Makonda na sakata la madawa ya kulevya

Wanasema ukitaka kujua tabia au mwenendo wa mtu, angalia mwandiko wake, mavazi yake, mwondoko wake na pengine hata alivyopangilia chumba chake, kitanda chake n.k.

Posting yako inadhihirisha ulivyo na upeo mdogo katika kudadavua yanayojiri katika jamii. Na niseme ni bahati mbaya mno kwamba tuna watu wa namna yako, wasiona kuna kasoro kwa kuwa tu jambo limefanywa na swahiba. Ni bahati mbaya kwa kijana Makonda hata baada ya kuona jamii ilivyoshitukizwa, hajaweza kukaa chini na kutafakari ni nini kimekwenda mrama. Sawa na Siro, afande ambaye alitishwa wakati fulani na Makonda kuhusiana na Shisha, sasa hivi hapendi hata kutafakari hatima ya haya anayosukumiwa. Mwisho wa siku jamii (mimi na wewe) tutalipia yote haya. Wanaotuhumiwa watashitaki na watashinda, kodi zetu ndio zitawalipa. Makonda haoni kwamba ameyumbisha mapambano, anadhani yuko sahihi- katika taaluma ya ufundishaji, tunasema ujuzi sio kukariri na kuonekana kujua kila kitu (kukumbuka!) bali ni kujua chanzo cha taarifa, kuweza kuhoji kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Umenisikitisha tena! Ni kama Makonda alivyonisikitisha - kijana wa leo, anashindwa kuandaa ile orodha fupi tu kwa kuichapisha ili isiwe na ubishi wa kimwandiko- kukaa kitako na kuitaipu (eti anawaambia waandishi wa habari atawapa wao waichape vizuri), lakini orodha isiyo kamili hata chembe, majina ya bandia yasiyo na wenyewe, jina moja moja nk
Dogo wewe ni fala tena lofa wa malofa sidhani kama una mtarimbo wa haja
 
Dogo wewe ni fala tena lofa wa malofa sidhani kama una mtarimbo wa haja

Moderators- kweli hii lugha ni kuvumilika? Nimerudia posting yangu mara kadhaa ili kuona ni kwa jinsi gani nimemsababisha huyu Nd Tiku ajibu kwa kejeli na matusi. Tafadhali mkemee lugha hizi - zinatuharibia ukumbi- Where we dare to talk openly- haina maana kutumia lugha isiyo ya ustaarabu!
 
Mkuu watanzania hatuelewi hata tunataka nini! Tunaongozwa na mahaba ya watu badala ya national interests. Nilitegemea watz tuchimbe mikwara mitandaoni tukionya ole kwa don yeyote atakayethubutu kumgusa Makonda, badala yake tunaongoza kumtishia maisha yake! Makonda amethubutu, no matter amechukua approach ipi, ghafla limeibuka wimbi la ma - experts wa kupambana na madawa ya kulevya wakikosoa kila anachofanya na kuwaunga mkoni washukiwa. Hivi ni nani katuroga? Kabla makonda hajathubutu, hakuna aliyelichukulia serious suala hili, alipoibuka tu, wajuvi wa intelligentsia wakaibuka kumpinga kwa kigezo dhaifu cha "wrong approach."

Mihadarati haina mipaka ya kisiasa wala udini, ina dini yake, serikali yake, mfumo wake nk. Tukikalia kuongozwa kwa itikadi na mahaba niue tutaua kabisa hata hiki kidogo kilichianzishwa.

Kwa miaka 10 kiongozi aliishia kutamka tu kuwa majina ninayo, mwingine ndani ya mwaka amethubutu kuwabainisha washukiwa na kuutikisa mtandao, unadhani ipi ni hatua moja mbele?

Mwacheni RC atekeleze majukumu yake.

Mwenyezi Mungu akulinde katika nia yako njema mheshimiwa RC.

Long live your Excellency Makonda!!
"wrong approach" sio kigezo kidogo ktk spheres za kisheria.
 
Ndugu wana jf natumaini muwazima , mimi ninapenda kuongelea sakata la madawa ya kulevya .

Mimi naona hakuna binadamu asiyeeleweka kama mtanzania, mwanzo watu walikuwa wanapiga kelele sana kuhusu vijana kuharibika na madawa ya kulevya ambapo hakuna mtu alipenda ile hali nakumbuka wako wati walidai wanaohusika na madawa wakamatwe wanyongwe,

Cha kunishangaza amejitokeza mtu mmoja ameamua kupambana nalo mh Makonda lakini kila mtu anainua mdomo juu kwa kumlaani na kumpinga, hivi kuna mtu gani mwingine hata aliwahi kuthubutu au kujaribu?

jaman huyu jamaa anahitaji kusaidiwa sana mimi naona kwa ushauri ni kipi afanye lakini si kumlaumu hivi hadi kumtukana wakati kizazi chenye nguvu kinaangamia,

Hivi ni nani aliethubutu kujaribu kulifatilia au kulianzisha tangu watu wameangamia na madawa?

Mimi nawashangaa sana watanzania vile hamuelewekagi mnaweza kusema tunapenda ama tunataka hiki mkifanyiwa mnalalamika ,

Kuna mtu anaitwa Mange Kimambi alikuwa mstari wa kwanza kuwalalamikia hawa wauza dawa za kulevya akawa hadi anawataja lakini siku Makonda kaanza hii vita tayari kakurupuka na kumtukana matusi machafu ya nguoni, kweli huyu mwanamke na nyuma yake kuna misukule wengi kweli wanamsaport,

Jaman mimi naomba tumshauri Makonda nini cha kufanya na sio kumvunja moyo vita hii ni ngumu mno maana inahusisha wakubwa wengi sana,

Acha ajirandue tutawapata wahusika tu na watachukuliwa hatua na hilo tatizo litaisha kabisa lakini mkiendeleza midomo midomo wakati mnaona hayupo atayejituma kwa hili hakuna litakalofanyika.
Hahahah wakati wewe unafikiria kumsaidia katika vita hii mwenzako anawaza atanufaikaje na vita hii....jamani hebu tuache kufunika kombe mwanaharamu apite.... nani ambaye hakuwahi kujua maovu ya Home Shopping Center aka GSM ?? REally?.. tusijitoe ufahamu jamai. Muda tu kabla hata vita ya Makonda haijaanza tulishaelimishwa juu ya Home SHopping Center mpaka namna alivyokuwa akinyanyasa wafanyakazi wake.

Ila bado alimpa support RC na yeye akapokea akijua kabisa huyu mfadhili ana kashfa na bado akapokea.... msaada wa Said mtobolewa macho wa nyumba sijui nini alipokea,.... eiysheeee hebu Watanzania fungukeni macho... hesabu ya 1 na 1 inatushinda??
 
Moderators- kweli hii lugha ni kuvumilika? Nimerudia posting yangu mara kadhaa ili kuona ni kwa jinsi gani nimemsababisha huyu Nd Tiku ajibu kwa kejeli na matusi. Tafadhali mkemee lugha hizi - zinatuharibia ukumbi- Where we dare to talk openly- haina maana kutumia lugha isiyo ya ustaarabu!
Mkuu unafurahisha sana... Toka lini nzi wastaarabu...
Huyo aliyekujibu ni punguani fulani hivi wa kijani.
Hata kwenye mambo ya maana huleta mihemko.
Haina haja ya kulalama mpuuze tu, anaitumia buku 7 vizuri.
Yupo kazini.
 
Mtu aliyepata fa fa fa anawezaje kushinda vita anayopigana na waliofaulu?
 
Back
Top Bottom