NAUNGA MKONO HOJA KIONGOZI,MIMI MWENYEWE NILISHAAPA KABLA KUWA HAKUNA MTOTO WANGU ATAITWA JINA LA KIGENI,NASHUKURU MUNGU NINA WATOTO WA3 NA WOTE WANA MAJINA YA KISWAHILI.Habari ya muda huu wanaJamii forums?.
Ni miongo kadhaa sasa nimekuwa nikifanya tafiti zangu binafsi juu ya baadhi ya Waafrika wengi (Zaidi ya 50%) hususan Watanzania Juu ya uelewa wa dhati juu ya TAFSIRI/MAANA NA ASILI YA MAJINA.Iwe ni Majina yetu binadamu na hata sehemu mbali-mbali katika Taifa letu na Bara lote kwa Ujumla.Leo nitajikita zaidi katika Majina yetu na siyo Majina ya sehemu mbali-mbali.
Tumeshindwa kuwa wazalendo kwa Makusudi kwa kuendekeza Falsafa ya Chochote cha mzungu ni bora kuliko chetu.Kuanzia aina ya Maisha tunayoyaishi,Imani,Tamaduni,Siasa nk.Ieleweke kuwa siyo kila kitu cha mzungu kinatufaa na pia baadhi yanatufaa kama watu wenye Fikra,Utashi na Maarifa sahihi juu ya adhma na hatima ya Maisha yetu.
Hoja ya msingi juu ya bandiko hili ni kusaili kila tukionacho,Tukisikiacho na hata tuyasomayo katika vyanzo mbali-mbali (Iwe magazeti,vitabu,Luninga nk).Ni lazima ukose utulivu wa Mawazo,Lazima uwe RESTLESS ili basi mwisho wa siku uweze kuchagua kitu bora kati ya vingi.Hivi ndivyo walivyofanya kina Ngugi wa Thiong'o,Chinua Achebe nk.
Hivi unajua kuwa Wayahudi wanatumia majina yao ya kiyahudi,Wajapan ya kijapan,Wakorea ya kikorea,Wahindi ya kihindi,Waarabu ya Kiarabu,Waingereza ya kingereza,Warusi ya kirusi nk?.Sisi Waafrika hususan Watanzania ndiyo tuna Kasumba ya kuazima Majina yao na kuwapa wenetu.Ni kwanini lakini?.Ni kirusi gani inayotuandama hadi kwenye mambo siriazi namna hii?.
Kuna wakati tunashindwa kutumia bongo zetu ipasavyo kwa kudhani kuwa Majina kama Muhammad,Rahma,Hassan nk ni majina ya kiislamu jambo ambalo siyo kweli.Haya ni majina ya Kiarabu na siyo ya Kiislamu.Kadhalika kwa Wakristo nao,wanadhani majina kama Albert,Grace,Francis nk ni majina ya kikristo kumbe siyo.Haya ni majina ya Waingereza na hayana uhusiano wowote na Ukristo.Huku Jamii Forums ndiyo usiseme,Wapo wenye majina ya ulaya wazi-wazi kama Copenhagen DN ,FaizaFoxy ,Evelyn Salt ,the american dream nk.Wapo baadhi wenye Majina ya Kiswahili na ya asili kama OLESAIDIMU ,kisu cha ngariba ,mshana jr ,MziziMkavu nk.Nawakubali sana.
Uislamu maana yake ni Usafi,Utii na Unyenyekeve mbele za Mungu.Hauna uhusiano wowote na Uarabu.Unaweza kuwa muislamu/Mkristo safi ukaitwa Saningo,Masanja,Macha,Msangi,Mwakaage,Mshana (Endelea).... nk na siyo kubandikwa majina ya kina Hamad,Ramadhani,Andrew,Joseph (Endelea).....nk ambayo hata tafsiri ya majina haya hatuifahamu.Tufahamu kuwa majina ya Kiarabu na yale ya Kikristo yalikuwepo miaka mingi kabla dini ya Uislamu na Ukristo haijaanza. Waarabu wametufanya tukadhani kuwa Uarabu ndio Uislamu.Kadhalika wazungu nao wametufanya tuamini kuwa Uzungu ndiyo Ukristo.Ndio unaona watu wanavaa kama Waarabu, wanatumia lugha yao, wanachukua majina yao, na hata wanataka kuongea kama wao wakidhani kuwa huo ndio Uislamu kumbe siyo.Ukristo siyo kuzungumza Kizungu wala Uislamu siyo kuzungumza Kiarabu.
Sote tuna ushahidi wa kutosha kuwa haya ni majina toka Ulaya na Yesu ambaye ndiye Wakristo wanamfuata hakutoka Ulaya wala Asia.Hakuwahi kufika Uingereza,Japan,Urusi nk,na wala hakuongea Kiingereza,Wala Kiarabu.Hakufika Ufaransa wala Italia.Alikuwa myahudi. Alizungumza lugha ya Aramaic na alienenda katika taratibu na tamaduni za kiyahudi.Kwanini sisi Waafrika tuyaige maisha yao?.
Waafrika tupo nyuma mno Kiuchumi,Kiteknolojia nk lakini tusiwe nyuma hata katika hili la kuuenzi utamaduni wetu.Huu ni umasikini wa fikra,Ni jambo hatari sana kwa Usalama wa Tamaduni zetu.Na ndiyo maana wapo Waarabu wengi wanaoishi Uarabuni ambao ni Wakristo na wanatumia majina ya tamaduni yao ya Kiarabu bila kujali kuwa ni Waarabu au Wakristo.
Wapo Wamarikani wengi wa Kaskazini wenye majina ya Kiswahili ambao nimewapenda mno kwa kuuenzi utamaduni wa Kitanzania.Kwa uchache tu ni kama wafuatao;
Talib Kweli (mwanamuziki wa Rap), Amiri Baraka (mwandishi, mwanaharakati, na mshairi), Haki Madhubuti (mshairi), Maulana Karenga (mwanzilishi wa sikukuu ya Wamarekani Weusi yenye jina la Kiswahili, Kwanzaa na Mkurugenzi wa Idara ya Masomo ya Waafrika katika Chuo Kikuu cha California, Berkley) na mke wake Tiamoyo Karenga, Maisha Ongoza, Mapinduzi Leo, Rafiki Mtumishi, Malaika Jabali (mcheza sinema), Fani Adili, Harambee Afrika, Ujamaa Muhammad, Akili Mali, Sheria Haki, Mtoto Wa Afrika, n.k.
USHAURI.
Tuachane na Utumwa Mamboleo.Tuuenzi utamaduni wetu kwa kuwapa Wenetu majina ya Asili yetu na Utanzania.Tuachane na majina ya Kiarabu,Kiyahudi na Kizungu.Tuchague majina yetu yenye tafasiri nzuri na Kuwapa wenetu.
Ruhuksa kunikosoa na Kunielimisha.Karibuni.
Hongera sana Mkuu Mbalamwezi1 .Upo very active.NAUNGA MKONO HOJA KIONGOZI,MIMI MWENYEWE NILISHAAPA KABLA KUWA HAKUNA MTOTO WANGU ATAITWA JINA LA KIGENI,NASHUKURU MUNGU NINA WATOTO WA3 NA WOTE WANA MAJINA YA KISWAHILI.
Naitwa Dahafrazeril ila tafsiri yake nimekwishaitoa katika post za mwanzoni kabisa.Okol ni jina la wapi vile?.Nawewe waitwa Nani Kumbe
Mpeane majina mazuri, haijalishi hilo jina la lugha, kabila au taifa gani mradi liwe zuri tu.
Hata yawe ya Kiasili, Kiarabu na Kiyuropa kama si mazuri hayafai binadam kuitwa.
Mfano mtu anaitwa M'boro kwa Kichagga lakini Kilugha ya Taifa ni tusi, kwa mtu mwenye heshima zake huwezi hata kumuita au mtu kwa Kiswahili anaitwa "Mume wangu", mleta mada utaweza kumuita mwanamme mwenzio "Mume wangu"?
Ugumu wa haya mambo uko wapi mama yangu Faiza?
Hakuna jambo la aibu na kusikitisha kama kuwa na jina ambalo mama yako, marafiki zako, majirani, babu na bibi, n.k. hawawezi kulitamka. Na sababu pekee inayokufanya uendelee kuvaa jina hilo ni imani kuwa jina hilo ni la "kikristo" au la "kiislamu" .Dunia nzima Waafrika ndio tunaongoza kwa kuazima majina toka Ulaya na Uarabuni. Wachina, Wahindi, Wayahudi, Waarabu, Wajapani, n.k. wanatumia yao...sisi ndio tunahaha huku na kule kuchukua majina ambayo hata kuyatamka hatuwezi. Joseph inatamkwa Josefu, George inakuwa Joji, Godson inakuwa Gudisoni...
Nadhani suala la kujiheshimu kwa kutumia majina yetu, tunayoweza kuyatamka, tunayojua maana yake sio msimamo mkali bali ni msimamo wa busara na heshima kwa utamaduni wako.
Jibu la swali uliloliuliza mwishoni ni "Hapana".