Malipo ya Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption

Status
Not open for further replies.

kaka wewe ni mfanyakazi,mfanyabiashara au mkulima???kama ni mmoja kati ya hayo mambo lazima unafanya kwajili ya familia yako ile bwana. iyo ndo africa jinsi ilivyo dts y hakuna mambo ya ku volunteer africa,tunafanya kazi kwajili tule
well suala la NAO kua taasisi ya umma ni ttz la siasa na system,mana INTOSAI standards inataka NAO iwe independent ila utumishi na ikulu hawataki kabisa hayo mambo ili waweze kuiba hela za wananchi,kwaiyo ndo ujinga wa wanasiasa wetu huo
 
Bunge letu sasa liamke. Liache kufanya siasa peke yake. Limfanye CAG na NAO yake wawe huru. Liwafanye PCCB wawe huru. Wakamate na kushtaki watu moja kwa moja bila kupitia kwa DPP. Nchi inatafunwa hii si kawaida.
 

Mag3,

Nikuulize swali kujibu swali lako kuna ushahidi wowote wa malipo ya kifisadi kwa wakuu wa NSSF au wafanyakazi ulitolewa hapa JF? Ikiwa kama upo naomba unionyeshe. Of course hata huu unaotolewa hapa unaweza kuwa umetengenezwa ila report nyingi zilizopita nyuma kama magazeti na baadhi ya thread zinaonyesha kuna uwiano wa karibu hapa. Hivyo basi nikuulize je watu wote wakuseme wewe (ni mfano tu nikimaanisha PPF) huoni kama pengine unaweza kuwa wewe (yaani PPF) ndio tatizo.
 
Aisee...nimefumbuka maskio leo! Yanafanana kimatamshi bana, ni rahisi kweli ku-confuse...aaaaggggrrr...:attention:
Senksi nimegonga mkuu!
mzee mwenzangu; ukiamini hawa ni Watanzania wenzetu utafanya makosa; hawa ni Tunaowazania wenzetu!
 
Mwanakijiji nilicho na hakika nacho ni kuwa haya ya PPF ni kama ligi ya chandimu tu kwa NSSF inayocheza ligi kubwa - hata hivyo naendelea kusubiri majibu ya Mdondoaji.

Mkuu,

Toa vithibitisho badala ya kufanya mkusanyiko wa habari. Umejuaje ya NSSF ni shughuli nzito wakati wewe kama mimi huna mahali unaweza kulithibitisha hilo.
 
Mzee Mwanakijiji: Shikamoo kaka!

Mzee Mwanakijiji Nakupa salute kaka 2.13 Billion kwa malipo ya wakurugenzi sita, na kati ya hizo 1.89 malipo ya kuondokea nayo baada ya kustaafu. Halafu mtumishi wa umma akienda kudai mafao yake wanamlipa 40,000 kwa mwezi na kejeli kwamba mfuko hauna hela!!!. Tanzania kweli tunataniana!!!
 

Hivi ni nani anafanya auditing ya mfuko wa afya wa taifa, eti mwanakijiji...
 

Hivi Mwanakijiji unajua ni watu wangapi, wanajikusanya ili waunge mkono mapambano kutokana na hamasa wanayopata kutoka kwako. We retire, lakini ujue una-retire na mamia ya watu nyuma yako...
 
Wengi wao kati ya hao waliolipwa hayo mamilioni walishaondoka hapo PPF. Mtawapata wapi?
 
Hapa naona ni kizunguzungu tu kwangu. Naomba mtu anisaidie hili. Nimestaafu kutoka kampuni ya Umma mwaka juzi nikiwa na Umri wa Miaka 50 na nikapewa shilingi MILIONI TANO NA LAKI MBILI NA senti kadhaa kama NUSU ya kiinua mgongo changu kwa miaka KUMI NA NANE niliyofanya kazi kwenye kampuni hiyo.
Nimeambiwa kuwa NUSU iliyobaki nitalipwa shilingi LAKI MOJA MIA MBILI NA TANO kila mwezi kama kiinua mgongo changu kuanzia JULAI 2014 nitakapokuwa nimetimiza Miaka 55!!
Kwa ulaji huu ninaanza kuhisi kuwa hela hiyo itakuwa hadithi wakati utakapofika. Ninatafuta namna ya kupata changu kabisa ili niondokane na presha ninayopata kila mara ninaposoma ulaji kama huu kwenye taasisi inayosemekana kunitunzia pesa zangu.
Naweza kufanaya nini ili nipewe changu kabisa????
 
Alifichwa hii ripoti
Hahahahahahaa.......

Ripoti ni ya Mkaguzi. Mkaguzi atafichwaje ripoti?

Soma madai ya Mzee Mwanakijiji:

Mzee Mwanakijiji: Wakaguzi wa nje (External Auditors) wa TAC Associate wanaofanya Audit kwa niaba ya Controller and Auditor General (CAG) wameeleza kuwa malipo hayakuwa sahihi. Walipeleka ukaguzi wao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Gray Mgonja ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi PPF ambaye hakuufanyia kazi - labda kutokana na matatizo yake mwenyewe. Pia walipeleka nakala kwa CAG.

Upo?

Sasa CAG alipotoshwa na nani nini?

Na jana Mwanakijiji kasema hii ni "rushwa." Nyaraka aliyobandika leo inasomeka kwamba PPF walifata taratibu zao kwa kupitisha maazimio kwa vikao. Na kama PPF wanapewa mamlaka ya kujitungia taratibu basi wamefata sheria!

CAG alipotoshwa nini, na rushwa alitoa nani?
 
Mwanakijiji nilicho na hakika nacho ni kuwa haya ya PPF ni kama ligi ya chandimu tu kwa NSSF inayocheza ligi kubwa - hata hivyo naendelea kusubiri majibu ya Mdondoaji.
Wakuu

One step at a time... ngoja yaishe haya ya PPFna NSSF italetwa tu na wenyewe yakwiazidi, tusihamishe magoli tuta-dilute mada

Pia kuhusu NSSF, huko ni balaa maana kwa fitna ni nambari wani
 

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…