Majina ya miundo mbinu yanaweza kutangaza Utalii...

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
3,147
5,492
Pamoja na kwamba sina tatizo na majina yanayotolewa kwa huduma/miundo mbinu Nchini ILA napendekeza ile miundo mbinu yenye sura ya kimataifa ipewe majina ya kuwakilisha vivutio vyetu kama sehemu ya kutangaza Nchi
Nikisema sura ya kimataifa , naanisha miundo mbinu ambayo kwa kiasi kizuri itahudumia watu wa kimataifa
Naamini majina yatakuwa na faida sana kama yatautambulisha Mlima Kilimanjaro upo Tanzania kwa mfano, CHIMPANZEE wapo Mahale (Tanzania), nk nk

Zamani kabla sijasoma utalii wa Dunia nilifikiri sisi tu ndio tuna vivutio vizuri; kumbe Duniani kote ikiwemo Marekani wana mbuga za wanyama na kuna nchi zenye vivutio vizuri sana hivyo tunatakiwa kujitangaza zaidi kaka Mama alivyotuanzishia
 
Njia mojawapo ya kukuza utalii iwe ni kuondoa viza kwa watalii wasiozidi siku 14
Yani mtu apewe visa on arrival na hii iwe kutoka nchi yoyote duniani hata kule kwa kina penguin
Of course Ile royal tour ilikuwa matata sana
 
Back
Top Bottom