faru john junior
JF-Expert Member
- Dec 26, 2016
- 1,596
- 1,719
Una zidi kuniongezea stress ngoja kwanza nitafute kiroba japo vimekuwa adimu sana ila kwa Mama nani ntapta tuMaisha ni safari ndefu sana lakini ukishafikia umri wa miaka 30 hapo utakuwa ndio umri wa kustaafu ujana na kuachana ujana.
Baada ya kijana kufika miaka 30 na kustaafu ujana hivyo kuachana na kufanya visivyo vya msingi kama vile kubadilisha wasichana, kwenda club, kukesha bar, kutafuta Malaya, kuacha kukaa vijiweni.
Vitu vya msingi vya kufanya;
1.Aanzisha uhusiano na mdada au mkaka mwenye mwelekeo wa maisha wa kukufanya muyajenge ya baadae.
2.Jenga urafiki na marafiki waliofanikiwa angalau upate exposhure ya mafanikio.
3.Jitahidi utafute fani yoyote ya kukuwezesha uweze kujiajiri na kuajiriwa.
4.Usipende kukaa vijiwe ambavyo watu wengi story zao nyingi ni mpira, siasa na dini kwa maana story hizo zinaweza kukupotezea mwelekeo wako wa maisha.
5.Epuka kukutana au kukaa na watu ambao muda wao mwingi wanazungumzia maisha ya watu.
6.Achana na tabia ya kuhonga bia na pesa.
7.Kama huna ajira unafikia miaka 30 basi tumia plan b ya kujiajiri wewe mwenyewe katika kipindi hiki cha mpito.
8.Kama wewe ni mpenzi wa muziki jitahidi sana uwe unasikiliza bongo fleva za zamani au zilipendwa kwa maana zinamafundisho.
9.Katika uvaaji jitahidi uwe unavaa nguo za heshima lakini pia ubadilike kimawazo.
10.Usiendekeze mambo ya mahusiano na mapenzi kwa mtu ambae hana mwelekeo wa maisha zaidi ya kukunyonya ulichonacho.
Ni hayo tuu wengine mnaweza kuendelea.