Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,521
- 4,381
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametaka kufikishwa mahakamani haraka kwa watumishi wanaodaiwa kuhusika na upotevu wa shilingi Milioni 428 ambazo ni fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Makonda ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa watumishi wanaodaiwa kuhusika na upotevu wa fedha hizo wafikishwe mahakamani kwa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) tayari imekamilisha uchunguzi wake.
"Vyombo vimeridhika kwa uchunguzi uliofanyika mtu anaingiziwa shilingi Milioni 428 kwenye akaunti yake sio msambazaji wala sio mkandarasi waliomuingizia hizo fedha wanazunguka upande wa pili na kwenda kuzichukua wanagawana na kumuachia fedha katika akaunti yake kama kishika uchumba kwa kazi ya kuficha fedha za wananchi wa hali ya chini". amesema Makonda