Magufuli ataligharimu taifa, wengi wanafurahia pasipo kujua athari mbeleni

Mfumo wa uongozi aliouweka Rais
Magufuli awamu hii ndio utakaoliingiza taaifa hili pabaya. Magu amejitahid na amefanikiwa kuweka mfumo wa watu kuwaona wote wanao-challenge mawazo yake ni wezi, wapiga deal, mafisadi, wala rushwa au wamepewa chochote kile wamkosoe. Huu utaratibu ni mbaya na naona taratibu unaanza kulitafuna taifa. Ss hv ukiongea tofaut na mawazo ya Rais au Serikali yako basi ww utaonekana ni moja ya watu hao niliowataja hapo juu. Kuna vitu vingi tu ss hv Mh. Rais anachemka lkn watu (wataalam) wanapiga kimya kwa kuogopa kuonekana hawaitakii mema nchi hii au wamepewa hela (wamehongwa). Hii ni mbaya sana kwa taifa. Ku-challenge (kuhoji) maamuz au mawazo ya Rais (au Seikali) sio usaliti kwa nchi, ni njia nzuri ya kufanikisha mambo yaende, hatuwez kufanana mawazo au mitazamo naukiona mnafanana kwny kila jambo basi ujue anguko lenu limekaribia.

Kwny taarifa ya jana kuna vitu vimepotoshwa /vimekuzwa lkn watu hawawez kuviongelea kwa kuogopa km nlvyosema hapo juu. Mkulu anaposema kwa makontena yale 277 serikali ilkuwa inapoteza mapato kati ya Bil 676 na Trilion 1.147 ya dhahabu sio sahihi. Hizi ni true value (thamani halisi) ya dhahabu iliyopo kwny makontena ambayo ikiuzwa, serikali kupitia TRA itachukua kodi/tozo/mrahaba wa 4% kwa sheria ya ss hv. Kwahiyo hiyo hela yote sio ya kwetu, sisi tuna % tu ya hela hiyo iliyotajwa. Tatizo lililopo ni kuwa kulingana na taarifa ya tume, thamani halisi ya dhahabu ni ndogo kuliko iliyotajwa hapo mwanzoni. Sasa hili tumelikuza na kuwaaminisha wanatanzia tumeibiwa kati ya Bil276 na Trilion 1.147 wakati si kweli chetu pale ni 4% ya true value (Bil 676 to Tril 1.147)
Ni km kwny biashara zingine tu za uzalishaji, utazalisha soda utauza zile soda, baada ya mauzo halisi ya soda zile kwa thamani sahihi ya soda, ile hela iliyopatikana (gross revenue) itapigwa % kadhaa kama kodi/tozo na mzalishaji atabaki na chake baada ya kodi/tozo (net revenue). Sasa jana tumeaminishwa ile gross revenue baada ya kuuza zile dhahabu ni yetu yoteee. Hili tulikosea jana na kuleta tahaaruk kubwa ya kuonuesha kuwa tunaibiwa sana. Ni kweli tunaibiwa lkn tuepuke kukuza mambo.

Haya yote aliyoongelea Maguful hayajaanza leo kuongelewa, yamesemwa muda mrefu tu. Tatizo kubwa ni la mikataba mibovu tuliyokishau kuingia, hii ndio itatupeleka kwenye matatizo. Hatuwez kunufaika kwa kumfuka Prof Mhongo, ndio ana mapungufu yake meng tu, lkn yy sio source ya matatizo ya madini tuliyonayo. Kwa hli alilolifanya mkulu, we will feel the pain in the future, wenye migodi wamewekeza hela nyng sana and they are very smart to make sure they follow the state's (world) rules. Hawawez kuona hisa zao zinaporomoka hv na wasichukue hatua. Km tunavyoona ss hv tuna suffer kwa maamuz mabaya ya Mkapa, vivyo hivyo awamu zijazo tutasuffer kwa maamuzi haya mabaya ya Magufuli

Kwa ujinga tuendelee kuumia mpaka mwisho wa dunia au toa mbadala kifanyike nini
 
Mikataba kuhusu madini and it's related iwe ya uwazi na ijadiliwe bungeni pia walipinga uteuzi wa muhongo kuwa waziri na nyinyi CCM mkapinga

mkuu wewe mgeni humu, na ukitaka usiaibikwe uwe na free mind, usiwe inclined upande huu au ule

kutetea, ku support au kupinga kitu hakukufanyi kuwa wa chama hiki au kile

kwa hapo tu nishakudharau, una akili za kitoto
 
Uzi wako wa Kitoto Sana Jamii Forums Moderators watautoa Soon.

Usinichukie.
Kwa nini nikuchukie, sina sababu ingawa umetumia derogatory language, let me spare you at least for now!
Chuki yako na Lisu haiondoi facts alizozisema. Watu, wenyeji, kuvamia mgodi tu wanaenda arbitration, ! ona hatua walizochukua! sembuse hii ya mali iko njiani
 
Hakuna maendeleo bila sacrifice na uchungu. Wengine tulishauona uchungu toka anaingia lakini ana nia njema na taifa. Kikwete alikuwa ameachia fedha lakini miundombinu na hazina,madeni ya taifa yanazidi.
 
MKWEPA KODI , sina uhusiano wwt na ACACIA, wala hata hawanijui.
Hili la kuona mtu mwingine mwenye mawazo tofauti na mawazo ya watu wengine katumwa, kahongwa, msaliti, mwiz, fisadi, litatupeleka pabaya. Lazima tutofautiane katika hoja ili tuweze kupata mawazo yaliyo sahihi zaidi. Katika hili, Mh amekosea kudeal nalo.
kweli mkuu kumbe pesa yetu ni 4% tu
 
Very true ukianika ukweli hivyo watakuita unapinga Mara ww chadema Mara nyumbu ila time will tel.hawa watu wanafuata mikataba tuliowekeana nao.mm pamoja na kumshukuru mh.rais kwa barua zake nadhani angeanza kujiondoa kwenye hiyo mikataba mibovu na pia mikataba yote ya serikali iwekwe wazi ili tuweze kucriticise ili nao waweze kuincoperate some changes
Huyo mikataba sii Ilipitia baraza la mawaziri
 
maslahi ya taifa kwanza ubinafsi hauna nafasi!!

heri ya lawama kuliko kunyonywa rasilimali zetu!!
 
Ulipewa thamani ya madini yaliyokuwemo na so hela tunayostahili.Sisi tunanufaika kupitia mrabaha na corporate tax.Watu wenye uelewa km wako ndo wanpotosha.
Licha ya thamani kamati haikuainisha garama za kuprocess kupata hayo madini
 
mkuu wewe mgeni humu, na ukitaka usiaibikwe uwe na free mind, usiwe inclined upande huu au ule

kutetea, ku support au kupinga kitu hakukufanyi kuwa wa chama hiki au kile

kwa hapo tu nishakudharau, una akili za kitoto
Mkuu ukinidharau usiponidharau kwangu hakipungui kitu nimekwambia kile kilichopo nafikir umenielewa na hizo kusema mtu ana akili za kitoto ndio silaha yenu mtu akipingana na nyinyi nimemaliza
 
Back
Top Bottom