Mama Mgwhira asisitiza kwamba hajaachia Uenyekiti wa ACT Wazalendo hadi Juni 15

Kiongozi mkuu anatafuta njia ya kujisafisha ndio maana kamuondoa faster , ila ameshachelewa watu wameshang'amua mbichi na mbivu ni zipi.
 
Atuambie kwanza uataratibu uliotumika kwenye uteuzi wake wa mkuu wa mkoa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Anna Mgwira amesema yeye hajapinga kuondolewa uenyekiti wa ACT wazalendo ila amepinga utaratibu uliotumika.

Hapingi utaratibu kwa ajili yake ila ni utaratibu unaotakiwa kuwa kwenye vyama vyote, kuwamteuliwa wa mkutano mkuu hutenguliwa na mkutano mkuu, mteuliwa wa halmashauri kuu pia hutenguliwa na halmashauri kuu na ACT wamefanya haraka mno na alikuwa ameshawaomba wakutane tarehe 15 lakini wakaharakisha

Amewashangaa waandishi wa habari kuchukua habari nusu na kuacha habari za muhimu kwa maendeleo

Chanzo: Millard Ayo
Kwani yeye alivyokubali haraka haraka kuwasaliti wenzie alifuata utaratibu?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mama viya ya madaraka haijawahi kumuacha mtu salama, endelea na upande mpya fanya kazi ya wananchi uliyoteuliwa matamko ya ACT, achana nayo..huwezi tumikia mabwana wawili, hivi kwa mfano wakuache ifike muda wakuombe uitishe mkutano wa ACT utafanya hivyo? utahudhuria au ndio utatoa udhuru na kutuma muwakilishi?! Acha maneno weka kiti pembeni.
 
Wakae tarehe kumi na tano huku yeye alikubali uteuzi haraka bila hata kukijulisha chama chake? chagua moja mama kunyoa ama kusuka , huwezi kutumikia mabwana wawili., vikao vya ccm uongoze halafu uhudhurie vikao vya chadema pia
 
Kesho vichwa vya habari kwenye magazeti vitasomeka kama ifuatavyo:-

1- MAGUFULI ASABABISHA MPASUKO ACT
2- ACT WAZALENDO, YAPASUKA RASMI
3- MAGUFULI ASAMBARATISHA ACT WAZALENDO
4- ANNA AKAMILISHA MISSION NA KUREJEA CCM
5- ZAWADI YA U-RC YASABABISHA MTAFARUKU NDANI YA ACT
 
Huku ataka na huku ataka ankula huku!

Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Anna Mgwira amesema yeye hajapinga kuondolewa uenyekiti wa ACT wazalendo ila amepinga utaratibu uliotumika.

Hapingi utaratibu kwa ajili yake ila ni utaratibu unaotakiwa kuwa kwenye vyama vyote, kuwamteuliwa wa mkutano mkuu hutenguliwa na mkutano mkuu, mteuliwa wa halmashauri kuu pia hutenguliwa na halmashauri kuu na ACT wamefanya haraka mno na alikuwa ameshawaomba wakutane tarehe 15 lakini wakaharakisha

Amewashangaa waandishi wa habari kuchukua habari nusu na kuacha habari za muhimu kwa maendeleo

Chanzo: Millard Ayo
 
Waambie Mama, hivi vyombo vya habari ni shida kubwanchini. Hawajali kweli kwa sana tu maendeleo ya wananchi, hata kutupatia habari nzuri za kupaisha nchi bali udaku zaidi.
Hata mimi nawashangaa sana waandishi wa habari kuacha habari nzuri za maendeleo zinazomhusu Bashite halafu wanaenda kung'ang'ana na habari za "kipuuzi" zinazohusu mwenyekiti wa chama cha upinzani kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa!
 
ACT na CUF tayari bado Chadema, Dkt Mashinji amyooshe Suti ya kuapishiwa Ikulu Muda wowote JPM anaamsha Dudu!

Naota Wimbo la BAVICHA wakisikia hii

'Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Dkt Mashinji Katibu Mkuu wa Chadema kuwa Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuanzia leo'
 
Back
Top Bottom