Maisha yanaenda kasi sana leo Sport Extra ya clouds ni kama enzi za RTD

Mukuu123

JF-Expert Member
May 7, 2019
319
1,223
Kwa kweli Wasafi na EFM wameleta mapinduzi makubwa sana kwenye vipindi vya michezo kuanzia kwenye kuhabarisha na kuchambua.

Yaani ukikaa juu sana jua unakaribia kudondoka hii nimeiona Kwa hawa CMG, kwanza siyo kila habari ni ya kuhabarisha yani leo hii clouds mnaanza ku report sijui league na uchaguzi wa viongozi wa mikoa kama katavi halafu mnategemea nisi switch efm na wasafi kwenye habari zinazo make headline na uchambuzi wa kiufundi.

Kwaherini mawinguni nimehamia EFM na Wasafi
 
Ushawishi wa kusikiliza radio umepungua sana kwa jamii ya sasa wanahabari wanaofanya updates za habari mitandaoni wanatengeneza hela sana

Millardayo amekua brand kubwa sana inawezekana anafatiliwa sana kuliko clouds ambae ndo waajiri wake
 
Kwa kweli Wasafi na EFM wameleta mapinduzi makubwa sana kwenye vipindi vya michezo kuanzia kwenye kuhabarisha na kuchambua.

Yaani ukikaa juu sana jua unakaribia kudondoka hii nimeiona Kwa hawa CMG, kwanza siyo kila habari ni ya kuhabarisha yani leo hii clouds mnaanza ku report sijui league na uchaguzi wa viongozi wa mikoa kama katavi halafu mnategemea nisi switch efm na wasafi kwenye habari zinazo make headline na uchambuzi wa kiufundi.

Kwaherini mawinguni nimehamia EFM na Wasafi
Tunatofautiana huku chuga ikifika saa tatu uck show ya michezo ndio inasikilizwa mawingu fm Kona zote
 
Tatizo lenu watanzania wengi mnapenda mda wote ziongelewe tu timu zenu kulwa na doto,sasa unataka mambo na mada nyingine zakimichezo zikazungumziwe kwenye kipindi cha mahaba au siasa? Habari zote za ndondi,mpira wa pete,riadha,kuogelea,pooltable,bao n.k zinatakiwa ziende kwa hewa kupita kipindi cha michezo sio kila siku mpira tu!
 
Kipindi kikubwa cha michezo Tanzania muda huo wa saa tatu kamili radio nyingine wameukimbia wanajua Sports Extra ni dude linabeba michezo yote ,na habari za michezo ,zikiwemo siasa za michezo
 
Redio zote zina angle yake ambayo ni mboni ya kuvuta walaji au wasikilizaji. Ila wasafi fm,efm na Ufm wameleta mapumduzi makubwa mno dhidi ya clouds fm. Mfano wasafi fm na Ufm muda wote utasilikiliza mpira kasoro wasafi ukitaka siasa za mpira na mengine Wana Kona ya kudere. Hii ni tofauti na efm wao huchanganya vyote na wanakosea sehem moja tu unaweza kushtuka mpira hauongelewi kwa asilimia kubwa na kuegamia zaidi kuongelea siasa za mpira. Clouds wako vzuri ila matangazo aisee! Hata kama unampa value mteja ila Sasa ndo iwe kila saaa aisee! Wabadilike kidogo
 
Back
Top Bottom