Makonda Alienda Clouds Kufuatilia Documentary Yake ya Mwaka Mmoja Madarakani

Status
Not open for further replies.

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,142
Licha ya watu wengi kuzungumza mengi kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam 'kuvamia' ofisi za Clouds Media kwa lengo la kuwatisha vijana wachapakazi wanaopendwa mpaka na viongozi wa juu serikalini, Shilawadu (Qwisa na Soud Brown), inaelezwa kwamba mkuu huyo wa mkoa, hakwenda kwa shari.

Inaelezwa kwamba alikwenda kufuatilia utaratibu wa documentary yake ya mwaka mmoja madarakani, iliyofanyika pale Officers Mess, Oysterbay kwa sababu anataka irushwe kwenye kituo hicho, ili watu wengi zaidi waone matunda ya jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya na namna anavyoungwa mkono na waathirika wenyewe.
Clip inayosambaa, haioneshi popote kwamba mheshimiwa alitumia nguvu kuingia, na zaidi kuna mtu anaonekana mapokezi ambaye ndiye aliyekuwa akiwafungulia mlango wa ndani. Hakuna mtangazaji yeyote aliyepigwa na kulikuwa na mazungumzo ya kawaida tu ambayo hata hiyo, haifahamiki yaliishaje.
News Spinning...
 

Kwenda clouds..had aende na police?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…