Mapato ya TRA mwezi Juni yatashuka

Mkuu, hizo ni hisia zako tu ila ukweli unabaki kwamba TRA wanakusanya mapato kwa kuvuka malengo yao

Wewe ni zaidi ya Lusinde mpaka upewe ukuu wa wilaya ndio utatulia kiukweli mpaka sasa Jk uongozi wake ulikuwa upo vizuri kuliko huu

Nyie taka taka mnafikiri ya kishuka au kukosekana kama mnavyo penda nani ana salimika? Au mnafikiri mnaishi Tanzania nyingine? Mtabaki kupiga ramli huku TRA ikivuka malengo iliyojiwekea!

Ikulu mtaisikia kwenye TV na radio..Tangu lini nyie wanafiki wazandiki mkamsifu JK?
Mwaka huu kazi mnayo!

Soma hapa
TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI KWA MWEZI MEI 2016

MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo.
Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka katika ukusanyaji wa mapato.
“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha, ambapo kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo hususani katika pwani ya bahari ya Hindi na mipaka yote, kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za kodi za keielektroniki , kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema Kamishna Mkuu.
Bw. Kidata ameendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.
Katika kutekeleza agizo la Mh. Rais na kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD Mamlaka imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wadogo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
TRA imeanza ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wapatao 5,703 wenye mauzo ghafi kati ya Shilingi milioni 14 na milioni ishirini (20) kwa mwaka, wafanyabiashara hao wanatakiwa wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato za Mikoa wanayolipia kodi ya Ilala, Kinondoni na Temeke ili waweze kuhakiki usajili wao wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na kupewa kibali cha kupewa Mashine ya EFD zoezi lililoanza Juni Mosi alisisitiza Kamishana Mkuu.
Aidha, Bw. Kidata alifafanua kuwa zoezi hili litaendelea katika Mikoa yote Tanzania kwa awamu kwa utaratibu utakaotangazwa mara kwa mara na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wenye mauzo tajwa wote nchini kutoa ushirikiano pindi inapofika zamu yao katika Mikoa yao.
Zoezi hili litasaidia kuongezaka kwa Mapato ya nchi endapo wafanyabiashara na wananchi watakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha wanatumia mashine hizo na kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu wafanyabiashara wote watakao kiuka kutumia mashine hizo za EFD.
Kwa upande wa wananchi, kamshna mkuu amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia sambamba na risiti walizopewa
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

TRA ni wajanja wanaweka makadirio madogo ili waweze kuvuka makadirio yao.Ni kwanini makusanyo yanazidi kupungua mwezi baada ya mwezi? kama awatuhadai wangetakiwa waweke malengo makubwa kuliko mwezi wa mwisho kukusanya mapato.Mfano Mei wamekusanya trillion 1.02 malengo ya mwezi june yanatakiwa yazidi mapato ya mwezi may.
Lakini wanatuhadaa kwa kupunguza kiwango.

Kwani wewe unavyoelewa kuvuka malengo ni kupi? Nijuavyo mimi ni kwamba unavuka malengo pale ambapo umezidisha kile ulichojipangia. Kumbuka malengo ya TRA hayapangwi kienyeji kama mapato yenu pale Ufipa
Si kile atayepingana na wewe yuko Ufipa.

Hoja hapa wala siyo kuvuka malengo. Hata kama malengo yanapangwa kitaalamu(hilo linafaamika), hoja ni kwa mimi malengo yanazidi kudidimia?

Kama mwanzo ulikuwa na lengo la trilioni Moja nukta nne.....miezi sita iliyopita.....Leo unaweka lengo la trilioni moja....si umerudi nyuma? Na bado mteremko unaendelea
Huyo achana naye, si unaona alivyopaniki? Unafikiri atakujibu la maana.? Na hapa si ajabu yupo katika "ebigata" anakumywa "nkanja".

Si kile atayepingana na wewe yuko Ufipa.

Hoja hapa wala siyo kuvuka malengo. Hata kama malengo yanapangwa kitaalamu(hilo linafaamika), hoja ni kwa mimi malengo yanazidi kudidimia?
Swali Zuri kabisa ambalo analikwepa lizaboni

• Thanks
Reactions: Izc
Mwenyewe ukiuza, ukinunua hutoi wala hudai risiti, itapandaje kodi, wafanyabiashara wanaangalia upepo unaendaje. Kukaza kukiisha biashara imeisha

Si kile atayepingana na wewe yuko Ufipa.

Hoja hapa wala siyo kuvuka malengo. Hata kama malengo yanapangwa kitaalamu(hilo linafaamika), hoja ni kwa mimi malengo yanazidi kudidimia?
Yamekuwa kama ni pipa linalo vuja au taili lenye sloo pancha

• Thanks
Reactions: Izc
Yamekuwa kama ni pipa linalo vuja au taili lenye sloo pancha
Teh teh! Lumumba wenyewe walevi na mada hii imeletwa usiku sijui kama wataleta cha maana. Rutashobya ameamka kwenye usingizi wa lubisi na nkanja akaanza kutukana, lizaboni ndo kabisa aelewi.

CCM WANAHANYA SASA ETI HAPA KAZI WAKATI UONGOZI UMEWASHINDA HADI NJE INAONGOZWA KWA MAWAZO YA RAISI BILA KUFUATA KATIBA

Teh teh! Lumumba wenyewe walevi na mada hii imeletwa usiku sijui kama wataleta cha maana. Rutashobya ameamka kwenye usingizi wa lubisi na nkanja akaanza kutukana, lizaboni ndo kabisa aelewi.
Lizaboni keshapiga mataputapu yaani komoni sasa hivi yupo hoi

• Thanks
Reactions: Izc
Teh teh! Lumumba wenyewe walevi na mada hii imeletwa usiku sijui kama wataleta cha maana. Rutashobya ameamka kwenye usingizi wa lubisi na nkanja akaanza kutukana, lizaboni ndo kabisa aelewi.
Hahahaa Mkuu....wamekurupuka wako kit

• Thanks
Reactions: Izc
Back
Top Bottom