A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na tabia ambayo imezidi kumea katika jamii yetu na nchi kwa ujumla kwa makampuni ya mikopo kutuma msg kwenye siku zetu wakitangaza huduma zao.
Idara za masoko za makampuni ya kukopesha yamekua yakituma msg kwa wananchi kujitangaza ili kuoata wateja.
Hofu yangu kubwa ni wapi wanapata namba zetu za simu mpaka inafikia wananitumia matangazo yao ya biashara.
Kwa mfano mie sijawai kuomba mkopo kutoka katika taasisi/makampuni ya kukopesha ila nimekua napata msg kwenye simu yangu mara kwa mara kuhusu aina za mkopo na package wanazotoa na mchakato mzima wa kuomba na kupata mkopo wao.
Naelewa kuitangaza kampuni na bidhaa yake ni jambo jema sana ili kupata wateja ila hofu yangu ni kwenye usalama wa faragha zetu wananchi.Najiuliza maswali mengi sana;
Moja wapi wanapata namba zetu za simu ili watutumie msg za matangazo?
Mbili wanabuni tu hzo namba kisha wanatuma msg au kuna taasisi ambazo wanavujisha na kuwapa namba makampuni/taasisi za mikopo
Tatu vipi usalama wa faragha zetu kama itakua ni kweli kuna watu wanawapatia hizi kampuni za mikopo namba zetu za simu.
Nafikiria ni wakati muafaka kwa serikali na taasisi kama TCRA na polisi kutoa miongozo na kusimamia usalama wa faragha za wananchi na ktoa adhabu kwa mtu/watu/kampuni au taasisi zinazotumia vibaya namba za watu bila ridhaa yao.
Kwanza hizi msg zinanirusha mtu nakua nawaza mambo yangu kisha inaingia msg isio na kichwa wala miguu.
Nimeambatanisha msg moja nikiyotumiwa na kampuni moja ya mikopo