Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2020 umekamilika rasmi Leo kwa mshindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Joseph Pombe Magufuli Kukabidhiwa cheti cha Ushindi.
Katika hekaheka za Kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, zilizodumu kwa siku 60, kuna Tuzo kumi bora zinazostahili kutolewa kwa wahusika kutokana na ubora uliojidhihirisha.
1. Tuzo ya Gazeti bora la Kampeni inaenda kwa gazeti za Mwananchi. Katika siku 60, gazeti hili lilijitahidi kuwatendea haki wagombea wa vyama vyote kwa kuandika habari zao pasipo kuegemea upande wowote. Hongereni sana Wamiliki wa gazeti hilo kwa kutenda haki.
2. Tuzo ya Kituo bora cha Televisheni inachukuliwa na ITV. ITV walijitahidi sana kuwa neutral na kutoa fursa sawa kwa wagombea wote. Hawa waliifunika hata UTV inayomilikiwa na AZAM Media. Hongereni sana ITV.
3. Tuzo ya Mgombea Chipukizi aliyevuta mioyo ya watanzania inakwenda kwa Queen Sendiga. Dada huyu ingawa wengi hawafahamu wasifu wake lakini aliweza kujieleza vyema na kunadi Sera za chama chake ADC. Katika mitandao mbalimbali, watu wanamuona kama mbadala wa Anna Ngwira, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aliyetikisa kampeni za 2015 kupitia ACT Wazalendo. Wapo wanaoamini Dada huyu mwenye uthubutu anaweza kuteuliwa kushika nyadhifa kama Mbunge mteuliwa wa Rais, mkuu wa mkoa, wilaya au mkutugenzi, dada huyu ni hazina kwa Taifa kwa siku za usoni.
4. Tuzo ya Mpinzani Halisi, inaenda kwa Tundu Antipasi Lisu, huyu ameonesha ujasiri wa dhati na upinzani thabiti. Alipokosa kivuko kwenda Ukerewe alipanda Mtumbwi, aliponyimwa kibali cha kurusha Chopa alipaa hivyo hivyo. Ingawa watanzania wanamuona kama kibaraka na wakara wa mabeberu, amethubutu kusimamia anachokiamini na sifa yake kuu ni kupinga kila kitu.
5. Tuzo ya Kada mnyenyekevu inakwenda kwa Agrrey Mwanry, Mzee wa Sukuma Ndani. Mwanry alishindwa ubunge na Dr. Mollel mwaka 2015, Mollel akitokea Chadema. Mwaka huu Mwanry alizidiwa kura moja na Mollel 147 kwa 148, hivyo CCM ikamteua Mollel. Mzee Mwanry kwa unyenyekevu mkubwa, amezunguka kumnadi Dr. Mollel ili kumwombea Kura tofauti na makada wengine ambao baada ya kuangushwa ktk kura za maoni hawajaonekana jimboni. Bwana Mwanry anapewa tuzo hii kwa unyenyekevu wake na uungwana ambazo ni tunu katika siasa.
6. Tuzo ya urafiki wa kisiasa inakwenda kwa Godbless Lema & Mrisho Gambo, wa jimbo LA Arusha mjini. Pamoja Kugombea jimbo moja, wagombea hawa walionesha urafiki na kupendana. Naamini hata baada ya uchaguzi huu, urafiki wao utaendelea. Siasa sio uadui ndiomaana wawili hawa wanatunukiwa tuzo hii ya Ushikaji wa kisiasa.
7. Tuzo ya Chama bora cha kisiasa inakwenda kwa CCM na Mgombea wao Dkt Magufuli, katika uchaguzi huu, wana CCM walikuwa wamoja na umoja wao ndio Ushindi wao. Kabla ya kampeni, waliwarejesha kundini wale wote waliokikosea chama. Mfano: Kinana, Nape, Sophia Simba, Lowasssa, na waliwatumia wastaafu kama Kikwete, Pinda na Sumaye katika kusaka Kura tofauti na vyama vingine ambavyo viligawanyika. Mfano: hadi mwisho wa kampeni, hajaonekana Lazaro Nyarandu akimnadi Lisu tangia aenguliwe kugombea Urais. Jambo hili limechangia ushindi wa JPM kwa kiasi kikubwa
8. Tuzo ya wimbo bora wa kampeni inakwenda kwa 'Tanzania ya Sasa,' chini ya Zuchu. Wimbo huu umetikisa ndani na nje ya nchi, unaibua hisia na hali ya kuipenda Tanzania na kumchagua Dkt Magufuli.
9. Tuzo ya Mtandao bora wa Kijamii katika uchaguzi wa 2020 inakwenda kwa JamiiForums na wamiliki wake, Melo na wengineo. JF, ilitoa fursa sawa kwa wote, mabandiko ya wagombea wote yalipewa nafasi sawa, JF iliyodhaniwa ni ya mabeberu au mawakala wao wapinzani, mwaka huu imejisafisha na kudhihirisha uzalendo. Hata internet iliposuasua katika Instagram, Twitter, Facebook na WhatsAp, Jamii Forum ilikuwa hewani na kampeni zikaendelea. Nawapongeza sana wana JF kwa kutoa fursa sawa kwa CCM (Pascal Mayalla) na Chadema (Mshana Jr) pamoja na vyama vingine.
10. Tuzo ya Uzalendo, Umoja, Amani na Utulivu inakwenda kwa Watanzania wote. Tangia wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na hata baada ya matokeo kutangazwa, watanzania wamebakia kuwa wamoja, wenye amani, uzalendo na utulivu. Watanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida wakijua uchaguzi umekwisha na mshindi kapatokana. Wengi wanashangaa matamko ya kukataa matokeo, kuyapinga na kuandamana. Hongereni sana watanzania kwa tabia hii njema.