Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 52
- 137
MKe wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi amesema Zanzibar inaendelea kuchukua juhudi maaluum za kudhibiti maradhi ya kuambukiza yanayowapata kinamama kipindi cha ujauzito.
Amesema, juhudi hizo zinalenga kuhakikisha ustawi wa mama na mtoto na udhibiti wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo Ukimwi, kifua kikuu na utapiamlo.
Soma Pia: Mama Mariam Mwinyi awasilisha juhudi za Serikali na ZMBF Uingereza
Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye idadi kubwa ya kinamama wanaojifungua, hivyo juhudi za pamoja za wadau na mashirika ya kimataifa zinahitajika kulipa kipaumbela suala la ustawi wa mama wajawazito na watoto.
Halikadhalika, amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inashirikiana na Taasisi ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation” (ZMBF) na kwamba wataendeleza programu tofauti ambazo tayari zimeanza kuleta mafanikio ya kunusuru maisha ya mama na mtoto ili kufikia malengo yaliyomo kwenye Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2025 na ile ya dunia ya 2030.
Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa jamii, sekta binafsi na taasisi za kimataifa kuendeleza juhudi za pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa kwa kila mdau kutimiza wajibu wake kwenye eneo lake kwa dhamira ya kuwajengea mazingira bora kinamama wakati wa ujauzito, kujifungua na kuwa na uhakika maisha ya mtoto anayezaliwa.
Kongamano hilo la siku tatu litahitimishwa kwa kutolewa ripoti ya miaka mitano ya Mradi wa Udhibiti wa Afya ya mama na mtoto na kukinga na maradhi ya TB, Ukimwi na Malaria.