Mahakama ya Kisutu yawanyima dhamana Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare

Hao kuendelea kuwalaza rumande pia ni matumizi mabaya ya majengo ya serikali....hao wangenyongwa tu au wangepigwa risasi hadharani.....
 
Safi sana lazima mafisadi wote wakione cha moto, hii ndio serikali ya Magufuli, bado fisadi papa wa richmond.
 
zito alisha wahi kusema haya
"Kila mara ninapokaa na Harry Kitilya naona namna ambavyo baadhi ya Watanzania wana moyo wa dhati wa kufanya kazi na kuweka 'legacy' ya kudumu. Wakati Watanzania fulani wanamzodoa, kuna nchi kama Ethiopia zinamwomba kwa kumpigia magoti aende kuongoza Mamlaka yao ya Mapato. Changamoto moja kubwa, TRA inakusanya, matumizi ya fedha hayaonekani kwa wananchi kwani nyingi zinaishia kulipa posho, safari na matumizi ya hovyo. Laiti kama watumiaji wangekuwa na moyo wa dhati kama mkusanyaji Kitilya, tungepiga hatua kubwa sana"
Kumbe naye alikuwa anatetea ufisadi
 
Wengi tunachangia huku tukiwa tumejawa na wivu wa kimasikini!!!!.


Pole yao watuhumiwa wote, hilo kosa la kutakatisha fedha halina dhamana. Mungu awatangulie katika safari yenu ya kupambania haki yenu ya msingi.
Wivu au uchungu? Sisi wengine tunalipa kodi wengine wanachezea, wache wakale ugali wa bure.
 
Tuachie mahakama ipi wakati wewe mwenyewe umeshatoa hukumu mtoa mada kuwa Ni mafisadi lazima yafungwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…