Kuna tetesi zinazoendelea chini kwa chini ndani ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa uchaguzi wa mwaka huu wataamua kuchagua wawakilishi wabunge na madiwani kutoka vyama vya upinzania baada ya kubaini kuwa wabunge wengi wa CCM wanashindwa kuwatetea kwenye mambo ya msingi kwa kuhofia kutoteuliwa na CCM kugombea uchaguzi wa mwaka huu.
Tetesi hizo zimeenea katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kagera, Geita na Kigoma ambapo wananchi wa hali ya chini wanalalamikia uwakilishi duni wa wabunge wa CCM katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwatuhumu kwa mambo mbalimbali ikiwemo kukubali kupitisha Sheria mbovu zinazowakandamiza, kushindwa kuwatetea kwenye mambo ya kilimo, madini, uvuvi huku sekta hizo zikiwa zinabeba uchumi wa kanda ya ziwa.
Vijiwe vingi vya Kahawa katika Jiji la Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Geita na Kagera mada hizi za uwakilishi mbovu wa wabunge zimekuwa zikijirudia mara kwa mara na kuapa kurudisha nguvu ya upinzani ya miaka ya 2010 ambapo majimbo mengi Kanda ya Ziwa yalikuwa upinzani.
Majimbo yaliyokuwa na wabunge wa upinzani ni pamoja na Nyamagana, Ilemela, Ukerewe, Bukoba Mjini, Bukombe, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Bunda, Serengeti, Maswa Mashariki, Maswa Magharibi, Meatu, Itilima.