Makonda hana jipya, amekuja tu kuvuruga CCM, Serikali na vyombo vya dola. Anapita tu!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
11,367
40,034
Siku chache sana baada ya Paul Makonda kuteuliwa kushika cheo cha Katibu mwenezi na itikadi wa CCM, cheche za siasa zake za toka zamani zimeanza kuonekana. Makonda ameanza kwa mikwara ya matamko ya vitisho, kebehi na amri za ajabu ajabu kwa watu mbali mbali na taasisi mbali mbali.

Kwa watu wanaoelewa siasa tayari wameshajua dhamira halisi ya Makonda na mwelekeo wa siasa zake.

Kwa haraka haraka, haya yako wazi;
1. Kuna watu au mtu mwenye mamlaka aliyempa Kiburi kikubwa Makonda na sio cheo ndio kinampa kiburi.

2. Upeo wa Makonda ni mdogo, haukui na haubadiliki (amedumaa kiupeo). Huo ndio mtaji wake, anaweza kutumiwa kwa lolote na yoyote.

3. Anakuja huku akiwa amejipanga kwa shari dhidi ya watu fulani fulani mahususi. (Ametumwa kwa kazi maalum)

Makonda anapita tu!


NOTE
Popote ulipo Kassim Majaliwa kaa vizuri kisiasa, hali huenda akawa ni tete sana, hii ngoma inakuja kuchezewa ulipo.
WAMEJIPANGA!
 
Hana jipya huyo Makonda ni mihemuko ya watu. Yeye atakuwa chawa namba moja wa kumsifu mama na CCM. Halafu Hana ubavu wa maamuzi.
 
Bwana usitusemee wanaCCM tuliowengi. Sisi hutuambii kitu kuhusu Makonda. Tunamkubali sana na kwetu ni Kiongozi mzuri sana.
 
Back
Top Bottom