Maoni yangu juu ya Mfumo wa kujitolea na Usimamizi wa Ajira za dharura Serikalini

Mar 23, 2023
83
100
Katika muktadha wa ajira serikalini, suala la kujitolea linazua changamoto nyingi, hasa linapokuja suala la kutumika kama kigezo cha ajira za kudumu.

Ingawa ni muhimu kutambua mchango wa wanajitolea, kutumika kwa kigezo hiki kunaweza kufungua milango ya upendeleo wa kifamilia au urafiki.

Kujitolea hakupaswi kuwa msingi au dhamana ya kupata ajira katika serikali kuu; vinginevyo, nafasi za kujitolea zitatafutwa kama ajira, hali inayoweza kutengeneza umasikini.

Ajira za Dharura na Mfumo wa Kudhibiti Kujitolea

Ni muhimu serikali kuzingatia jinsi watu waliojitolea kwa dhati wanaweza kupewa kipaumbele katika nafasi za dharura zinazotokea mara kwa mara kutokana na mahitaji ya haraka, kama vile kustaafu, kifo, kuacha kazi, au ongezeko la mahitaji ya wafanyakazi katika mikoa husika.

Ili kufanikisha hili, ni lazima kuwepo vigezo maalum vya ushindani kama vile muda waliotumia kujitolea, mwaka wa kuanza kujitolea, na mchango wao katika kazi.

Nafasi hizi zinapaswa kuombwa moja kwa moja wizarani, na mifumo ya kuhudhuria kama vile fingerprint sign-in na sign-out iwekwe ili kuthibitisha uwepo wa walimu shuleni. Aidha, wanajitolea wanapaswa kufanya declaration ya kujitolea kwa hiari yao wenyewe, si kutafuta dhamana ya kupata kazi.

Hata hivyo, ikitokea nafasi za dharura, waliojitolea wanaweza kupewa kipaumbele, lakini tu ikiwa watakidhi vigezo vya na muongozo wa kupata kwao nafasi iyo.

Mfumo wa Uwazi na Usimamizi wa Ajira za Kujitolea

Kujitolea kinapaswa kuwa wazi kama nafasi ya kujipatia uzoefu, si dhamana ya kupata kazi. Ni muhimu kwa watu kufahamu kwamba kujitolea hakuhakikishi ajira serikalini, lakini inaweza kuwasaidia kuingia kwenye orodha ya wahitaji wa ajira za dharura pale nafasi zinapotokea.

Kwa mfano, nafasi zinazo tangazwa na wakurugenzi ngazi ya mkoa zinaweza kutolewa kwa waliojitolea na kwa ufanisi, ikiwa wanakidhi vigezo vyao vya kiushindani lakini ajira za selikali kuu lazima wafanye usaili na kigezo icho kitumike kama kipaumbele pale atakapo faulu usaili hasa kwenye mgongano wa maksi tu

Mfumo wa Kuwezesha Maombi na Uthibitisho.

Soma Pia: Kujitolea hakufai kua kigezo cha taifa watu kupewa ajira; Badala yake serikali iongeze ajira kutaondoa tatizo

Ili kuhakikisha usawa na uwazi, serikali inapaswa kuanzisha mfumo rasmi wa maombi ambapo mtu anaweza kuomba nafasi ya kujitolea au internship katika shule yoyote inayopatikana.

Hii itasaidia kuzuia rushwa za ngono, hongo, na ukabila. Shule zinapaswa kuonyesha kama kuna nafasi za kujitolea, na serikali itakagua na kuthibitisha maombi hayo.

Endapo shule haina uhitaji wa haraka wa walimu wa kujitolea, serikali itamfahamisha mwombaji mapema na kumpa maelekezo ya maeneo mengine yenye nafasi.

Usimamizi wa Walimu wa Kujitolea na Interns Shuleni

Mara tu maombi ya kujitolea au internship yanapopitishwa, mwombaji atapangiwa shule husika, na mkuu wa shule atakuwa na jukumu la kuwashughulikia kama walimu wengine.

Hii inamaanisha kuwa mkuu wa shule atakuwa na jukumu la kuwasimamia na kuwapa maelekezo, lakini hata kuwa na mamlaka ya kukubali au kukataa mtu kujitolea kwa sababu binafsi.

Wizara itakuwa na kumbukumbu za maombi yao na mahudhurio yao.

Uthibitishaji wa Huduma za Kujitolea

Ili kuepuka ulaghai, barua za uthibitisho wa kujitolea zinapaswa kutolewa kwa uwazi na kwa mfumo wa kitaasisi, ikijumuisha uthibitisho wa mahudhurio wa kidigitali na wa mwandiko.

Tathmini ya utendaji wa wahusika lazima ifanyike ili kuepuka watu wenye lengo la kukwepa majukumu kwa kisingizio cha kujitolea.

Hitimisho

Kwa kutumia mfumo thabiti wa kudhibiti kujitolea na kuweka wazi kwamba nafasi za dharura tu ndio zitakazotolewa kwa kipaumbele kwa waliojitolea, serikali itajivua kwenye mzigo wa upendeleo na kuboresha uwajibikaji.

Kujitolea kinapaswa kuwa njia ya kupata uzoefu na si kigezo cha ajira za kudumu serikalini. Huu ndio mpango bora wa kusimamia ajira za dharura, huku ukihakikisha usawa na uwazi katika mchakato wa kuajiri.

Haya ni mawazo binafsi ambayo yanahitaji kukosolewa na kuboreshwa kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuwa na mfumo bora wa ajira serikalini.


BY Josephat
 
Nafikiri kama bunge lilivyokataa kigezo cha mafunzo ya JKT kwenye ajira za baadhi ya taasisi hivyo hivyo na hiki kigezo cha kujitolea kutumika kutoa ajira isiwepo popote.

Hii ni kwa sababu ukiangalia mtaani watu wengi wanataka kujitolea lakini unakuta nafasi zinazotolewa za kujitolea mfano kwenye hospital au shule fulani ni 5, wanaoomba kwa maana ya kuonesha nia ya kutaka kujitolea ni mfano 20. Lakini mwishowe ni watu watano (5) tu watapewa nafasi hizo, sasa hao 15 waliobaki na walitamani kujitolea siku nafasi za ajira zikitangazwa waachwe kwa sababu hawajitolei? Au kama basi wakipewa uwanja sawa wa kufanya interview lakini wale 5 wakaongezewa sifa ya kujitolea inakuwa upendeleo wa moja kwa moja kwa sababu wote walitaka kujitolea lakini kutokana na uchache wa nafasi wengi wamebaki bila kujitolea.

Kwa hiyo ajira zitolewe kupitia njia za wazi kama interviews bila kuzingatia kigezo cha kujitolea kwani nafasi za kujitolea hutolewa kulingana na uhitaji na uwezo wa taasisi husika na si kwa kuangalia wingi (idadi) ya wanaohitaji kujitolea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…