Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Magembe,leo amezindua rasmi makumbusho ya Waziri Mkuu wa Pili wa Tanzania,Mzee Rashidi Kawawa a.k.a Simba wa vita katika eneo lililokuwa nyumba yake maeneo ya Bombambili Manispaa ya Songea,mkoani Ruvuma.
Waziri huyo alikuwa mgeni rasmi katika Sherehe ya Kumbukizi ya miaka 110 ya vita vya majimaji na Tamasha la utalii.
Sherehe hizi husherekewa kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka mashujaa wetu waliokufa wakitetea nchi hii,mnamo tarehe 27/02/1906,mashujaa wetu wapatao 66 walinyongwa na Wajeruman huko mjini Songea na kuzikwa katika makaburi mawili yaliyopo katika makumbusho hayo.
Jana tar 26,katika ukumbi wa Manispaa ya Songea,kulifanyika mawasilisho ya mada mbalimbali kutoka kwa wadau,ambapo mojawapo iliyowasilishwa na Dk.Nancy Rushohora mhadhiri wa Mtwara University, mada;Vita vya majimaji ni vita au Mauaji ya halaiki.