Mwenge utafika zanzibar??
Hizi ni drama kweli kweli....![]()
Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano.
By Matern Kayera, Mwananchi Digital
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.
Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.
Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.
“Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”alisema Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali.
Alizitaja baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa ajira, uwezo mdogo wa kuajiri kwenye soko la ajira, ukosefu wa mitaji rafiki kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya vijana kwa kuchagua kazi.
Makamu wa Rais pia amewataadharisha vijana kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya. Amesema vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 ndiyo wanaongoza kwa kuathiriwa na maambukizi ya ukimwi. Amesema athari za ukimwi na madawa ya kulevya kwa vijana ni kubwa lakini pia zinaongeza mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa vifo.
Kwa upande wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amemtambulisha George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisaidiana na wakimbiza mwenge wengine watano. Alisema sherehe za kuhitimisha mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafanyika mkoani Simiyu tarehe 14 Oktoba mwaka huu.
Mwenge ni symbol muhimu sana KWA Taifa, wakati Mataifa mengine kama Rwanda wanaona Mwenge ni chombo cha kuondoa Matabaka ya kikabira, koo na Koo, walio nacho na wasio nacho, sisi tunaona Mwenge ni anasa au ni Upuuzi! Wenye mawazo kama ya kwako hawajui / hawaelewi umuhimu wa Chombo hicho.Sijui tufanye nini ili wajue kuwa wananchi hatutaki mbio za mwenge
Kunakuwa na vitendo vya uzinzi kupita kiasi hasa maeneo ambayo mwenge unalala, hebu tembelea maeneo ambayo mwenge umelala uoneMwenge ni symbol muhimu sana KWA Taifa, wakati Mataifa mengine kama Rwanda wanaona Mwenge ni chombo cha kuondoa Matabaka ya kikabira, koo na Koo, walio nacho na wasio nacho, sisi tunaona Mwenge ni anasa au ni Upuuzi! Wenye mawazo kama ya kwako hawajui / hawaelewi umuhimu wa Chombo hicho.
Any way sijajua wewe ni wa kizazi kipi, kizazi cha FB na Jamii Forum?
Uzinzi ni Tabia ya mtu lakini msisingizie Mwenge unamfundisha mtu umalaya...Kunakuwa na vitendo vya uzinzi kupita kiasi hasa maeneo ambayo mwenge unalala, hebu tembelea maeneo ambayo mwenge umelala uone
Hizi ni drama kweli kweli....
-Mwenge UNAMLIKA mafisadi au UNAMLIKIA mafisadi?
-Mwenge unaleta matumaini au unaondoa matumaini?
-Kuna haja gani ya kuendelea na mwenge kama dhima yake kuu ilikuwa kuondoa ufisadi na sasa ufisadi unaondolewa kwa kile kinachoitwa UTUMBUAJI?
(Hapo mbona kuna mkanganyiko?)
Kama dhima kuu ya mwenge ilikuwa kumlika mafisadi na wezi je hawakuweza kuonekana kwa huo mwanga wa nwenge?
Kama hawakuonekana je kuna haja gani ya kuendelea na kitu kisicho na uwezo wa kuofanya kazi iliyokusudiwa?
Kama uliweza kumlika je wako wapi waliomlikwa?
Kwa muda wote huo umemulika je kuna haja gani ya serikali kulalama juu ya mafusadi hadi kuunda sera nyingine ya MAJIPU ili hali kazi inafanywa na mwenge?
Je serikali haioni kwamba kuna tatizo mahala na hicho chombo chao??
Kama lengo la mwenge ni kuchochea maendeleo, Kwa nini hizo pesa za kugharamia uchochezi zisitumike kwenye MAENDELEO moja kwa moja??
Kama lengo ni kupambana na maambukizi ya VVU kwa nini hizo gharama zisitumike kusafirisha wataalamu kwa kutoa semina kwa vijana juu ya maambukizi?
Kama tatizo ni ajira na mitaji kwa vijana kwa nini hizo gharama za kutembeza mwenge zisitumike kutoa MIKOPO midogo midogo kwa vijana?
HAPO MI NAONA KUNA KITU KWENYE HUO MWENGE.....
WATANZANIA TUJITATHIMINI JE KWETU UNA FAIDA GANI!
Huu mwenge ndio ulionifanya kumnyima magufuri kura kwa kujua utaendelea tu nikiwa darasa la tatu nimesomea chini ya mti wa acacia tukikaa kwenye mawe kaptura zilichanika kila mara na darasa la sita kwenye jengo lisilo na paa kumbe watawala waliona mwenge nikipaumbele walimu walituchangisha hamsini hamsini na kutuamru kujipanga barabarani kuushangilia poor my TZ