Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwatanda

New Member
May 13, 2024
1
0
Nawasalimu kwa Jina la Muungano wa Tanzania!

Samahani, naomba kuwasilisha MAONI kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kimtandao kuanzia tarehe 11.05.2024 hadi hivi sasa. Hali ambayo inazua taharuki kwa vijana waliyokidhi vigezo vya kufanya maombi ya nafasi za ajira zilizotangazwa kwenye mfumo wa ajira wa Jeshi la Polisi na websites za Jeshi la Polisi Tanzania.

Kutokana na changamoto hiyo ya kimtandao inayoendelea hadi hivi sasa, imekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana dhidi ya kutuma maombi yao kwa wakati kwenye mfumo wa ajira kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la nafasi za ajira hiyo.

Maombi yangu ni kwamba Jeshi la Polisi Tanzania lifikilie namna ya kuongeza siku za kufanya maombi kutokana na kuathiriwa kwa siku za zoezi hilo kwa uwepo wa tatizo hilo la kimfumo wa mtandao. Maana tangazo limetolewa tarehe 09.05.2024 na changamoto ya kimtandao imeanza kujitokeza kuanzia tarehe 11.05.2024 hadi hivi sasa. Huku ikiwa mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 16.05.2024.

Hivyo basi, kuna haja ya Jeshi la Polisi Tanzania kulifikiria kwa makini suala la kuongeza muda wa kufanya maombi hayo kutokana na changamoto hiyo.

Naomba kuwasilisha.

Wako katika Ujenzi wa Taifa.
 
duh kuna watu mpka leo wanaenda kuwa manjagu hakuna kingine cha kufanya au wanapenda kuvaa sare
 
Nimekutana na changamoto hii unakuta page haifunguki hata usiku wa manane pia haifunguki..tunaomba serikali iingilie kati hili suala
 
Kwa afande agp.
Awali ya kwanza ni kumshukuru mwenyemungu muweza wa yote

Dhumuni, andiko langu ni kuomba kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kuongeza utumaji maombi kwa vijana wetu wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi baada, mtandao polisi utumaji maombi kufeli kupokea maombi ya waombaji wa nafasi mlizotangaza na kesho ndo mwisho .

Kwa mujibu wa tangazo mliotoa jeshi.la polisi.kuongeza mda kuwapa nafasi vijana kutuma maombi kazi polisi Kama mlivyotangaza uongozi jeshi polis Ione busara ya kuongeza muda utumaji maombi.ya kazi vijana wanahangaika toka mlivyotangaza kutuma maombi bila mafanikio ufikiaji mtandao wenu wa kitehama upokeji maombi ya kazi kwa jeshi la polisi .

Ni tumaini langu kuwa maombi yafanyiwa kazi mbele ya ofisi yako

Wenu katika ujenzi wa Taifa

Kiforokwinyo
 
1715818454398.png

Sasa ni saa 9:10 usiku wa manane mtandao wa jeshi la Polisi la kufanyia maombi kuna ujumbe huo leo tarehe 16.05.2024, maombi online bado ni changamoto hakuna namna ya kufanya
 
Mifumo mingi Tanzania ni shida
Inawezekana vyeti feki au ukosefu wa uzalendo au ununuzi uliofanyika haukuzingatia ubora wa bidhaa.
Mfano hivi inaingia akilini taasisi kubwa na nyeti nchini inashindwa kutatua tatizo la kiufundi kwa siku zaidi ya tano je,wale walioweka cable baharini na wamemudu kurekebisha ndani ya siku tatu wao wakoje?
Leo vyuo kupeleka uthibitisho ili wanafunzi wapate AVS Namba bado ni kizungumkuti sijui wa Tz tulilogwa na nani!! Mifumo ya kulipa kodi za ardhi na e government ubabaishaji umejaa mno ni aibu.
 
Wana bodi habari za asubuhi kutoka upande wa malampaka hizi ajira za jeshi letu la polisi kwa nini website yao iko down muda wote ukianza utaratibu wa kuomba baadae unagoma kufunguka ata izo siku walizo ongeza wamefanya kitendo sawa na bure.
Mtandao haufunguki ningeshauri jeshi letu la polisi lipokee maombi kwa njia ya posta.
Hii mambo ya mtandao naona tumefeli hatuko well equiped kwenye mitandao...
 
mkuu njoo hapa FDC tukusaidie
 
Litakuwa tatizo la network kwa upande wao
 
Back
Top Bottom