DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 42,265
- 105,470
Habarini wakuu,
Ni wasaa wetu pia sisi wababa na WA mama wenye nyumba za kupangisha tupate uwanja wetu WA kujadili fursa,uzoefu na changamoto zinazoikabili hii biashara yetu kongwe ya kupangisha.
UZOEFU WANGU ni HUU.
1. CHANZO kikuu Cha migogoro mingi Kwa wapangaji ni umeme,choo na maji. Ukiweza kuwatenganishia hivyo, utajiepushia Vikao vya hovyo Kila mara na wapangaji wako.
2. Wapangaji wengi WA vyumba vya Bei ndogo (visivyo na finishing nzuri), ndo huwa wanasumbua sana kulipia Kodi Kwa wakati.
3. Wapangaji wengi WA vyumba vya Bei kubwa, Huwa Sio washindaji sana WA nyumbani. Hivyo Nyumba Yako haichakai.
4. Wapangaji wengi WA vyumba vya Bei kubwa, ni Mara chache sana ukute wamebandika magazeti ukutani, wanalala na baiskeli/pikpiki, gunia la mkaa au gunia la mahindi.
5. Watumishi wengi WA serikali ni walipaji wazuri WA Kodi Kwa wakati, isipokua TU kwa maaskali polisi na wanajeshi.
6. Ukipata Wapangaji WA kisabato au wale waislamu Safi wenye msimamo mkali, ni wasafi mno WA kutunza mazingira ya nyumba.
7. Wapangaji wengi WA single room, wengi wao hawana MKE/mume.
Kama unapendelea sharti la "lazima uwe mke/mume" , Sio vyema kujenga vyumba vya single room vingi kupangisha.
8. Wapangaji wengi WA single room, wanachakaza sana nyumba, tofauti na wale WA Chumba na sebule au nyumba nzima (Wanajaza sana vitu).
9. Nyumba yeye tiles, Kama unawapangaji wenye pikipiki, wajengee sehem maalum ya kulaza pikipiki zao nje ya vyumba vyao. zinaharibu sana tiles.
10. Ukijenga Nyumba ya wapangaji, jitahidi nje mlangoni pa kuingilia pawe na Baraza lenye paa, mvua na jua vinachakaza sana milango.
11. Kama mpangaji anataka kubadilisha rangi ya Chumba chake, usimruhusu atumie rangi ya mafuta. Inasumbua sana kukarabati pindi atakapohama.
(Atumiwe ya maji au wash&wear)
12. Kuepusha nyumba Yako kutobolewa tobolewa na misumari, wawekee wapangaji wako enga za Nguo na pazia, vyumbani na vyooni.
13. Kuepusha kuchakaza paa lako, wajengee wapangaji sehemu maalum ya kugongea madishi ya ving'amuzi vyao.
14. Kuepusha kutoboa toboa gypsum bodi Yako au madirisha Yako, jitahidi kuwawekea Tvswitch Kwa ajili ya kuvushia waya WA king'amuzi. (Weka na waya WA dish kabisa utokee nje, akifika aunge na kuchomeka TU)
15. Nyumba ya kupangisha ikishajaa sana Wamama wengi (hasa wanaoshinda nyumbani) jiandae kuitwa kusuhisha kesi za Kila mara.
Mengine tueendelee kufunguka ndani ya Uzi......