzisha uzi huu ili tuweze kupeleka mawazo yetu kwa serikali ya Magufuli juu ya mambo ambayo yanapswa kufanywa ili shilingi yetu ya Tanzania iweze kuimarika.

Miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha kuporomoka kwa shilingi yetu ya Tanzania ni balance of trade ambapo hapa tunaona kuwa nchi yetu inatumia bidhaa nyingi sana za nje kuliko za ndani na inauza bidhaa zake nje kwa kiasi kidogo.

Kutokana na hali hiyo ninapendekeza serikali ya Magufuli ipige marufuku uingizaji na matumizi ya bidhaa za nje ambazo sisi Watanzania tuna uwezo wa kuzizalisha na kuagiza tu zile bidhaa ambazo hatuzalishi na ambazo tuna uhitaji nazo na badala yake serikali itilie mkazo katika matumizi ya bidhaa za ndani ambazo tunazalisha sisi wenyewe.

Endapo serikali itachukua hatua hii kama hatua ya awali ya kuimarisha shilingi yetu itasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania wakati hatua nyingine za kuongeza uwekezaji na viwanda zikifuata.

Nakaribisha mawazo yenu wadau na wazalendo wa nchi yetu juu ya namna ambavyo tunaweza kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania.
Pia mimi nigeshauri wapige marufuku kwenye maduka kuweka price ya vitu kwa dola iwe ni Tsh only hapo tutaweza imarisha shilingi yetu ukija tanzania na dola zako utaziacha aiport na kuchukua Tsh
 
Tunasema kuwa maduka ya pesa yaendelee tu ila humu nchini ukitaka kununua chochote kile kiwe kwa shilingi na ni kosa kubwa kutumia sarafu ya nchi nyingine. Kwa mfano umeenda kulala Serena Hotel unakuta chumba ni Tzs250,000 inabidi ulipe shilingi hiyo na fedha uliyonayo ya kigeni uibadili kulipia huduma hiyo. Iwapo hoteli itakuwa na sehemu ya kubadilishia itabidi ufanye hivyo.

Tunachopinga kwa nguvu zote ni pale ambapo niko mtaani huku Mikocheni, Mbezi Beach nk mtu anasema anapangisha kwa US$ hapa ni kosa kubwa. Ukiwa ndani ya Tanzania bei ni zote ziwe kwa shilingi. Ikiwa hii itasimamiwa utaona automatically bei ya shilingi inaanza kupanda kutoka TZS2,150 hadi tuseme TZS1,100 kwa US$.

Bureau De Change zinauza kulingana na soko la sarafu (demand and supply) hivyo zitaji adjust tu. Ukienda nchi za watu na una dollar yako hupati huduma hadi ubadili. Lakini kwetu hapa mtu anapokea na anaenda baadaye kubadili. Hii tabia iachwe mara moja na tujivunie shilingi yetu. Kwa sasa ni vingumu kwa sababu serikali inaipendelea dollar sehemu kubwa kuliko shilingi. Mbona TRA wanatoza shilingi tu iweje wizara ya Nishati na Madini na utalii wang'ang'anie pesa ya Obama badala ya kwetu?

Asante sana mkuu kwa mawazo yako mazuri. Una wazo jingine tofauti na hili ambalo unahisi linaweza kuchangia katika kuimarisha thamani ya shilingi yetu?
 
Natamani shillingi ibaki kuwa chini, imesaidia sana biashara yangu za kusafirisha mikeka na majamvi.

Hivi kwanini haswa unataka shillingi ipande? Hususan unapotaka tuuze sana nje.
kwahiyo kuanzia sasa unatambulika kama " bibi mikeka " a.k.a "bibi majamvi" bin "bibi tarabushi."
 
Kutokana na hali hiyo ninapendekeza serikali ya Magufuli ipige marufuku uingizaji na matumizi ya bidhaa za nje ambazo sisi Watanzania tuna uwezo wa kuzizalisha na kuagiza tu zile bidhaa ambazo hatuzalishi na ambazo tuna uhitaji nazo na badala yake serikali itilie mkazo katika matumizi ya bidhaa za ndani ambazo tunazalisha sisi wenyewe.
Kupiga marufuku kuagiza vitu haiwezekani kuna sheria za kimataifa za biashara zinazozuia kufanya hivyo .Ukifanya hivyo nchi zile ambako tunapeleka bidhaa zetu nao watalipa kisasi kwa kupiga marufuku bidhaa za kutoka Tanzania zisiingie nchini kwao.

Kinachoweza kufanyika ni kupunguza Demand ya dola kwa kuzuia dola kutumika nchini kwa shughuli zozote za biashara iwe kupangisha nyumba,kununua bidhaa nk

Hatua ingine ni kuhamasisha watanzania wazalishe bidhaa nzuri ili watanzania wenzao wapende kuzinunua itakuwa haina maana upige marufuku bidhaa watu wasinunue toka nje wakati wazalishaji wa ndani ni wababaishaji,matapeli na wazalishao bidhaa zisizokuwa na ubora.Wazalishaji wa ndani wakae wajitafakari waelewe kwa nini wazawa hawataki bidhaa zao watafute solution kwa kuzalisha bidhaa nzuri zinazokubalika sokoni na wateja si kwa ubora tu bali na kwa wingi pia.Inakuwa haina maana unakuta mfano mtu anazalisha sabuni miche mia kwa siku hata kama ina ubora haikidhi soko.Uzakishaji wetu hata kama upo haukidhi mahitaji ya soko.Soko kubwa kuliko uwezo wa uzalishaji hivyo kupelekea uagizaji toka nje.

Hatua ingine iwe ni kuhamasisha watu kuwa wazalendo wapende nchi yao na kununua vitu vilivyozalishwa nchini mwao.Nashangaa VISHIRIKA VISIVYO VYA kiserikali vingi hujikita kwenye vitu vya ubabaishaji eneo hili la uhamasishaji watu kuwa wazalendo wapenda nchi na vidhaa zake na huduma zake ni la muhimu sana tena sana.Watu wakihamasika watanunua.Wahindi wamehamasika hupenda kuvaa nguo za kihindi zilizozalishwa na wahindi,Wanigeria vivyo hivyo.Watu wakihamasika basi itasaidia kupunguza demand ya vitu vya nje.

Pia serikali inatakiwa iongeze kodi kwenye mafuta hasa ya magari madogo yanayotumia petrol.Sehemu kubwa ya mafuta yanayoagizwa nje ni kwa ajili ya petrol.Kupunguza matumizi ya hayo magari serikali iweke kodi juu sana kwenye mafuta ya petrol watumiaji wakipungua demand ya hela za kigeni kuagiza mafuta ya petrol itashuka

Lingine ni kuweka kodi kubwa sana kwenye mavazi mapya sio mitumba.Mtu kama anaweza kununua kiatu cha laki moja dukani serikali iangalie hilo eneo.Vitu vya anasa mfano maredio,matv,nguo kama masuti toka ufaransa sijui italy sijui wapi serikali ipige kodi kubwa hasa.Pia kodi kwenye vinywaji toka nje serikali ipige kodi kubwa.Ndani ya nchi kuna cocacola lakini mtu unakuta anataka kunywa iliyotoka nje ya nchi hapo ndipo pa kumpata.Vitu vyote vya anasa serikali ibane kwa kutumia kodi

Eneo lingine na la ushuru wa magari madogo na spare parts za magari madogo.Serikali itwange kodi ya uhakika ku-discourage imports

Lakini pia udhibiti wa safari za nje ya nchi pia unasaidia kupunguza demand ya hela za kigeni
 
Asante sana mkuu kwa mawazo yako mazuri. Una wazo jingine tofauti na hili ambalo unahisi linaweza kuchangia katika kuimarisha thamani ya shilingi yetu?

Mawazo mengine ni kupambana na mtandao haramu wa utakatishaji fedha ambao husababisha shilingi kushuka ghafla na kuathiri mfumo mzima wa soko huria.
Biashara za madawa ya kulevya zikithibitiwa na watu wote ndani ya uchumi wetu kutumia shilingi katika mahitaji ya kila siku ikiwemo mishahara ya wageni walio wengi tutaimarisha mno sarafu yetu. Wengi mishahara yetu ni kwa $$ ili kuzuia kuyumba kwa uwezo wa kununua (purchasing power) kwa sababu ikiwa kama mshahara wangu ulikuwa Tzs4.2million kwa rate ya Tzs1,600 nilkuwa na uwezo wa kubadili na kupata US$2,625 ghafla rate inakuwa Tzs2,100 kwa dollar moja hivyo ninapata $2,000 na kupoteza $625 ($2,625-2,000). Hii ni mshituko mkubwa kwa wale wanaopokea shilingi tu bila ku hedge (kukinga) na madhara ya kutosimamia sarafu. Unategemea iweje kwa huyu mfanyakazi? Atabuni mbinu ya kupambana na upotevu wa purchasing power ambayo itakuwa siyi mzuri kiuadilifu!
 
KUPANDISHA SHILINGI YETU MPAGO AMBAO NI REALISTIC NA NINAUONA UNATEKELEZEKA KIRAHISI SANA NI KILIMO, TUKILIMA KILIMO KIZURI CHA UMWAGILIAJI PAMOJA NA UFUGAJI, KWA KUTUMIA ADVANTAGE YA MVUA NA MITO NA MABONDE YA HAPA KWETU TUTAFANYA EXPORT NYINGI SANA ZA KUINUA SHILINGI YETU, NCHI ZINAZOTUZUNGUKA KAMA KENYA BURUNDI, RWANDA TUTAWAUZIA SANA KWA KUA WAO WANA ENEO DOGO NA KAMA KENYA HIVI ENEO LAO HASA KASKAZINI NI KAMA JANGWA, HAYA MAMBO YA KUSEMA KUSUBIRIA KUFUFULIWA VIWANDA NA WAKATI TEKNOLOJIA YA KISASA YENYE UFANISI WA KUSHINDANA NA VIWANDA VYA NJE, HATUNA NA UMEME WENYEWE WANASEMA GESI, GESI KILA SIKU TUSIYATEGEMEE WAKUU, TANZANIA INA ADVANTAGE YA KUWA NA MAJI MENGI YA MVUA MITO NA MAZIWA, NGUVU KAZI KUBWA (WATU MIL 50), NA ENEO KUBWA PAMOJA NA UTULIVU, BANDARI KWENYE MAZIWA PAMOJA NA MAZIWA TUKIAMUA KUTUMIA VITU HIVI KUWEKEZA KWENYE KILIMO KWA UFANISI, SHILINGI YETU ITAPANDA SANA, TUMEKOSA TU VIONGOZI WAZURI NA WANANCHI WAVIVU WA KUFIKIRI NA KUFANYA KAZI, ILA TUKIAMUA TUTAFIKA MBALI
 
Mimi nianaamini kwamba, mbali na kujitahisi kuzalisha bidhaa nyingi hapa hapa kwetu, pia watanzania tuelimishwe umuhimu wa kuthamini vya nyumbani kuliko vile vinavyotoka nje. Watanzania Tukijenga tabia na utamaduni wa kuzipendelea bidhaa zetu pale tunapofanya manunuzi, ninaamini shilingi itaimarika. Faizafoxy anatamani shilingi iendelee kushuka kwa maslahi yake binafsi, hii ni utovu mkubwa sana wa uzalendo. Mimi kwenye profession yangu ninalipwa kwa dola, pamoja na kwamba kuanguka kwa shilingi kunaniweka kwenye nafasi nzuru zaidi ya kufaidi, lakini kwasababu za kizalendo siwezi kupenda hali hiyo iendelee kutokea. Faizafoxy, tafadhali badilisha mtazamo wako. Shilingi inapoimarika maisha ya watu yanaboreka.
 
Nashukuru kwa mawzo yako mkuu, wadau hapo juu wamependekeza zuio la baadhi ya bidhaa ambazo sisi tuna uwezo wa kuzizalisha na sio bidhaa zote. Je kuna athari yoyote kwa kukataa kuingiza bidhaa kutoka nje amabazo tuna uwezo wa kuzizalisha?

Binafsi naona kama tusipozuia uingizaji wa bidhaa amabazo tuna uwezo wa kuzizalisha itakuwa ngumu sana kuwashawishi Watanzania kutumia bidhaa za ndani hata kama ziwe na ubora sawa na hizo za nje hivyo mimi bado naona ni vyema kuzuia uingizaji wa bidhaa kutoka nje ambazo sisi tuna uwezo wa kuzizalisha sio ili tu kuimarisha shilingi ya Tanzania, bali pia ili kuweza kuwashawishi Watanzania waweze kupenda na kutumia bidhaa za Tanzania.

Pili kupandisha kodi kwenye mafuta na bidhaa nyinginezo mimi naona sio sahihi, huoni kuwa uamuzi huo utaumiza na kukandamiza Watanzania hasa wale wa kipato cha chini?
 
Natamani shillingi ibaki kuwa chini, imesaidia sana biashara yangu za kusafirisha mikeka na majamvi.

Hivi kwanini haswa unataka shillingi ipande? Hususan unapotaka tuuze sana nje.
unauza sana huenda bei yako chee kutokana na dhamani ya shilling. badala ya kuchekelea inabidi kutathmini. kama thamani ya shilingi ingekua juu huenda ungeweza kupata zaidi kwa kusafirisha kidogo kuliko kuumia kifua kwa kunyonywa nguvu na muda
 
KUPANDISHA SHILINGI YETU MPAGO AMBAO NI REALISTIC NA NINAUONA UNATEKELEZEKA KIRAHISI SANA NI KILIMO, TUKILIMA KILIMO KIZURI CHA UMWAGILIAJI PAMOJA NA UFUGAJI, KWA KUTUMIA ADVANTAGE YA MVUA NA MITO NA MABONDE YA HAPA KWETU TUTAFANYA EXPORT NYINGI SANA ZA KUINUA SHILINGI YETU, NCHI ZINAZOTUZUNGUKA KAMA KENYA BURUNDI, RWANDA TUTAWAUZIA SANA KWA KUA WAO WANA ENEO DOGO NA KAMA KENYA HIVI ENEO LAO HASA KASKAZINI NI KAMA JANGWA, HAYA MAMBO YA KUSEMA KUSUBIRIA KUFUFULIWA VIWANDA NA WAKATI TEKNOLOJIA YA KISASA YENYE UFANISI WA KUSHINDANA NA VIWANDA VYA NJE, HATUNA NA UMEME WENYEWE WANASEMA GESI, GESI KILA SIKU TUSIYATEGEMEE WAKUU, TANZANIA INA ADVANTAGE YA KUWA NA MAJI MENGI YA MVUA MITO NA MAZIWA, NGUVU KAZI KUBWA (WATU MIL 50), NA ENEO KUBWA PAMOJA NA UTULIVU, BANDARI KWENYE MAZIWA PAMOJA NA MAZIWA TUKIAMUA KUTUMIA VITU HIVI KUWEKEZA KWENYE KILIMO KWA UFANISI, SHILINGI YETU ITAPANDA SANA, TUMEKOSA TU VIONGOZI WAZURI NA WANANCHI WAVIVU WA KUFIKIRI NA KUFANYA KAZI, ILA TUKIAMUA TUTAFIKA MBALI

Mkuu, wazo lako ni zuri sana lakini wazo hilo haliwezi kufanikiwa kukuza thamani ya shilingi yetu bila ya viwanda. Tunaweza tukalima mazao yenye ubora wa kimataifa kwa kutumia kilimo cha kisasa lakini bila ya viwanda vya ku-process hayo mazao bado mazao hayo hayawezi kusaidia kuiingizia nchi pato kubwa na kukuza thamani ya shilingi yetu.

Ili mazao hayo yaweze kuliingizia Taifa pato kubwa na kukuza thamani ya shilingi yetu ni lazima tujenge viwanda vya ku-process na kupack hayo mazao kwa viwango vya kimataifa ili mazao hayo haweze kuuzika nje na kuliibgizia Taifa pato kubwa na kusaidia kukuza thamani ya shilingi yetu.
 
Mawazo mengine ni kupambana na mtandao haramu wa utakatishaji fedha ambao husababisha shilingi kushuka ghafla na kuathiri mfumo mzima wa soko huria.
Biashara za madawa ya kulevya zikithibitiwa na watu wote ndani ya uchumi wetu kutumia shilingi katika mahitaji ya kila siku ikiwemo mishahara ya wageni walio wengi tutaimarisha mno sarafu yetu. Wengi mishahara yetu ni kwa $$ ili kuzuia kuyumba kwa uwezo wa kununua (purchasing power) kwa sababu ikiwa kama mshahara wangu ulikuwa Tzs4.2million kwa rate ya Tzs1,600 nilkuwa na uwezo wa kubadili na kupata US$2,625 ghafla rate inakuwa Tzs2,100 kwa dollar moja hivyo ninapata $2,000 na kupoteza $625 ($2,625-2,000). Hii ni mshituko mkubwa kwa wale wanaopokea shilingi tu bila ku hedge (kukinga) na madhara ya kutosimamia sarafu. Unategemea iweje kwa huyu mfanyakazi? Atabuni mbinu ya kupambana na upotevu wa purchasing power ambayo itakuwa siyi mzuri kiuadilifu!

Asante sana mkuu kwa mawazo yako mazuri. Bila shaka mawazo haya yakitiliwa mkazo na serikali yatasaidia sana katika kuimarisha shilingi ya Tanzania.
 
Mimi nianaamini kwamba, mbali na kujitahisi kuzalisha bidhaa nyingi hapa hapa kwetu, pia watanzania tuelimishwe umuhimu wa kuthamini vya nyumbani kuliko vile vinavyotoka nje. Watanzania Tukijenga tabia na utamaduni wa kuzipendelea bidhaa zetu pale tunapofanya manunuzi, ninaamini shilingi itaimarika. Faizafoxy anatamani shilingi iendelee kushuka kwa maslahi yake binafsi, hii ni utovu mkubwa sana wa uzalendo. Mimi kwenye profession yangu ninalipwa kwa dola, pamoja na kwamba kuanguka kwa shilingi kunaniweka kwenye nafasi nzuru zaidi ya kufaidi, lakini kwasababu za kizalendo siwezi kupenda hali hiyo iendelee kutokea. Faizafoxy, tafadhali badilisha mtazamo wako. Shilingi inapoimarika maisha ya watu yanaboreka.

Umenena vyema mkuu. Nashukuru kwa mawazo yako chanya na ya kizalendo.
 
Natamani shillingi ibaki kuwa chini, imesaidia sana biashara yangu za kusafirisha mikeka na majamvi.

Hivi kwanini haswa unataka shillingi ipande? Hususan unapotaka tuuze sana nje.
Hili swali ni la Kisayansi, Dada FaizaFox faida unazozipata kutokana na udhaifu wa shiringi yetu ni za mda mfupi tu, ikiendelea kuporomoka itafika mahala itapelekea mfumuko wa bei ambao hutaweza hata kununua malighafi za kutengenezea hiyo mikeka na Majamvi, kwa manufaa ya mda mrefu ni vema tukihangaika kuimarisha Shiringi yetu
 
Back
Top Bottom