Makonda ana maana ipi katika hii clip?

Alitaka kuwatosa wabaya wake (paka) wa Dar... Badala yake akajitosa yeye..!

My take: anajuta sana. Anawaza ni heri hata angekuwa mtoto labda angepata msamaha..
 
HABARI ZENU HUMU NDANI
Leo nimeamua kupitipitia instagram page ya RC wa Dsm.post yake ya mwisho ni video fupi ikimwonyesha dogo anataka kumtupa paka kwa bwawa la kuogelea lkn paka anachoropoka na dogo ndo anadumbukia....kwa wataalam wa kwenda beyond the reality nna uhakika kuna ujumbe anatufikishia sisi wakazi na watanzania kuhusu suala lake nyeti.
Hebu nnasidien na nyinyi mnaelewa vipi hapo

Ni rahisi kuweka video za kimajungu kuonyesha mtoto anacheza na paka lakini ni vigumu kuweka ata kipande cha cheti ili kukanusha upepo mbaya unaovuma hii ni aibu kwa jitu zima kama bashite.
 
John Mallya

Paul Makonda;
MNguzo ya bandia iliyomong'onyoka kama kipande cha mkate kilichotiwa kwenye kikombe cha chai.

'Mungu' wa Dar es Salaa alikikimbia kiti chake cha enzi.

Jemedari wa vita alieuwawa kwa risasi ya maji.

Kiongozi wa mapambano aliegeuka mwombolezaji wa machozi na makamasi.

Hadithi ya kisiasa ya Daudi Bashite imeanzia ujanani na kuishia ujanani. Ameukimbia mji aliokua akitishia kuwakimbiza wengine, ametorokea pasipojulikana! Ameondoka bila kusema kwaheri, jambo la mwisho alilolifanya ni kujaza machozi kwenye madhabau za masinagogi, kupiga magoti ya hatia akiwa ndani ya mavazi ya rangi za giza. Amezamia Afrika Kusini kule vijana wenzie ambao hawakusoma na hawana ajira wamekua wakizamia.
Mambo 3 ni dhairi na muhimu, ni somo kwa vijana.
1. Unapopewa madaraka ukiwa kijana, ni fursa ya kua taswira ya vijana ambao wanaota kushika madaraka ya kiuongozi, chukua muda kusoma mazingira ya kazi yako, jua maslai ya ofisi yako, tenda kwa haki, na kamwe usitafute utukufu binafsi.
2. Usikufuru Mwenyezi Mungu, usijifananishe nae, na zaidi usitukane wala kudhalilisha watumishi wake (wana wafuasi wao) ni waombaji wanaoongea na Mungu. Usionee watu kwa sababu za kisiasa au kwakua ni tishio la nafasi yako.
3. Usijipendekeze kwa mtu mmoja ukaacha watu wengine wote, usitukane au kudharau wasaidizi wako, jua historia ya taasisi ya unayoiongoza.
4. Hayo matatu hapo juu hayategemei kwamba una cheti cha shule au lah! Yanatokana na uelewa, akili na busara, ambavyo kwame havipimwi kwa cheti. Wapo chungumzima ambao hawana vyeti lakini wana uelewa, akili na busara, kama hata hivi vya bure navyo ulikosa basi hakuna anaeweza kukusaidia duniani, wala mbinguni.
Umebaki kuwa mtu unaempa mteuzi wako wakati mgumu kuliko watu wote nchini kwetu. Sio Mteuzi wako wala wasaidizi wake wenye jeuri ya kukutetea. Wamekuacha uwe kituko na panchi begi unaepigwa toka pande zote. Tusalimie huko ulipo.
Jambo lingine la muhimu na lakujifunza kwenye zama hizi ni nguvu ya mitandao ya kijamii, (social Media) mashambulizi ya Mange Kimambi kutoka Los Angels California yamemkimbiza Daudi Ilala, Dar es Salaam!!! It tells a lot.
Hizi ni zama nyingine
jhnmallya07
 
Kwa kuwa uwezo wake wa kufikri ni mdogo alikuwa anajifurahisha tu
 
Nimekuja mbio nikijua kaweka vyeti kumbe anaendeleza mipasho! Bashite weka vyeti.
 
Kwa kuwa uwezo wake wa kufikri ni mdogo alikuwa anajifurahisha tu
Kweli mkuu thinking capacity ya Makonda ni ndogo mno angekuwa January angalau ningejifikirisha lakini huyu hata sijisumbui ni kama picha za Tom and Jerry.
 
Mlisema ni fa fa fa fa yaani zero, sasa iweje mshindwe kupata maana halisi ya hiyo clip? Hapa tutajua yupi fa fa fa na yupi fu fu fu. Kuna nadharia moja inaitwa hemenitik inamsaidia mtu kupata maana ya clip na matini mbalimbali
 
Back
Top Bottom