LGE2024 Makada wa CCM wajitupa chini watoa shutuma kwa wanaokata majina katika kura za maoni Arusha

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,666
6,428
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Longdon kata ya Sokoni One Jijini Arusha, wamedai kuwa hawatashiriki uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa eneo hilo kutokana na aliyeongoza kupata kura za maoni 189 jina lake limekatwa na aliyepata kura 36 jina kurejeshwa kama mgombea kupitia chamba hicho.

Inaelezwa kuwa katika matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho ndugu Ibrahimu Mkurunzi ambaye alikuwa anatetea kiti chake amepata kura 189 na Jeradi Saitoti amepata kura 36.

Chanzo: Gadi TV
 
Afu bado mtu anaamini CCM itashindwa sikumoja au mtu aseme wameibiwa kura CCM kila kona wamejlpanga haaaa wechaliii tafuta nafasi ata ya ujumbe CCM ndio safari isiyoyumba. nikama yanga imeshindikana africa miaka 100 ijayo totoz za kiarusha CCM siami mm mama mitano tena.🖐
 
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Longdon kata ya Sokoni One Jijini Arusha, wamedai kuwa hawatashiriki uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa eneo hilo kutokana na aliyeongoza kupata kura za maoni 189 jina lake limekatwa na aliyepata kura 36 jina kurejeshwa kama mgombea kupitia chamba hicho.

Inaelezwa kuwa katika matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho ndugu Ibrahimu Mkurunzi ambaye alikuwa anatetea kiti chake amepata kura 189 na Jeradi Saitoti amepata kura 36.

Chanzo: Gadi TV
#HABARI Wanachama wa chama cha Mapinduzi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam wamendamana wakiwa na mabango katika ofisi za makao makuu ya chama kwa kile wanachodai kuwepo kwa wizi wa kura na rushwa katika uchaguzi wa kura za maoni.

Wanachama hao kutoka Chanika, Buguruni, Tandika, na Ukonga nje ya Ofisi za makao makuu ya chama Mkoa wamesema fujo zimekithiri sana katika uchaguzi kutokana na wagombea ambao muda wao umeshapita na kukosa ushawishi kutaka kurudi kwenye madaraka pamoja pamoja na rushwa iliyokithiri.

“Fujo zimekithiri sana kwa sababu ya wagombea walio tangulia walishakosa sifa za kurudi kwenye madaraka yao ambayo wao wameyang’ang’ania lakini kitu cha pili ni rushwa kwanzia ngazi ya tawi kata mpaka wilaya. Imefika wakati wagombea hawa wamepewa nguvu bila sababu za msingi” Amesema mwanachama wa CCM

Aidha itakumbukwa kwamba fujo hizo katika kura za maoni zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini ikiwepo Mkoani Manyara pamoja na Mkoani Kigoma
#EastAfricaTv
 
Back
Top Bottom