MAMESHO
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 1,432
- 1,737
Ili tuweze Kufikia malengo tunahitaji kuwa na juhudi, tuweze kuvuka vikwazo na kukamilisha mipango sahihi. Viongozi wetu waonyeshe dira, pamoja tufanye kazi, tuweze kuzalisha ili tufikie maendeleo. Kuweza kujenga jamii yenye heshima kuna mambo ya msingi ambayo tunapaswa kuzingatia.
Tanzania ya ndoto yangu inahitaji mambo tisa muhimu yafanyike;
Uwekezaji uweze kuleta matokeo yanayokusudiwa. Kupanua uwekezaji kutakuza uchumi. Ikiwa uwekezaji mwingi hautaleta faida inayokusudiwa, mikopo na madeni hayataweza kulipwa. Tutakuwa na madeni mabaya ambayo yataleta hali mbaya kwa taasisi zetu za kifedha na nchi itatumbukia kwenye kilindi cha madeni. Ingawa mikopo tunayochukua ni ya muda mrefu ni muhimu miradi ifanikiwe ili kulinda mitaji yetu. Ni vyema kufanya tathmini ya uwekezaji uliofanyika na namna ambavyo tunalipa deni. Tusipofanya hivyo baadaye tuakuwa na mzigo wa madeni na uwekezaji mwingi usioleta matunda, faida na tija kwa nchi yetu.
Bidhaa ziwe na soko. Soko ndio moyo wa biashara. Utafiti wa masoko utatujulisha kuhusu aina ya uwekezaji tunaopaswa kufanya. Tanzania isipozingatia soko makampuni yanayozalisha yatapata hasara. Yatakuwa yametumia rasilimali vibaya kuzalisha bidhaa ambazo hazina soko. Nchi ikipata masoko ya uhakika itaweza kukuza uwekezaji. Soko la uhakika litaweza kushawishi makampuni na vyama vya ushirika kuzalisha bidhaa husika ambazo zinahitajika na soko. Kwa mfano Dhahabu, Shaba na Korosho pamoja na utalii inaongoza kutupatia fedha nyingi za kigeni ni vyema kuwekeza vya kutosha.
Makampuni yapate faida. Kampuni binafsi na za serikali zikipata hasara kwa muda mrefu itaathiri ukuaji wa uchumi, mapato ya waajiriwa na ya serikali hivyo kuleta athari za kifedha na kijamii. Sera na mipango ilenge kuwapatia faida. Serikali iweke mazingira rafiki ya kufanya biashara. Kwa mfano kuwa na mchakato rahisi wa kufungua na kuendesha makampuni, kodi rafiki, miundombinu ya uhakika, umeme, maji, upatikanaji wa mitaji na maeneo ya kufanya biashara hizo. Wajasiriamali waweze kupata mafunzo, mitaji, utaalamu na usimamizi wa biashara zao hasa wakati wa mwanzoni. Hawa wapunguziwe utitiri wa leseni, kodi na masharti kandamizi ambayo huongeza gharama wakati wa kuanzisha biashara kabla hawajapata faida.
Wafanyakazi walipwe viwango stahiki. Watu wanahitaji kuendesha maisha yao vizuri. Haitakiwi walipwe chini ya kiwango kwani hawataweza kufanya kazi vyema kwa sababu ya gharama za maisha. Pia watakimbilia nchi ambazo zitawalipa vyema. Pamoja na kwamba uchumi unaokua mishahara inapanda kwa haraka, ni vyema wazingatiwe kwenye maslahi yao. Sambamba na hilo upatikanaji wa huduma za kijamii utasaidia kupunguza gharama za maisha kwao. Kwa mfano, huduma za afya,maji, elimu ya gharama nafuu, nishati endelevu na ya bei nafuu na uhakika wa chakula.
Serikali ikusanye kodi. Ili tupate huduma za jamii kama afya, maji, nishati pamoja na miundombinu ni muhimu ikusanye kodi stahiki. Tanzania niitakayo itumie fedha kwa busara. Mitaji isaidie wazalishaji na watoaji wa huduma za kisasa, bunifu kwenye kilimo na viwanda. Izibe mianya yote ambayo wajanja na wanyonyaji wanaitumia kukwepa kodi. Kuweka adhabu kubwa na sheria kali kwa wote ambao wamebainika kufanya makosa hayo.
Ubunifu, sayansi na teknologia. Tunahitaji teknolojia mpya, viwanda vipya na biashara mpya. Ubunifu ndio uti wa mgongo wa nchi. Tuunge mkono jitihada za watanzania wabunifu mbao wamejikita kutatua changamoto tunazokutana nazo katika jamii yetu. Kamwe tusiwapuuze watu wa aina hii. Tuwape msaada kufanikisha ubunifu wao, kwani matatizo ya dunia ya sasa yanatatuliwa na ubunifu. Wabunifu wamekuwa na kilio cha kuhangaika muda mrefu pasipo kupata msaada na fedha kwa ajili ya kukamilisha ubunifu walio nao. Wengi pia wamehamia nchi nyingine na ubunifu walionao umetumika kwa faida ya wengine.
Tuzalishe bidhaa tunazoagiza Zaidi. Ni rahisi kujua bidhaa tunazoziagiza kwa kuwa zinapita kwenye bandari zetu na usafiri wa Anga. Ili tusitumie fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa nje, inatubidi tufanye tathmini ili kuweza kuzalisha bidhaa tunazoagiza zaidi kwa ubora. Hii itasaidia upatikanaji wa bidhaa zenyewe, ajira hasa kwa vijana za muda mrefu na muda mfupi na pia kukuza uchumi wa nchi yetu. Kwa mafano; badala ya kuagiza bidhaa za chakula na mazao ya mifugo ambazo tunaweza kuzalisha hapa nchini. Ni vyema kuweka miundombinu rafiki na tafiti ili kusaidia wakulima wetu kuzalisha, kuhifadhi, kuchakata na kutoa bidhaa mbali mbali za vyakula. Hili litaongeza usalama wa chakula nchini, uhakika wa upatikanaji na usambazaji. Tanzania isibaki kuwa wazalishaji wa malighafi za kulisha viwanda vya watu wengine bali kuweza kutumia malighafi hizo na kuzalisha bidhaa husika. Japo mchakato huo utachukua muda lakini kuanza safari hiyo ni muhimu sana.
Tulide mazingira na rasilimali asili. Utakubaliana nami athari za viwanda na mabadiliko ya tabia nchi imeleta hasara kubwa sana katika nchi za wenzetu, jambo hili limepelekea wao kuingia gharama kubwa sana kutunza na kuhifadhi mazingira. Nchini kwetu rasilimali asili zinatuletea pato kubwa kupitia utalii. Ni jukumu la kila mmoja wetu kulinda na kutunza mazingira. Kuwa na nishati mbadala pia kutaongeza uhifadhi wa mazingira kwani tuatapunguza ukataji wa miti na kuzuia nchi yetu kupoteza uoto wa asili na kugeuka jangwa.
kuondosha umasikini, ingawa jitihada kubwa zimefanyika katika kuondoa umasikini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Ni muhimu kusaidia wajasiriamali, kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi ambayo ndiye muajiri mkubwa. Kusaidia upatikanaji wa huduma za muhimu kama afya, maji na elimu. Itasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa watu katika umasikini uliokithiri.
Ni muhimu kwamba Tanzania ya ndoto yangu ikwe tayari kukubali mabadiliko. Tutakapo fanya mabadiliko hayo yatatuletea matunda tuliyokusudia. Haya yote yanawezekana ikiwa tutafanya kazi kwa pamoja kufikia malengo haya.
Mchoro: Tanzania ya Ndoto yangu. chanzo, mwandishi