DOKEZO  Malalamiko yaendelea kuhusu malipo ya 'Mchango wa Uendeshaji wa Shule Tsh 65,000' licha ya Serikali kufuta ada

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580
Ujumbe wa Mdau ambaye mtoto wake anasoma kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ruvu ametoa povu:

Jamani tusaidieni kupaza sauti. Tuliambiwa ada ya shule zimeondolewa lakini bado wazazi tunatakiwa kulipa Tsh. 65,000/= kama pesa ya uendeshaji ili hali fomu ya kujiunga inamtaka kwenda na mahitaji yote kama ream paper, dissecting kit.

Sasa hii pesa ni uendeshaji wa nini? Kama ada ipo serikali iseme wazazi tujue moja.
Ruvu.jpg

Pia soma:
  1. DOKEZO - √ - Shule ya Msingi Tumaini ya Tabata Kimanga Wanafunzi wasiochangia Tsh. 800 wanatolewa Darasani
  2. DOKEZO - √ - Wanafunzi wa kidato cha tano kukataliwa kisa hawajamaliza michango ni usumbufu kwa wanaotoka mbali
  3. DOKEZO - √ - Wazazi wa wanafunzi Shule ya Sekondari BUJUNANGOMA, tumechoka na Michango, Rushwa, Utumikishwaji wa watoto wetu shuleni
  4. DOKEZO - √ - Wanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Chanika wazuiliwa kuingia darasani kutokana na kutochangia 500 ya masomo

UFUATILIAJI WA JAMII FORUMS
Uchunguzi uliofanywa na JamiiForums umebaini kuwa katika fomu zote za kujiunga na Kidato cha Tano katika zote Shule za Serikali kuna maelekezo ya michango hiyo.

Maelekezo ya fomu yanayosomeka “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI TANZANIA” kutoka TAMISEMI yanaonesha Shule za Bweni kiasi kinachotakiwa kulipwa ni Tsh. 65,000 wakati kwa Shule za Kutwa ni Tsh. 35,000.

Maelekezo hayo yanapatikana kupitia: UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2023
Soma hapa majibu ya Waziri: Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda apiga marufuku Shule kuzuia Wanafunzi ambao hawajalipa fedha za michango
 
Kwakweli ni wizi mtupu! Nimesoma joining instructions za shule zoote za A level zinataka mwanafunzi alipe kiwango fulani cha fedha kuanzi sh. 80,000 na nyingine hadi 150,000/ sasa cha kujiuliza, hii hela ya nini ili hali karo zimefutwa? Na karo yenyewe ilikuwa 20,000
 
Mwambie huyo mzazi aache ujinga. Sh 65000 Ni nini kwa elimu itakayomjenga mtoto wake? Halafu hiyo 65000 Ni kwa mwaka sio kwa wiki. Kwani yeye anakula ngapi, anahonga ngapi na bar anakunywa pombe ya sh ngapi kwa siku.

Yaani anataka azae tuuu halafu serikali imfanyie kila kitu?

Aache ujinga. Wazazi wengine wanalipa milioni tano Tanzania hii hii.

Aseme Kama Yuko kwenye list ya TASAF .
 
Hivi mnajua pamoja na nia nzuri ya serikali kufuta ada za shule lakini mzigo mkubwa unaziangukia shule husika.
Hiki kiasi ambacho serikali ya CCM inakitoa (EMBM) hakitoshi kabisa kuendesha taasisi za shule.
Shule zina hali mbaya sana kifedha, samani zimechakaa, vifaa vya kufundishia hakuna. Hapo bado kulipa fedha za ulinzi wa shule, maji, umeme na uendeshaji wa shule
Bila kuchangisha kwa wazazi shule hazitoboi na zitakuwa fukara kupindukia.
 
Ujumbe wa Mdau ambaye mtoto wake anasoma kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ruvu ametoa povu:

Jamani tusaidieni kupaza sauti. Tuliambiwa ada ya shule zimeondolewa lakini bado wazazi tunatakiwa kulipa Tsh. 65,000/= kama pesa ya uendeshaji ili hali fomu ya kujiunga inamtaka kwenda na mahitaji yote kama ream paper, dissecting kit.

Sasa hii pesa ni uendeshaji wa nini? Kama ada ipo serikali iseme wazazi tujue moja.
Yaani 65k kwa mwaka unataka usaidiwe? ......ujinga ni bora kuliko 65k ? Jaribu ujinga
 
fedha za ulinzi wa shule, maji, umeme na uendeshaji wa shule
Kuwa muwazi kwa hili jamani
1- mlinzi Ni sh ngapi kwa mwezi kwa mwaka Hawa kwa wanafunzi wote??
2--maji na umeme Ni Bei gani kwa mwezi na kwa mwaka pia Mana umeme najua Ni mwanga tu kumulika Ni hela ndogo mno.
3-- uendeshaji wa shule vipi ,yaani Ni Nini kinachohitajika hapa si waweke wazi kuwa serikali haiwezi kuendesha shule zake. Mkuu ana fungu lake,kuweni wakweli ama mnataka hela kijanja janja.
Lebo 5k,id 5k kweli hii thamani inafika. Na sio kuwa mnawapenda hao watt kuliko wazazi wao.
 
Unalinganisha gharama za umeme wa nyumbani sawa na kuendesha taasisi kama shule (angalia idadi ya majengo na pia vifaa vilivyopo shuleni ambavyo vinatumia umeme).

Kuhusu maji inategemea, baadhi ya shule hazipo kwenye mfumo wa maji eg. Dawasco, wananunua kwenye maboza.

Pia kuna suala la samani (meza na viti vya wanafunzi) na samani kwa ajili ya walimu, kumbuka vilivyopo vinachakaa na kuharibika kila wakati.

Kuna vifaa na kemikali za maabara kwa ajili ya kufundishia na pia kwenye mitihani ya kitaifa.

Kuna stationeries kwa ajili ya nyaraka mbalimbali za kufundishia na pia mitihani ya kila mwezi, nusu mihula na mihula pia.

Kuna ulinzi (idadi ya walinzi inategemea na ukubwa shule).

Kuna kusoma baada ya muda wa kazi (remedials) ambapo serikali inasisitiza uwepo wa remedials na ni lazima kwa kila shule.

Kumbuka mwalimu ni mtumishi wa serikali kama walivyo watumishi wengine hivyo muda wa kuingia ni saa 1:30 asubuhi na kutoka ni saa 9:30 alasiri. Hizo remedials zinaanza saa 9:30, hivyo mwalimu lazima alipww posho ya kutumia muda wa ziada. Hizo fedha zinatoka wapi?

Kuna masuala mazima ya uendeshaji wa taasisi za shule kama ukarabati, madawa ya binadamu na mambe mengine kadha ya kadha.

Fedha ambazo zinatolewa na Serikali katu haziwezi kuhimili hili hata kidogo

Walio nje ya system za uongozi wa shule wanaweza wasijue nini kilichopo ndani.

Bila kupata fedha za kuendesha shule nje ya ruzuku, uendeshaji unaweza kuwa mgumu sana na ndio maana shule nyingi kama sio zote zina madeni sugu na yasiyolipika kwa haraka kutoka kwa wazabuni
 
Tatizo wa Tanzania mnapenda siasa za kudanganywa. Serekali haiwezi kuhudumia Kila kitu, ukiona serikali imeahidi kukusaidia jambo Fulani ujue wanaajenda Yao ili ipite lazima wawalambishe utamu kidogo na wakishafanikisha kadri muda utakavyoenda utaona kabisa asali inaanza kuwa shubiri. Ipo siku ada zitarudishwa kabisa
 
Unalinganisha gharama za umeme wa nyumbani sawa na kuendesha taasisi kama shule (angalia idadi ya majengo na pia vifaa vilivyopo shuleni ambavyo vinatumia umeme).
Kuhusu maji inategemea, baadhi ya shule hazipo kwenye mfumo wa maji eg. Dawasco, wananunua kwenye maboza.
Pia kuna suala la samani (meza na viti vya wanafunzi) na samani kwa ajili ya walimu, kumbuka vilivyopo vinachakaa na kuharibika kila wakati.
Kuna vifaa na kemikali za maabara kwa ajili ya kufundishia na pia kwenye mitihani ya kitaifa.
Kuna stationeries kwa ajili ya nyaraka mbalimbali za kufundishia na pia mitihani ya kila mwezi, nusu mihula na mihula pia.
Kuna ulinzi (idadi ya walinzi inategemea na ukubwa shule).
Kuna kusoma baada ya muda wa kazi (remedials) ambapo serikali inasisitiza uwepo wa remedials na ni lazima kwa kila shule. Kumbuka mwalimu ni mtumishi wa serikali kama walivyo watumishi wengine hivyo muda wa kuingia ni saa 1:30 asubuhi na kutoka ni saa 9:30 alasiri. Hizo remedials zinaanza saa 9:30, hivyo mwalimu lazima alipww posho ya kutumia muda wa ziada. Hizo fedha zinatoka wapi???
Kuna masuala mazima ya uendeshaji wa taasisi za shule kama ukarabati, madawa ya binadamu na mambe mengine kadha ya kadha.
Fedha ambazo zinatolewa na Serikali katu haziwezi kuhimili hili hata kidogo
Walio nje ya system za uongozi wa shule wanaweza wasijue nini kilichopo ndani.

Bila kupata fedha za kuendesha shule nje ya ruzuku, uendeshaji unaweza kuwa mgumu sana na ndio maana shule nyingi kama sio zote zina madeni sugu na yasiyolipika kwa haraka kutoka kwa wazabuni
Basi Kama vipi serikali iseme imeshindwa kazi ibinafsishe shule zake.mana huku wanajinadi public kisiasa lakini kwa uhalisia haupo ivyo.wanapiga porojo tu. Ila mbona jpm hii michango haikuwepo,Mana walikuwa hawatoi hata Mia mbovu. So hapo na Hilo unaliongeleaje kaa hili
 
Ujumbe wa Mdau ambaye mtoto wake anasoma kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ruvu ametoa povu:

Jamani tusaidieni kupaza sauti. Tuliambiwa ada ya shule zimeondolewa lakini bado wazazi tunatakiwa kulipa Tsh. 65,000/= kama pesa ya uendeshaji ili hali fomu ya kujiunga inamtaka kwenda na mahitaji yote kama ream paper, dissecting kit.

Sasa hii pesa ni uendeshaji wa nini? Kama ada ipo serikali iseme wazazi tujue moja.
Neno ELIMU BURE hapa ni utapeli uliotukuka. Hiyo hiyo 65,000/- ndio ada yenyewe. Wanasiasa wamelitumia hili neno kupata cheap popularity.

Utapeli huu nilishawahi kuuona shule moja hivi iko maeneo ya Goba. Shule ni English Media yenye mazingira mazuri tu ya kusomea na hata ufaulishaji wake ni mzuri.

Hii shule niliambiwa Ada unatozwa laki 1 kwa mwaka mzima ila form ni 3.2mil. Cha ajabu kila unapomaliza darasa moja kwenda linalofuata lazima uchukue tena form.
 
Mwambie huyo mzazi aache ujinga. Sh 65000 Ni nini kwa elimu itakayomjenga mtoto wake? Halafu hiyo 65000 Ni kwa mwaka sio kwa wiki. Kwani yeye anakula ngapi, anahonga ngapi na bar anakunywa pombe ya sh ngapi kwa siku.

Yaani anataka azae tuuu halafu serikali imfanyie kila kitu?

Aache ujinga. Wazazi wengine wanalipa milioni tano Tanzania hii hii.

Aseme Kama Yuko kwenye list ya TASAF .
Acha dharau mkuu! Hujui chochote kuhusu maisha! Kama unajiona mambosafi uenda hujui nyuma yako kuna nini kilichokushikilia! Kwani karo ya shule za msingi na sekondari zilizofutwa na Magufuli ilikuwa shilling ngapi? Ilikuwa ndogo sana chini kabisa ya 65,000. Lakini angalia matokeo yake ni kuongezeka kwa uandikishwaji wa wanafunzi zaidi ya 250% kulikopelekea kuhitajika madarasa na madawati mengi! Narudia! Acha dharau! Wewe kama unajiona unahela ya rushwa na wizi na madawa ya kulevya na magodfathers, wengine hela yao ya halali wanaipata kwa kupambana! Kama karo ya serikali kuu imefutwa ambayo kimsingi ni ndogo, iweje shule au halimashauri zianzishe michango mikubwa kuliko karo? Hii haikubaliki na haina maana! Hoaxer
 
Basi Kama vipi serikali iseme imeshindwa kazi ibinafsishe shule zake.mana huku wanajinadi public kisiasa lakini kwa uhalisia haupo ivyo.wanapiga porojo tu. Ila mbona jpm hii michango haikuwepo,Mana walikuwa hawatoi hata Mia mbovu. So hapo na Hilo unaliongeleaje kaa hili
Hili limama sijui lilitokea wapi? Liongo na lijizi linawaza kuuza bandari tu!
 
Ujumbe wa Mdau ambaye mtoto wake anasoma kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ruvu ametoa povu:

Jamani tusaidieni kupaza sauti. Tuliambiwa ada ya shule zimeondolewa lakini bado wazazi tunatakiwa kulipa Tsh. 65,000/= kama pesa ya uendeshaji ili hali fomu ya kujiunga inamtaka kwenda na mahitaji yote kama ream paper, dissecting kit.

Sasa hii pesa ni uendeshaji wa nini? Kama ada ipo serikali iseme wazazi tujue moja.
Kilichoondolewa ni ada ila michngo mingine ilikuwepo kabla hata ada haijaondolewa.
Kama hiyo michango mwanzo haikwepo na imekuja baada ya ada kuondolewa basi ni sahihi kwake kulalamika ila kama sivyo basi atulie tu.
 
Acha dharau mkuu! Hujui chochote kuhusu maisha! Kama unajiona mambosafi uenda hujui nyuma yako kuna nini kilichokushikilia! Kwani karo ya shule za msingi na sekondari zilizofutwa na Magufuli ilikuwa shilling ngapi? Ilikuwa ndogo sana chini kabisa ya 65,000. Lakini angalia matokeo yake ni kuongezeka kwa uandikishwaji wa wanafunzi zaidi ya 250% kulikopelekea kuhitajika madarasa na madawati mengi! Narudia! Acha dharau! Wewe kama unajiona unahela ya rushwa na wizi na madawa ya kulevya na magodfathers, wengine hela yao ya halali wanaipata kwa kupambana! Kama karo ya serikali kuu imefutwa ambayo kimsingi ni ndogo, iweje shule au halimashauri zianzishe michango mikubwa kuliko karo? Hii haikubaliki na haina maana! Hoaxer
Imebidi nikae kwa kutulia.
 
Ujumbe wa Mdau ambaye mtoto wake anasoma kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ruvu ametoa povu:

Jamani tusaidieni kupaza sauti. Tuliambiwa ada ya shule zimeondolewa lakini bado wazazi tunatakiwa kulipa Tsh. 65,000/= kama pesa ya uendeshaji ili hali fomu ya kujiunga inamtaka kwenda na mahitaji yote kama ream paper, dissecting kit.

Sasa hii pesa ni uendeshaji wa nini? Kama ada ipo serikali iseme wazazi tujue moja.

Kwahiyo 65,000 ndo imekufanya uje kufungua uzi Mkuu?
Unadhani kuendesha shule ni jambo jepesi ambalo linaweza kuwa covered kwa ruzuku ya sh. 15,000 kwa mwezi?
Huo mchango ni sawa na sh. 5416 kwa mwezi
Hivi kwa akili ya kawaida sh. 5000 kwa mwezi inakutoa roho tena juu ya mwanao!
Lunch peke yake ama jioni ukikaa na washkaji huwa unaunguza 5000 ngapi?
 
Kwakweli ni wizi mtupu! Nimesoma joining instructions za shule zoote za A level zinataka mwanafunzi alipe kiwango fulani cha fedha kuanzi sh. 80,000 na nyingine hadi 150,000/ sasa cha kujiuliza, hii hela ya nini ili hali karo zimefutwa? Na karo yenyewe ilikuwa 20,000

A level karo ilikuwa 20,000?
 
Back
Top Bottom