Makonda atangaza vita na watumishi hewa mkoani Dar

SIMAMISHENI ULIPAJI MISHAHARA BANK KWA MUDA /
ILIPWE KATIKA VITENGO MAALUM CASH. MTU KABLA HAJACHUKUWA ATATAKIWA AJE NA FULL DOCS ZA AJIRA YAKE!
NA KITAMBULISHO CHAKE MUONE MADUDU MSHANGAE.

kama hamkupata watu 450-550
 
sijui kama mtu anaweza kuanzisha vita na watumishi hewa!!! yaaani sijui hiyo inawezekanaje kwasababu tayari ni watumishi hewa
 
Unfortunately, Magufuli ameaminishwa kuwa huyu Makonda ni mfanyakazi ili hali ni mtu wa kupenda sifa na mkurupukaji ambae ataharibu sifa ya utendaji ya Magufuli. Nitatoa mfano mmoja tu wa yule aliyekuwa mpurugenzi wa Kinondoni ambaye Makonda alimshitaki kwa ubadhilifu na kurudishwa kutoka Babati kuja kuhojiwa; ikagundulika kuwa Makonda kwa kutaka sifa alikurupuka na mashitaka ya kufikirika na yule bwana akaonekana hana hatia!!!! Magufuli should be careful na Makoda atamuingiza choo cha kike!!
Iweke hiyo habari hapa JF kuhusu yule mkurugenzi wa zamani wa Kinondoni.kwamba alisingiziwa Na yuko huru.
Nyie mbona mko wengi msio mtakia mema RC Makonda.
Mtasuburi sanaaaaa tu 7/24/365x5
 
Nasubiria Ombaomba na Machangudoa nao waishe Dar. Rahisi sana kuzungumza kuliko kutekeleza
 
Kama hewa inashitakiwa mahakamani kwel TZ tumepiga hatua....
kamata waidhinishaji wa watumishi hewa
 
Makonda, kuna standard 7 failures serikalini ambao wanatumia vyeti vya bandia na kushika madaraka serikalini huku wakiwa hawajuwi wakifanyacho na kuitia serikali hasara.
 
Sawa, jiji la Dar ni kioo. Wafanyakazi hewa wanachafua taswira ya jiji ila uchafu uliokithiri jijini; mitaro kuziba, takataka kila mahali, nk. hazichafui taswira ya jiji! Shughulikia pia swala la uchafu uliokithiri jiji la Dar tukuone kweli unafanya kazi!
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hajaridhishwa na idadi ya watumishi hewa aliyopatiwa na maofisa utumishi.

Mbali na hilo, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwahoji maofisa utumishi wote wa mkoa huo, kwani ndiyo wanaotoa taarifa zisizokuwa sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini wake jana, Makonda alisema haiwezekani Mkoa wa Dar es salaam ulio na wajanja wengi na matapeli kuwa na wafanyakazi hewa 71 tu.

“Baada ya Rais kutoa agizo la kutaka kila mkoa utaje idadi ya watumishi hewa, niliunda tume ya kufanya uchunguzi, lakini kwa uchunguzi wa awali nililetewa idadi ya watu 71 kwa kweli hii idadi sikubaliani nayo.

“Inaonekana kuna watu wanatengeneza habari ili wajiongezee kipato hali ambayo wanatoa takwimu zisizo sahihi, kwa kuligundua hili nimeamua kufanya uchunguzi upya na kila siku idadi inaongezeka,”alisema Makonda.

Alisema kutokana na udanganyifu wa takwimu zisizo sahihi, amewaagiza wakuu wa wilaya zote kuacha shughuli zao na badala yake wafuatilie idadi ya watumishi hewa kwa kila wilaya.

Alisema amefanya mazungumzo na ofisi ya utumishi wa umma ili kupata idadi kamili ya watumishi wa serikali walioko wilaya zote.

“Ofisi ya utumishi ndio ofisi inayojua idadi ya watumishi walioajiriwa, watatusaidia kujua ukweli baada ya hao wakuu wa wilaya kutoa taarifa za watumishi hewa ,”alisema Makonda.

Alisema katika hatua nyingine za kupambana na watumishi hewa, tumepata mfumo wa malipo unaotambulisha watumishi wote ambao wanapokea mishahara kutoka serikalini.

Alisema Wilaya ya Kinondoni tayari watu 34 wamechukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa jalada tangu Aprili 8 mwaka huu.

Alisema amepata taarifa ya kuwapo watumishi ambao wamejifutia madeni baada ya kusikia uchunguzi unafanyika.

Chanzo Mtanzania
 
weke hiyo habari hapa JF kuhusu yule mkurugenzi wa zamani wa Kinondoni.kwamba alisingiziwa Na yuko huru

Ninavyofahamu mimi engineer Natty yuko mtaani anadunda; kama wewe una taarifa tofauti toka kwa Makonda iweke hadharani!! Je Makonda amekwisha malizana na omba omba na machangudoa? Makonda lazima ajue kuwa hao hao waandishi wa habari anaofikiri wanampandisha chati ndio hao hao watakaomuangusha!! Kupanda upesi upesi hushuka haraka pia!
 
Makonda anaweza kuja kuwa kiongozi mzuri sana. Bado kijana na anaweza kufanya makosa ila haina maana ni mtu wa kupuuzwa. Wenye macho haambiwi tazama
 
Back
Top Bottom