Majibu na kauli za mke wangu yamenichosha

namba moja tuu

Senior Member
May 4, 2017
162
142
kauli zake
"nimechochola kuzaa na wewe"
"nimebugi kuzaa na wewe"
"najuta kuzaa na wewe" pia mwezi wa uliopita alisema hata nikimuacha nisije nikamsumbua kuhusu mtoto"naomba umsahau mpaka mtoto" hii ni kauli yake tena sasa nimechukua jukumu la kuachana nae kilichotokea sasa!!!!ananiomba msamaha mpaka analia NIFANYAJE sasa
 
kauli zake
"nimechochola kuzaa na wewe"
"nimebugi kuzaa na wewe"
"najuta kuzaa na wewe" pia mwezi wa uliopita alisema hata nikimuacha nisije nikamsumbua kuhusu mtoto"naomba umsahau mpaka mtoto" hii ni kauli yake tena sasa nimechukua jukumu la kuachana nae kilichotokea sasa!!!!ananiomba msamaha mpaka analia NIFANYAJE sasa
Ndio zao wakishakuwa ndani ya ndoa huwa wanasahau kuwa kuna kuachika,so sad..
 
Uli jishusha sana kwa uyo mwanamke ndiyo maana akakuzarau. Rudiana nae ila kua makini hesabu maneno take.
nilikua nampenda sana na kuhusu kutamka kuniacha ametamka mara nyingi sana ila mara zote nilikua naomba msamaha sasa naona dah enough
 
Namba moja kwann unagombana na mkeo hadi anakwambia maneno mabaya hayo aisee, usigombane na mkeo. Kumbuka kati ya watu Bilioni 7 na ushee duniani ni yeye ndio ulimchagua awe mkeo please usigombane nae. Mpende na kumjali mkeo atakuheshimu no matter what.
 
Ndugu, kwa mkeo inaweza kuwa moja kati ya haya ni sahihi;
1. Hasira na mdomo mrefu
2. Pushing you to the limits to see the other side of you.
3. Dhamira yake ya dhati kabisa kukuweka pembeni, anataka ujiongeze apate sababu.

Hakuna hata moja kati ya hayo hapo juu litakuwa limetokea kwa bahati mbaya na halihitaji kuombea msamaha, ni mipango.
 
Nami nimejitahidi kuwa namba moja tuu katika kuchangia hapa. Si vinginevyo. Lakini, lazima kutakuwa na jambo linalomkera. Jitafakari na kujitathmini vyema Mkuu


"Mara nyingi mwanamke ni mwaminifu kwa kiwango kikubwa na kushikamana na familia yake. Hata hivyo, kuna sababu kadhaa wa kadhaa ambazo humsukuma kufanya usaliti.

Aidha, mara nyingi mwanamke hufanya usaliti kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake ya ndoa. baadhi ya sababu ambazo humfanya mwanamke kufanya usaliti ni kutomjali na kutomheshimu.

Licha ya kwamba kuna sababu kadhaa za hatua yake hiyo, lakini hii ni miongoni mwa sababu kubwa.

Mwanamke anapoona kwamba hana nafasi nyingine isipokuwa ulezi au upangiliaji wa nyumba, anaweza kwenda kwa mwanaume mwingine anayemjali na kumpa uzingativu.

SABABU nyengine "Anapohisi upweke na kupuuzwa na mume"

Mwanamke anapotumia muda wake mwingi akiwa peke yake nyumbani huku mumewe akimpuuza na kutompa muda wake mwingi, hujikuta kwamba maisha yake yakikosa maana. Hapo anaweza kufikiria kuwa na mwanaume ambaye anaziba pengo hilo.

Wanaume tunatakiwa kuhakikisha kuwa KIPAUMBELE NAMBA MOJA ni wake zetu, Mwenza wako anatakiwa kuwa namba moja katika maisha yako ya kifamilia. kuwa serious usifanye mchezomchezo kwenye familia yako. Wajibika kwa familia yako kwanza kabla ya kuwajibika kwa wengine." By somebody!

Ingawa mleta uzi hajasema sababu ni nini haswa, ila kuna sababu tena yawezekana yeye ndo chanzo, mida mingine ktk mahusiano jinsi anavyo behave mwanamke ni reflection ya tabia ya mwanaume! Ni kama taswira ya matendo ya mwanaume!
 
nifanyaje sasa misamaha naomba kila siku kua asiniache halafu tumezaa mtoto mmoja tu ila yeye amezidisha kuniambia ananiacha sasa bora nijiache mapema mwenyewe au ntakua nipo wrong mkuu
Of course, you will be right as it will be your own decision. However, try to solve your misunderstandings amicably.
 
Muulize ni kwanini ajute kuzaa na wewe? Kama kunamakosa na wewe badilika
anajuta kisa mimi kua ni malaya ila kwa maneno ya kuambiwa na watu ila sio kujionea mwenyewe na mtu anae mwambia hayo alikuaga x girlfriend kabla yake ila kwa sasa sipo nae huyo x
 
Back
Top Bottom