Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,182
- 5,553
Mahakama Kuu ya Tanzania leo September 09,2024 imesema kuwa waleta maombi kwenye shauri ambalo walikuwa wanaomba idhini ya Mahakama wana haki ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Sheria ndogo zilizotungwa kwa lengo la uratibu na uendeshaji wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Bob Wangwe, Bubelwa Kaiza na Annanilea Nkya.
Katika shauri hilo waleta maombi hao walipeleka maombi mahakamani dhidi Waziri wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiiomba Mahakama kibali cha kuweza kufungua kesi kuhoji uhalali huo ambao umetoa nafasi kwa Wazara hiyo kuratibu uchaguzi huo.
Akisoma uamuzi huo Mh. Jaji Wilfred Ndyansobera amesema waleta maombi wameweza kuthibitisha maombi waliyowasilisha na wana maslahi katika kesi ya msingi
Waleta maombi walidai kuwa uhalali huo unapoka mamlaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha akizungumza mara baada uamuzi huo Wakili wa upande wa waleta maombi, Wakili Jebra Kambole amesema kuwa baada ya uamuzi wa Mahakama ndani ya siku 14 watafungua kesi ya msingi kupinga uhalali wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na kuomba zuio la Mahakama kwenye michakato ya uchaguzi huo inayoendelea.
Lakini kwa upande wajibu maombi Wakili wa Serikali,Deodatus Nyoni amesema kuwa wamepokea uamuzi wa Mahakama lakini amesisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa haujasimamishwa na amesema kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha Wananchi kushiriki uchaguzi huo huku akisema kuwa wapo tayari endapo itafunguliwa kesi ya msingi.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Kitendo cha Mahakama kwenda kutoa hukumu ya TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuzidi kubariki uovu wa CCM
- Kuelekea 2025 - Bob Wangwe aiomba Mahakama Kuu iizuie TAMISEMI kusimamia shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa