Mambo ya kuzingatia unapotaka kuanzisha Mobile App au Startup Company

Sea Beast

JF-Expert Member
Aug 5, 2022
2,202
4,780
Tech sasa hivi ndio industry yenye pesa Duniani kuliko industry yoyote, zamani visima vya mafuta ndio ilikuwa habari ila kwa sasa tech ndio kisima cha mafuta na DATA ndio mafuta, ukitaka kufanikiwa miliki DATA the way unavyozidi kuwa na DATA nyingi na ndio utajiri wako unaongezeka makampuni kama FACEBOOK na GOOGLE yana data kubwa sana ya watu ndicho kinachofanya wao kuwa na utajiri mkubwa sana.

Content creator kama Khabi Lame mpaka sasa ana mikataba na makampuni makubwa Duniani kwa sababu ya TikTok yake kuwa na Followers wengi wanaomfuatlia.

Kati ya njia ambazo unaweza kuzifanya kuwa DATA ni kuanzisha Mobile App, ukianzisha App inayotatua tatizo fulani na kupata watumiaji wengi maanake utakuwa na DATA ambayo unaweza kuigeuza kuwa pesa, Watu wengi wamekuwa na muamko wa kuanzisha Mobile App zinazolenga kutatua matatizo mbalimbali ila wengi wamekuwa hawana uwelewa wa kutosha wajinsi ya kuanza safari hiyo, wanaingizaje pesa na mambo mengine mengi hii ni kwa sababu wengi hawana uwelewa wa information tech ila wengi wanapenda kuwekeza kwenye technology
images (6).jpeg

Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuanzisha APP yako hii itakufanya uwe na chance kubwa ya kufanikiwa:

1)Niche
Kwanza hakikisha unaielewa Niche husika unapolenga kutatua tatizo mfano wa Niche kilimo, ajira, elimu, afya, usafiri. Inakuwa vizuri zaidi kama hiyo Niche una taaluma nayo kama wewe ni Doctor ukileta digital solution kwenye afya itakuwa bora zaidi kwa sababu utakuwa na uelewa mpana na pia inakuwa rahisi kupata Fund, Grant au hata uwekezaji endapo umelenga hayo kwenye Model yako...ila pia sio lazima uwe umesomea hiyo Niche.
images (15).jpeg

2)Business Model
App yako unayoanzisha unaifanya kwa namna gani kama biashara ili uweze kuteka soko na kupata faida, kuna aina mbalimbali za Business Model kwenye Business kama vile B2B hii inamaanisha (Business to Business) mteja wako Biashara, B2C inamaanisha (Business to Customer) mteja wako mtu wa kawaida, B2G inamaanisha (Business to Government) mteja wako Serikali…katika Model hizi tatu Model nzuri zaidi kwa Tanzania ni B2B hii ni kwa sababu biashara na kampuni zinamuhamko wa matumizi ya technology pia muda wote zinatafuta solution za kukuza biashara zao, B2G ni Model nzuri endapo unalenga pesa in short run na kusepa ila kama unafanya for long run serikali haitabiriki ccc MAXMALIPO.

images (13.jpeg
Pia kuna model nyengine mfano JF Model yake ni User Generated Content so unapoanzisha App yako unweza kuanzisha kama zilizopo sokoni ila kwa Model yako ambayo itadaka soko kuliko competitor wako


3)Marketing
Kutengeneza App atakutengenezea Developer ila tambua Development na Coding kwenye App au Startup ni inachukua 10% tu ya mafanikio ya App kila aliye na pesa anaweza kumlipa Developer akatengeneza App ila kitu kinachofanikisha App 90% ni marketing App isiyokuwa na Idea kali na ikafanyiwa marketing itafanikiwa kuliko ilikuwa na idea kali na haifanyiwi marketing, wakati mwengine pia wateja hawajui wanataka nini kwa marketing ndio unawaonesha wanachotaka.

Hakikisha una clear marketing strategies platform nzuri za kutangaza App yako Twitter, FB, IG nk pia itategema na Niche au Business Model ya App yako.
images (12).jpeg
4)Monetaizing
Swali la App fulani inaingizaje pesa wengi wamekuwa wakijiuliza hii ndio inaitwa monitaiztion kabla ya kuazsia App yako inabidi uwe na clear EXIT PLAN ambyo utapata vipi pesa kuna njia kadhaa za kupata pesa kupitia App.
images (10).jpeg

#ADS: kuweka matangazo kwenye App yako ya biashara au google adsencehii ni njia nzuri ya kuingiz pesa endapo utakuwa na user wa kutosha kwenye App yako

#Paying User: kuwa na watumiaji ambao wanalipia huduma ya kutumia App kutokana na value unayotoa kuwa na umuhimu kwao

#Grants: hii endapo App yako inatatua matatizo ya kijamii zaidi kama Elimu, Afya, walemvu inakuwa rahisi kupata Grant


Kuna njia nyingi sana za kupata pesa kupitia App nyengine ni legal kijanjajanja

5)EXCUTION
Kuna idea nyingi sana za App kuliko App zilizopo watu wengi wamekuwa na Idea ila kuazisha App wanashindwa kwasababu za kutokuwa na pesa, kutokujua coding languages, kutokuwa na uwelew na tech nk.

Kuanzisha App unahitaji ujue Coding basi kama hujui Coding huwe na pesa za kumlipa Developer na Designer wa App yako.
images (11).jpeg
Njia rahisi ya kunzisha App au Startup Company yako ni kupitia Co-Founding kutafuta Co-founder mwenye anayejua coding utashirikina naye kuanzisha wote App wewe uhusike kwenye Pesa kidogo na operation nyengine na kwenye technical issues atahusika yeye.

Kitu cha kuzingatia huwezi kwenda kwa developer ukamwambia afanye kazi bure eti kwasababu wewe una idea yeye awe Co-founder lazima uwe na pesa ya kumlipa kwanza hata kidogo kama App kitengeneza 5M unaweza ukafany namna afanye kwa affordable cost na ukamuonesha value ya APP husika vitu vyengine utajua wewe utachezaje.

Njia nyengine nzuri ya kufanya excution ya Idea yako ni kufanya Prior Excution na Documentation, kwanza mpe Designer akufanyie Ui Design ya App yako, andika Business model, Marketing strategies na monitaizition na uziweke kwenye document kwa mtiririko, hii itakusaidia kupata muwekezaji, Co-founder kirahisi zaidi na itaonesha serious.



Bottomline
ukiwa na wazo lako la Mobile App nakusaidia kufanya Design ya muonekano wa App (UX/UI) kwa bei rahisi zaidi na pia nakufanyia documentation ya wazo lako na ushauri mbalimbali.

4562eadfa096952fb31bbb1277ed2307.jpg

0ac9a6c9a12a3f96f54744c267f5714b.jpg
 

Attachments

  • images (13).jpeg
    images (13).jpeg
    24 KB · Views: 34
Unatoa hela ufanyiwe kazi au unatamani utengeneze group umwage hela vijana wazame kwenye ugunduzi unachokutana nacho ni kuchorewa mistari alafu unaambiwa website tayari , ukiuliza vipi app unaweza anakubali ndio naweza basi sawa sh ngapi nikupe na inachukua mda gani, utasikia nipe miezi 4 hapo unachoka kabisaa
 
Unatoa hela ufanyiwe kazi au unatamani utengeneze group umwage hela vijana wazame kwenye ugunduzi unachokutana nacho ni kuchorewa mistari alafu unaambiwa website tayari , ukiuliza vipi app unaweza anakubali ndio naweza basi sawa sh ngapi nikupe na inachukua mda gani, utasikia nipe miezi 4 hapo unachoka kabisaa
Vijana wa ovyo sana, wanasomeshwa kwa ghrama alafu output ni ndogo sana.. wengne wana copy na ku paste..yaan app inakua haina... Creativity
 
Vijana wa ovyo sana, wanasomeshwa kwa ghrama alafu output ni ndogo sana.. wengne wana copy na ku paste..yaan app inakua haina... Creativity
Mkuu ni heri Yule wa kukopy mie nimekutana na wahitimu wa software engineering na computer science wengi tena wa pale idodomia wanatoambia kuwa wapo vizuri ila ni zero na hakuna chochote
 
Mkuu ni heri Yule wa kukopy mie nimekutana na wahitimu wa software engineering na computer science wengi tena wa pale idodomia wanatoambia kuwa wapo vizuri ila ni zero na hakuna chochote
Tatizo sijui ni ufindishaji.. au vijana wetu wamekua sheki sana kielimu
 
Tatizo sijui ni ufindishaji.. au vijana wetu wamekua sheki sana kielimu
Kwanzia lecture ni hovyo vijana ndio hovyo kabisaa mda wote wanalialia na mapenzi, na ukumbuke tech inataka ujitume mwenyewe na kutafuta maarifa kila siku
 
Bongo kufanya monetization ya app kazi sana. Mfano ADMOB hawakubali matangazo yenye maudhui ya kiswahili. Malipo yanafanyika kwa cards na wabongo pesa ziko Mpesa. Nafikiri wizara ingejitahidi ipatikane app store ya waswahili au platform yoyote nzuri ya kupublish apps
 
Kwa wale pia wanahitaji kufanyiwa Designing ya muonekano wa App yako unaweza ni PM through kuna kazi sasahivi za wana JF nazifanya.

Lengolangu kuhakikisha tunapeleka Tech mbali zaidi.

📌Pia kwa ushauri wa wazo lako la App, STARTUP, Online Business n Hustling unaweza nicheki tukabadilishana mawazo

📌Kwa wadau wanaotaka kuanza Online Business Kama Blogging, Freelancing, Forex nk na hawajui ipi Biashara ambayo inamfaa Nina E-book yake

📌Anauehutaji kuanza Freelancing na hajui pakuanzia nina E-book ya maelekezo Jinsi ya kuanza
 
Tunaendelea kufanya kazi ya kufanya Designing ya wazo lako la Mobile App, nakufanyia Designing ya App yako inayoendana na mtumiaji mlengwa

Naendelea na kazi za Wana JF Ni cheki kwa kazi
20221016_170236.jpg
 
Back
Top Bottom