Mambo ya kuzingatia ili wananchi waishi kwa amani chini ya utawala wa kiimla

Acha
Kufanya kazi kwa bidii sio ndio kupata maendeleo, hata Mbeba mizigo anafanya sana kazi kwa bidii ila maisha yake ni yale yale.

Acha dharau kuna wabeba mizigo wana akili na wanajitambua wanaishi kwa kazi hiyo na wanaiheshimu! wewe ulitaka wote tukae ofisini nani angeuza mboga, kulima, mikokoteni, konda etc kwa akili yako hiyo utateseka sana awamu hii
 
Kila mtu atakufa hapa, cha msingi ni kuishi kwa kufuata misingi iliyowekwa! Hao unaowataja akina Hitler, Idd Amin, Musolin na wengineo ungekua unaishi zama zao hata hiyo post uliyotoa ingekugharimu! Mshukuru Mungu sasa uko JF unafunguka kuna watu hawana fursa hii tena majirani zetu! ujifunze kuishi kwa kufuata sheria na kuheshimiana. Sikio halizidi kichwa.
Nafikiri hujaelewa!
 
madikteta wengi tunaowajua wametumia military coup kupoka madaraka ....je huyu umdhaniaye ametumia njia gani ili tujidhihirishe kama kweli ni dikteta.....
 
Ni ngumu sanaa kwa utawala wa kariba ya madictator kama idd amin, Adolf Hitler, na Benito musollin ku exist kwa karne hii..
 
Duh!
Umenikumbusha simulizi za babu juu ya kilichoangusha utawala wa machifu wetu wa jadi karne hizo. Eti watumishi wa chifu wanapita kwa wanakijiji wakiona mhogo mzuri unang'olewa na kupelekwa kwa 'mfalme' wa eneo, nasikia ikafikia muda wafalme wakavimba vichwa hata wakiona mwanamke mzuri wanamuru aletwe kwa mfalme bila kujali kama ana mume. Na hapo ndipo wananchi wakawa wako kimya lakini mioyoni wamefura na alivyokuja mkoloni tu wakasema nyie wapuuzi hamna maana ondokeni!
Tetetetetetetetetete
 
Back
Top Bottom