Mahakama ya rufaa Tanzania, acheni kuchezea maisha ya watu tumechoka na siasa zenu

Mzee wa giningi pole lakin mkuu jipe subira kupigiwa sim sio vibaya ndio maana nadhan mliweka no zenu za simu! Kuhusu kuilaumu taasisi sio vyema! kuwa nasubira tu hata sis tulioko sekta zisizo rasmi tunachangamoto lukuki ila mwanaume kamili haupaswi kulia mitandaoni look other altenative! Ikitokea u can go!
Asante mkuu but serikali hii haina huruma hata kidogo
 
Mkuu Mzee wa Giningi, kwanza pole!. Pili kama uliajiriwa, naamini uliajiriwa kwa barua, na kama ulisimamishwa pia ulisimamishwa kwa barua kupisha uhakiki. Katika barua ya kusimamishwa, hakuna time frame ya uhakiki utaisha lini, na hizo simu za mara kwa mara unazopigiwa ndio kuhakikiwa kwenyewe!, tena wewe ushukuru angalau unapigiwa simu, hiyo ni dalili tosha bado unahitajika, subiria tuu barua yako ya kuitwa kazini mara baada ya kukamilika zoezi la uhakiki.

Nakushauri kama unataka kuwa na future na ajira za serikali, kitu cha kwanza ni kujifunza heshima, adabu, utii na nidhamu!, usidhani kujificha kwenye chaka la majina bandia ya jf, kama Mzee wa Giningi ndio kinga ya kutoa kashfa kwa mwajiri unayembembeleza kukuajiri halafu unamuita hivi!.

Kwenye mambo ya ajira, haihitajiki huruma kabisa, hapa vinazungumza vyetu tuu, huruma ni hospitalini kwa wagonjwa, wenye majanga na misibani, na sio kwenye ajira!.

Hatutaki kabisa waajiriwa wa utumishi wa umma wanaotaka kuonewa huru, tunataka waajiriwa wanaostahili.

Paskali
Tumia akili mkuu angalau
 
  • Thanks
Reactions: SDG
JPM aliahidi mambo mengi sana,na alisema hii nchi ni tajiri sana na anaijua serikali kwasababu yuko humo zaidi ya miaka ishirini,lakini ninauhakika katika awamu hii,watu watateseka kuliko awamu yoyote ile,ajira za uhakika hazitakuwepo,mapato yatashuka na mambo mengine mengi kama kuingia kwenye migogoro yakimataifa pasipokua na busara wala hekima katika ushughulikiaji wa mambo mbalimbali.Hivi sasa hana hata mpango wakureplace ajira zilizokua feki,na alitoa maneno yenye faraja nakujisifu kua yeye sio mwanasiasa hivyo atatekeleza yale anayoyasema.Ndugu yangu siasa zunachanganya sana nchi hii,endelea kisubiri huku ukifanya mambo mengine mbadala.
Umeongea kweli serikali hii ya ajabu sana sijawahi ona
 
UHAKIKI umeweka kama kinga ya ktoktoa AJIRA mpya, ktopandsha madaraja, ktotoa uhamisho, kutokuongeza mshahara,

Ila lengo kubwa ni kupunguza watumishi nasio kuajiri, hapa bado report ya 2 ya serikali kuu! Kwa nn hawaktoa siku 1 wakati UHAKIKI ulianza pamoja? Hapa ni changalamacho na kuwaona watanzania mazezeta!

Toka UHAKIKI uanze hakna jpya utumishi zaid ya matamko tu, haya sasa wamesema walimu sanaa wamesema hawaajiri bado wapo wa ziada je course zake wamefuta vyuoni?

Kuna haja gani kukopesha watu mikopo na wasomee taaluma ya ualimu wa sanaa angali hakna ajira zao au uhtaj wao? Wajinga watasema wajiajili hiv taaluma ya ualimu utalinganisha na Biashara?

Mifumo yetu mibovu sana HVO ktokuajiri sio kigezo cha kutatua changamoto hiz, hafu wakija kuwaomba kura wanawadanganya tena watatoa AJIRA mkiwapa kura wanaenda kukalia UHAKIKI mwaka mzma!

Polen sana mliobado na imani na awamu hii ya hovyo, inafanyia kazi matukio, TUKIO LIFUATALO NI RIPORT YA 2 YA VYETI FAKE NA MAKONTENA MCHANGA PART 2, baada ya hapo UHAKIKI wa umri na vyeti vya ndoa!
Watu mbona op
Tumia akili mkuu angalau
Ili mtu atumie akili, jambo la kwanza ni lazima kwanza hiyo akili yenyewe iwepo ndipo itumike!. Mtu anayetakiwa kutumia akili ni mtu mwenye akili ambae hajaitumia, lakini kama akili yenyewe haipo, atatumia nini?.

Paskali
 
  • Thanks
Reactions: SDG
About AJIRA hamjaona ?
Ajira hamna jamani,kuna TEUZI tu
 
Watu mbona op

Ili mtu atumie akili, jambo la kwanza ni lazima kwanza hiyo akili yenyewe iwepo ndipo itumike!. Mtu anayetakiwa kutumia akili ni mtu mwenye akili ambae hajaitumia, lakini kama akili yenyewe haipo, atatumia nini?.

Paskali
Kaka yangu Mayalla achana nao hao mm ninaomba unijaalie kirefu cha kifupisho OC.
 
Jambo ukilijua halita kusumbua kabisa, kama hakuna time frame ya uhakiki, unapata wapi justification ya kuwapangia muda?.

Mimi niliwahi kuwa mtumishi wa umma, hivyo hata ukifuatilia tuu bunge la bajeti, wenye akili watakuwa tayari, wameishajua nini kinachoendelea!. Kama kuna vizara zimepatiwa OC less than 20% na hii ndio last quarter, then automatikally utaelewa kwa nini uhakiki unachukua muda mrefu hivi kukamilika, kama hata OC tuu hakuna, hizo fedha za kuwalipa hao waajiriwa wapya, zitatoka wapi?. Endeleeni kusubiri tuu.

Paskali
Mkuu Paschal waeleweshe watu kuwa serikali haina fedha za kuwalipa watumishi, ndiyo maana wameamua kufukuza/kupunguza kwanza watumishi, hakuna namna.
 
Tume ya Utumishi wa Mahakama iliajiri watanzania 300 mwaka Jana 2016 baada Ya kuwasainisha mikataba na kuwapa pesa za kujikimu iliwasimamisha kazi na kuwaahidi kuwa baada ya uhakiki itawarudisha kazini Leo hii watanzania Hawa wenzetu wapo nyumbani cha kushangaza zaidi toka mwezi wa pili mwaka huu wamekuwa wakiwapigia simu na kuwauliza maswali Yale Yale .

Hii ni Mara ya pili wamekuwa wakipiga simu kuwauliza maswali Yale yale bila kuwarudisha kazini, ukweli mnachofanya ni kitu cha ajabu Sana kwanini msipangilie mambo yenu ndoo muwaite watu moja kwa moja kazini huu ni uzembe

Mnawapigia watu simu na kuwaambia mambo Yale Yale je? Mahakama ya rufaa mnalijua hili la kuwatesa watanzania Bila kosa???
Ukose tu hiyo kazi itangazwe upya maana wewe ni kilaza. Umeanza vizuri kutaja TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA halafu unalaumu MAHAKAMA YA RUFAA!! Lini mahakama ya rufaa ilihusika na huo mchakato!?
 
Back
Top Bottom