Mama Yangu Kanikimbizia Mchumba Wangu!
Mimi ni binti wa miaka 30, sijaolewa ila niko kwenye mahusiano na Kaka mmoja huu ni mwaka wa saba. Mwaka jana tuliongea kuhusu ndoa akaniambia itakua mwaka huu, basi nilikubali nakukaa kimya, lakini mwezi wa sita alisimamishwa kazi hivyo nilishindwa kumuambia kuhusu mambo ya ndoa kwani alikua hayuko sawa kiakili kabsia.
Ilinibidi kunyamaza, lakini nyumbani walikua wnanipigia kelele sana, ilifikia kipindi mpaka Mama akanitafutia mwanaume kwakua tu alikua anahitaji mjukuu, basi kuna siku nilienda kuonana na huyo mwanaume, tukabaidlishana namba ili tu nimuangalie. Lakini nilijikuta namchukia tu kutokana na tabia zake na kwakua bado nilikua nampenda mwanaume wangu niliamua kumpotezea.
Mwezi wa 8 mwanaume wangu alirudi kazini, akawa sawa na kuniambia kuongea na nyumbani kuhusu ndoa, kweli nilifanya hivyo, lakini kabla hawajaja kwetu kuna siku akakuta meseji zangu na yule mwanaume, zilikua meseji za zamani wakati Mama aaniunganisha naye, nilijua nishazifuta lakini sijui nini kilitokea basi nikawa sina namna zaidi ya kumuambia ukweli.
Nikamuambia kuwa nyumbani walinitafutia mwanaume lakini baada ya kuongea naye mimi nilimkataa, aliniuliza inamaana ungemnkuta ni mzuri ungeenda kuolewa naye, nilibaki kimya, tuligombana sana, aliumia sana alikua mpaka analia kwa hasira mwisho akaniambia hahitaji tena kunioa kwani kama tatizo kidogo tu nimetaka kumaucha vipi tukiingia kwenye ndoa.
Kakatisha kila kitu, kachukua kila kitu chake na kunirudishia kila kitu changu, nimejaribu kumuomba msamaha, nimetumia rafiki zake lakini wapi. Naumia sana kwani tulikua vizuri sana, ananijali, ananihudumia yaani kila kitu kilikua sawa lakini sasa hivi hawezi kuwa na mimi, naomba ushauri wako sijui nifanye nini Kaka kumrudisha kwani nampenda sana nilionana na huyo mwanaume mwingine kwaajili ya Mama tu.