Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,047
- 13,856
Mradi huo, unaotekelezwa na Fundi Sanifu wa SUWASA Mkami Magesa, umehusisha uchimbaji wa mitaro, ununuzi wa viungio na mabomba yenye kipenyo cha nchi 1.5 kwa urefu wa mita 1,950, ujenzi wa chemba za vizuizi na uwekaji wa alama za za kuonesha njia za mabomba ambapo jumla ya gharama za mradi huo ni shilingi 12,600,745.
Akizungumza katika eneo la mradi, Magesa amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuboresha huduma ya majisafi kwa wananchi, hususani kwa wanawake ambao mara nyingi huathirika zaidi na changamoto ya upatikanaji wa maji.
"Tumekamilisha huu mradi na tunaamini changamoto za maji, hasa kwa kina mama wa kisaki, sasa zimepungua. SUWASA itaendelea kuboresha huduma katika maeneo mengine kadri bajeti itakavyoruhusu,"
Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumewapa faraja kwa kuwa sasa hawatalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi, hali ambayo iliwapotezea muda mwingi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ng’aida, Juma Issa, ameishukuru SUWASA kwa kufanikisha mradi huo na kubainisha kuwa huduma hiyo itapunguza mzigo kwa kina mama na kuimarisha afya za wananchi.
"Huduma hii itapunguza mzigo kwa kina mama na pia itaimarisha afya za wananchi wa mtaa wetu."
Kata ya Kisaki ni moja ya maeneo ambayo SUWASA imefanya maboresho ya huduma ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya majisafi na salama ambapo mpango huu ni endelevu.