Majibu ya Postmoterm yaonyesha kwamba Hayati Ali Kibao alipigwa sana na kumwagiwa Tindikali

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, amesema kwamba baada ya Uchunguzi wa Mwili wa Marehemu ulioshuhudiwa na Ndugu wa Marehemu pamoja na viongozi wa Chadema, Imebainika kwamba Ally Kibao ameuawa.

Zaidi ni kwamba amepigwa kupita kiasi na Pia alimwagiwa Tindikali ili aungue kabisa asitambulike.

Kwa maana hii sasa ni dhahiri kwamba kifo cha kinyama cha Mzee huyu SI KAZI YA MUNGU, Ni njama za watu waliotumwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipokee Roho yake, Amina.
Uko wapi utu wetu?
 
Mungu ingilia kati
Bwana teta na wauaji
Mungu ameshindwa kuteta na Israel waache kuua watoto na wanawake Wa kipalestina wasiyo na hatia yoyote ndo aje aingilie kati kwa kuteta na Hawa wauaji huku Tanzania? Wakati fulani tutumie akili, maarifa na uwezo aliotupa huyo Mungu kumaliza matatizo yetu. Pengine Mungu ana kazi nyingi za kufanya na yuko bize mno. Watu watachinjwa km Kuku kwa kumsubiri Mungu aingilie Kati.
 
Hivi unatoka kuua mtu kinyama namna hiyo harafu unarudi nyumbani unasema umetoka kazini na wanao wanakula chakula kwa pesa uliyoipata kwa kudhurumu uhai wa mtu 😭😭😭.Dah!?!?#%@%@@
Watoto wote wanasoma Ulaya, baada ya kazi mamilioni wanaenda kujiliwaza Dubai au South Africa wanakula bata la kufa mtu.

Mkuu Dunia hii ina starehe nyingi na kali mno.
 
Back
Top Bottom