Malipo ya Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption

Status
Not open for further replies.
Kumbe NAO ipo ili ninyi na wanenu muendelee kula! Haiwezekani TAASISI ya UMMA ikazikagua taasisi nyingine za umma. Tulikuwa na TAC kwa ajili ya mashirika ya umma. Karibu yote hayapo sasa na TAC yenyewe. Tuna COASCO kwa ajili ya vyama vya ushirika. Hakuna chama cha ushirika kilicho na afya.

kaka wewe ni mfanyakazi,mfanyabiashara au mkulima???kama ni mmoja kati ya hayo mambo lazima unafanya kwajili ya familia yako ile bwana. iyo ndo africa jinsi ilivyo dts y hakuna mambo ya ku volunteer africa,tunafanya kazi kwajili tule
well suala la NAO kua taasisi ya umma ni ttz la siasa na system,mana INTOSAI standards inataka NAO iwe independent ila utumishi na ikulu hawataki kabisa hayo mambo ili waweze kuiba hela za wananchi,kwaiyo ndo ujinga wa wanasiasa wetu huo
 
Bunge letu sasa liamke. Liache kufanya siasa peke yake. Limfanye CAG na NAO yake wawe huru. Liwafanye PCCB wawe huru. Wakamate na kushtaki watu moja kwa moja bila kupitia kwa DPP. Nchi inatafunwa hii si kawaida.
 
Mdondoaji, naomba na mimi nitoe my one cent kwa kukuuliza swali dogo tu, je huu ushahidi uliotolewa dhidi ya PPF unaafiki ni wa kweli au ni za mtu tu kujitungia na hakuna ukweli wowote. Kama ni kweli, je yawezekana hali kama hiyo hiyo ikatokea ndani ya mashirika mengine ? Na ikitokea ni hivyo kwa nini kwa shirika kama NSSF hali iwe nafuu kama si kuwa mbaya zaidi ?

Mag3,

Nikuulize swali kujibu swali lako kuna ushahidi wowote wa malipo ya kifisadi kwa wakuu wa NSSF au wafanyakazi ulitolewa hapa JF? Ikiwa kama upo naomba unionyeshe. Of course hata huu unaotolewa hapa unaweza kuwa umetengenezwa ila report nyingi zilizopita nyuma kama magazeti na baadhi ya thread zinaonyesha kuna uwiano wa karibu hapa. Hivyo basi nikuulize je watu wote wakuseme wewe (ni mfano tu nikimaanisha PPF) huoni kama pengine unaweza kuwa wewe (yaani PPF) ndio tatizo.
 
Aisee...nimefumbuka maskio leo! Yanafanana kimatamshi bana, ni rahisi kweli ku-confuse...aaaaggggrrr...:attention:
Senksi nimegonga mkuu!
mzee mwenzangu; ukiamini hawa ni Watanzania wenzetu utafanya makosa; hawa ni Tunaowazania wenzetu!
 
Mwanakijiji nilicho na hakika nacho ni kuwa haya ya PPF ni kama ligi ya chandimu tu kwa NSSF inayocheza ligi kubwa - hata hivyo naendelea kusubiri majibu ya Mdondoaji.

Mkuu,

Toa vithibitisho badala ya kufanya mkusanyiko wa habari. Umejuaje ya NSSF ni shughuli nzito wakati wewe kama mimi huna mahali unaweza kulithibitisha hilo.
 
Mzee Mwanakijiji: Shikamoo kaka!

Mzee Mwanakijiji Nakupa salute kaka 2.13 Billion kwa malipo ya wakurugenzi sita, na kati ya hizo 1.89 malipo ya kuondokea nayo baada ya kustaafu. Halafu mtumishi wa umma akienda kudai mafao yake wanamlipa 40,000 kwa mwezi na kejeli kwamba mfuko hauna hela!!!. Tanzania kweli tunataniana!!!
 
Mzee mifuko mingine inafanya ufisadi kwa namna nyingine kabisa kupitisha fedha haramu;

Fikiria mfuko unajenga nyumba kwa mkopo wa milioni 20 kwamba baadaye aliyejengewa ataulipa.
Baada ya muda aliyejengewa anashindwa kulipa
Mfuko unaichukua hiyo nyumba
Unaipiga bei kwa milioni 5
Guess nani ananunua.. !!

Halafu mfuko unajenga kwingine..

Hii ni mbinu mojawapo..

Hivi ni nani anafanya auditing ya mfuko wa afya wa taifa, eti mwanakijiji...
 
After this report I will retire from this kind of investigative political activism (including popular columns in some major newspapers) after almost six years of a very emotional engagement in Tanzania's political arena. Over the years, I have created many friends to last a life time. Unfortunately, I have created many enemies to last a lifetime as well - some may be even in the after life. I don't know how long I'll be in that retirement before something push me back in the fight. Between now and then we have work to do.[/I]

Hivi Mwanakijiji unajua ni watu wangapi, wanajikusanya ili waunge mkono mapambano kutokana na hamasa wanayopata kutoka kwako. We retire, lakini ujue una-retire na mamia ya watu nyuma yako...
 
Wengi wao kati ya hao waliolipwa hayo mamilioni walishaondoka hapo PPF. Mtawapata wapi?
 
Hapa naona ni kizunguzungu tu kwangu. Naomba mtu anisaidie hili. Nimestaafu kutoka kampuni ya Umma mwaka juzi nikiwa na Umri wa Miaka 50 na nikapewa shilingi MILIONI TANO NA LAKI MBILI NA senti kadhaa kama NUSU ya kiinua mgongo changu kwa miaka KUMI NA NANE niliyofanya kazi kwenye kampuni hiyo.
Nimeambiwa kuwa NUSU iliyobaki nitalipwa shilingi LAKI MOJA MIA MBILI NA TANO kila mwezi kama kiinua mgongo changu kuanzia JULAI 2014 nitakapokuwa nimetimiza Miaka 55!!
Kwa ulaji huu ninaanza kuhisi kuwa hela hiyo itakuwa hadithi wakati utakapofika. Ninatafuta namna ya kupata changu kabisa ili niondokane na presha ninayopata kila mara ninaposoma ulaji kama huu kwenye taasisi inayosemekana kunitunzia pesa zangu.
Naweza kufanaya nini ili nipewe changu kabisa????
 
Alifichwa hii ripoti
Hahahahahahaa.......

Ripoti ni ya Mkaguzi. Mkaguzi atafichwaje ripoti?

Soma madai ya Mzee Mwanakijiji:

Mzee Mwanakijiji: Wakaguzi wa nje (External Auditors) wa TAC Associate wanaofanya Audit kwa niaba ya Controller and Auditor General (CAG) wameeleza kuwa malipo hayakuwa sahihi. Walipeleka ukaguzi wao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Gray Mgonja ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi PPF ambaye hakuufanyia kazi - labda kutokana na matatizo yake mwenyewe. Pia walipeleka nakala kwa CAG.

Upo?

Sasa CAG alipotoshwa na nani nini?

Na jana Mwanakijiji kasema hii ni "rushwa." Nyaraka aliyobandika leo inasomeka kwamba PPF walifata taratibu zao kwa kupitisha maazimio kwa vikao. Na kama PPF wanapewa mamlaka ya kujitungia taratibu basi wamefata sheria!

CAG alipotoshwa nini, na rushwa alitoa nani?
 
Mwanakijiji nilicho na hakika nacho ni kuwa haya ya PPF ni kama ligi ya chandimu tu kwa NSSF inayocheza ligi kubwa - hata hivyo naendelea kusubiri majibu ya Mdondoaji.
Wakuu

One step at a time... ngoja yaishe haya ya PPFna NSSF italetwa tu na wenyewe yakwiazidi, tusihamishe magoli tuta-dilute mada

Pia kuhusu NSSF, huko ni balaa maana kwa fitna ni nambari wani
 
Jana tumeanza kuangalia suala la malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa wakurugenzi sita ndani ya shirika la Pensheni la Mashirika ya Umma (PPF). Tuliona baadhi tu ya invoices za malipo kwa Wakurugenzi hao. Malipo hayo toka mwanzo yalizua mgogoro ndani ya PPF baada ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu kutotaka kulipa na kujikuta akigongana na viongozi wake wa juu (ambao walikuwa walengwa wa malipo hayo). Pamoja na nia yake njema ya kujaribu kuliokolea shirika fedha hizo na kujaribu kusimamia utawala bora Mhasibu huyo aliondolewa makao makuu na baada ya kumrusha huko na huko amejikuta akirushwa Mbeya ambako juhudi za mwisho sasa hivi zinataka kuhakikisha anatolewa kabisa kwenye Shirika. Jitihada zake hazijapata mtetezi ndani ya serikali. Kukosekana kwa sheria ya kuwalinda Whistleblowers ni kizuizi kikubwa kwa watu kama hawa kujitokeza hadharani kwani ndio wanapata makali ya hasira ya viongozi wanaoumbuliwa.

Kutokana na mgongano uliotokea baada ya malipo kufanyika Shirika ikabidi liitishe Kikao cha ndani na ajenda ikiwa ni kujadili ripoti ya Wakaguzi wa Nje waliotumwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Barua hii sehemu kubwa inaelezea kile ambacho wakaguzi hao walikipata na mapendekezo yao.

Wakaguzi wa nje (External Auditors) wa TAC Associate wanaofanya Audit kwa niaba ya Controller and Auditor General (CAG) wameeleza kuwa malipo hayakuwa sahihi. Walipeleka ukaguzi wao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Gray Mgonja ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi PPF ambaye hakuufanyia kazi - labda kutokana na matatizo yake mwenyewe. Pia walipeleka nakala kwa CAG. Angalia ukurasa wa nane wa nakara ya ripoti ya TAC


Ukipitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu ya 2007/2008 (kipindi cha Malipo haya) huwezi kuona yale ambayo yanatajwa katika maoni ya wakaguzi hawa ambayo kama yangepewa uzito unaostahili leo hii (baada ya malipo mengine kufanyika kama inavyotarajiwa) tusingekuwa tunayazungumzia.



Ripoti Kamili Inakuja siku chache zijazo - Kurasa karibu 50 ambazo zitashtua watawala wetu. Tukitoka hapa tunaenda kule kwingine ili tusije kuonekana tunaing'ang'ania PPF!



Kundi hilo lililolipwa kiasi hicho ni hawa wafuatao na kiasi cha fedha ambazo walijilipa kama sehemu ya “mafao” yao kwa mwaka 2008.

1. Baduru Msangi -Mkurugenzi wa Pensions Tshs. 220,000,000 (Milioni 220)
2.Hossea Kashimba -Chief Internal auditor Tshs. 220,000,000 (Milioni 220)
3. Michael Mjinja- Director of Commercial Services-Tshs 172, 000,000(Milioni 172)
4. Charles Chenza-Director of Investiments- Tshs 172, 000,000 (Milioni 172)
5. Martin Mmari Director of Finance Tshs. 172,000,000 (Milioni 172)
6. Carina Wangwe-Director of computer Services. Tshs. 130,000,000 (Milioni 130)

Mwaka 2010 Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Erio alilipwa shilingi 520,000,000 yaani shilingi Milioni 520! Hii ni sasa na nusu bilioni!


Kwa kadiri ya kwamba Serikali itaendelea kukaa kimya bila kuonesha kuchukua hatua tutaendelea kufunua hapa JF sakata hili kwa kuendelea kuweka hadharani nyaraka mbalimbali zinazohusiana na utendaji mbovu katika mashirika haya ya hifadhi ya jamii... Hatua zozote za kuchunguza PPF ni muhimu kuhusisha mifuko yote mingine. Natumaini Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma itakuwa na la kusema japo sijui kwanini itakuwa hivyo sasa kwani jambo hili lina miaka mitatu sasa na hasa tukizingatia kuwa malipo mengine yatakuwa yamefanyika jana na mengine kufanyika leo huku mmoja wa waliolipwa safari iliyopita atadai kulipwa tena as "end of employment" kwani anakwenda Bodi mpya kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


carina.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom