Magufuli amekosa exposure

Wewe mleta mada ni pumbavu sana. Eti umefika Manhattan 2002 ukajiona umemaliza kabisa. Watu wameanza kufika huko USA na Europe early 60s, 70s,80s wakafanya kilichowapeleka na kurudi kujenga nchi Tanzania. Vijana Kama wewe mlioenda Marekani kwa Scout na Camp Mna matatizo sana. Status yako ikoje hapo ulipo!!?? Ulipofiwa uliweza kurudi Bongo!? Acha ulimbukeni kijana. Mh Rais haihitaji exposure kwa kuja Manhattan au Chicago...After all sisi Watanzania tunahitaji Maendeleo na huduma bora za Afya na Jamii kwa kila Mtanzania. Hayo mambo ya Exposure peleka Big Brother au kwenu Mpitimbi. Bado unatongoza visichana vya Chuo Facebook kwa kutumia Exposure ya kufika manhattan mwaka 2002!!!!???? Ama kweli Ushamba mzigo!!!
 
Mwacheni baba wa watu awatumikie waTanzania kama alivyowaomba!

Exposure........exposure my foot! Kikwete aliyekuwa na exposure ya Foreign for Ten years..ametufanyia nini? Zaidi ya kufanya nchi yetu ikawa shamba la bibi? To be honest......I see Magufuli as the Right man for the job!
 
Kuna mambo fulani kama unayakosa, inabidi ukubali tu kuwa huwezi na umuite mwingine mfanye kazi pamoja kwa manufaa ya wote. Sisi tuna rasilimali lakini hatuna teknolojia, so hatuwezi kukomalia tu kwamba wageni wanatunyonya. Mfano, tungewezaje kujua kama tuna gesi ya kumwaga nchini mwetu kama tusingeingia makubaliano ya uwekezaji na watafiti kutoka nje ya nchi? Wao wanayo teknolojia ya kujua wapi pana gesi, wapi pana uranium, wapi pana mafuta etc. So lazima tushirikiane nao, tuwaite waje kuwekeza katika tafiti na uvunaji, then tuingie mikataba iliyo wazi yenye kutunufaisha wananchi wengi. Lakini kama tukisema kila kitu tunaweza (wakati sio kweli), watoto wetu kukosa huduma bora za afya, maji na elimu wakati tunazo rasilimali za kugharamia hayo yote
Aende Botswana kuna Rais wao aliyepita Quett Masire yule aliwakomalia wazungu ,50/50 kwenye diamond na hawalimi wala hawavuni diamond huwalisha
 
HOJA yako halmanusura iwe na maana lakini,ulipoanza kuingiza yale unayoyashangaa ulaya na kuyaabudu na kutaka rais afuate sala yako hapo ndo nimekuona huna hoja nzito sana,ila inaonekana unaamini maendeleo kupitia akili za wengine na hasa wazungu hapo tumepishana pole
 
Ni watu wngapi wana hiyo exposure ba bado kimaisha wamechapika tu, au wewe eposure ni kwenda ulaya tu kushangaa magorofa, mbona wazungu pia hawana eposure lakini maisha yao yanasonga....
 
Wewe mleta mada ni pumbavu sana. Eti umefika Manhattan 2002 ukajiona umemaliza kabisa. Watu wameanza kufika huko USA na Europe early 60s, 70s,80s wakafanya kilichowapeleka na kurudi kujenga nchi Tanzania. Vijana Kama wewe mlioenda Marekani kwa Scout na Camp Mna matatizo sana. Status yako ikoje hapo ulipo!!?? Ulipofiwa uliweza kurudi Bongo!? Acha ulimbukeni kijana. Mh Rais haihitaji exposure kwa kuja Manhattan au Chicago...After all sisi Watanzania tunahitaji Maendeleo na huduma bora za Afya na Jamii kwa kila Mtanzania. Hayo mambo ya Exposure peleka Big Brother au kwenu Mpitimbi. Bado unatongoza visichana vya Chuo Facebook kwa kutumia Exposure ya kufika manhattan mwaka 2002!!!!???? Ama kweli Ushamba mzigo!!!
nitake radhi mimi sio kijana mwenzio
 
HOJA yako halmanusura iwe na maana lakini,ulipoanza kuingiza yale unayoyashangaa ulaya na kuyaabudu na kutaka rais afuate sala yako hapo ndo nimekuona huna hoja nzito sana,ila inaonekana unaamini maendeleo kupitia akili za wengine na hasa wazungu hapo tumepishana pole
hapo ndio msingi wa hoja yangu bora tupishane tuelimishane,hivi wewe una tecnology ipi ya kujivunia uliyobuni mwenyewe unaweza kujenga kiwanda kipi bila ushirikiano na hawa ngozi nyeupe,siwaamini ila najua na nakubali wametuzidi kitecnology hilo liko wazi
 
Kwa sisi Watanzania tunachokiona sasa kwa Mh. JPM na unachotuandikia wewe ni sawa nakutuambia kua Nyerere, Mwinyi,Mkapa na Kikwete walienda nje kupata exposure ya kuiharibu Tz na kuwadidimiza Watanzania,

Nasema hivi kwasababu huyu asiekua na exposure ya Ulaya anatusaidia sisi watanzania kuliko hao waliotembea Ulaya yote.

Go Magufuli Go, hamna cha wazungu wala nini, dhamira inatosha kutukomboa siyo lazima hao.
 
Ni watu wngapi wana hiyo exposure ba bado kimaisha wamechapika tu, au wewe eposure ni kwenda ulaya tu kushangaa magorofa, mbona wazungu pia hawana eposure lakini maisha yao yanasonga....
sijasema kushangaa maghorofa bali kujifunza wamefikafika je huko
 
hapo ndio msingi wa hoja yangu bora tupishane tuelimishane,hivi wewe una tecnology ipi ya kujivunia uliyobuni mwenyewe unaweza kujenga kiwanda kipi bila ushirikiano na hawa ngozi nyeupe,siwaamini ila najua na nakubali wametuzidi kitecnology hilo liko wazi

Technology inauzwa, tukiwahitaji tutawafuata kuchukua, hakuna sehemu Rais kasema watu wasiende soma nje, hajakataa kuongea nao chchte ila Mimi na wewe hatuez mchagulia aongee na huyu au yule. Naamini ikulu ina washauri wazuri tu so hatuna haja ya kumlaumu JM
 
Kwa sisi Watanzania tunachokiona sasa kwa Mh. JPM na unachotuandikia wewe ni sawa nakutuambia kua Nyerere, Mwinyi,Mkapa na Kikwete walienda nje kupata exposure ya kuiharibu Tz na kuwadidimiza Watanzania,

Nasema hivi kwasababu huyu asiekua na exposure ya Ulaya anatusaidia sisi watanzania kuliko hao waliotembea Ulaya yote.

Go Magufuli Go, hamna cha wazungu wala nini, dhamira inatosha kutukomboa siyo lazima hao.
ndugu yangu nyie ndio mnampotosha JPM ,mi sio shabikiwa donald trump ila tuwe wakweli bado hatujawa na uwezo wa kutamba bila wao,hapo mpaka nguo ya ndani umevaa ya kutoka china ,simu unayotumia ya kwao,kiti umekalia cha kwao,una nini cha kujivunia made in tanzania
 
nitake radhi mimi sio kijana mwenzio
Ungekuwa sio kijana usingeandika huo Upuuzi wa Exposure ya kufika Manhattan mwaka 2002. Sikutaki radhi mpaka utakapomtaka radhi Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kebehi na dharau uliyomuonyesha wewe muuza Pizza wa Papa John.
 
Kuna mambo fulani kama unayakosa, inabidi ukubali tu kuwa huwezi na umuite mwingine mfanye kazi pamoja kwa manufaa ya wote. Sisi tuna rasilimali lakini hatuna teknolojia, so hatuwezi kukomalia tu kwamba wageni wanatunyonya. Mfano, tungewezaje kujua kama tuna gesi ya kumwaga nchini mwetu kama tusingeingia makubaliano ya uwekezaji na watafiti kutoka nje ya nchi? Wao wanayo teknolojia ya kujua wapi pana gesi, wapi pana uranium, wapi pana mafuta etc. So lazima tushirikiane nao, tuwaite waje kuwekeza katika tafiti na uvunaji, then tuingie mikataba iliyo wazi yenye kutunufaisha wananchi wengi. Lakini kama tukisema kila kitu tunaweza (wakati sio kweli), watoto wetu kukosa huduma bora za afya, maji na elimu wakati tunazo rasilimali za kugharamia hayo yote
Sikatai ila hao tangia wawekeze wameacha technology gani kama huko migodini je niwa Tanzania wangapi wanaruhisiwa kupata hyo knowledge wanayoitumia ka sikuajiri experts kutoka nchini kwao na Watanzania kuwa vibarua tu. Nenda huko gesi ilipovumbuliwa ka kuna Mtanzania ana ruhusiwa kijua kinachoendelea. China, Singapore, Taiwani, south Korea tulikua almost the same ila nao wametuacha mbali. Wale walirndeleza internal capability, innovation na Ku ji invest kwenye elimu na kupata experts. Ili kuendelea lazima tuendeleze wazawa kwa kuwazesha. Na tutumie foreign experts kubenefit nchi sio makampuni yao
 
hivi unaweza ukakaa ndani dili zikajileta zenyewe,usidhani rais wa China na Obama kuja TZ mwaka 2013 walikuja kuuza sura,walikuwa wanafukuzia dill,hata wewe ulipomaliza chuo ulisambaza CV kutafuta kazi,ungekaa ndani hata hii simu unayotumia usingenunua
Kwahyo aende US, China kufanyaje labda zaidi ya kutembeza bakuli. Bila kujijenga ki ndani na kuimarisha mambo ya ndani ka elimu, miundo mbinu hata ahamie China nothing will change sasa nyie waumini wakuwa dependence ndo mnataka awe mzururaji mbona mlikuwa MNA mnanga mkwere
 
Katika sifa kadhaa za mgombea urais kwa tiketi ya ccm huwa ipo ya awe na uzoefu wa masuala ya kimataifa.

sifa hii kwa JPM ilifumbiwa macho,
Nyerere baada ya kusoma nchini alikwenda makerere Uganda na baadae uingereza kunoa Bongo mwinyi alishawahi kukaa Misri ubalozini kwa miaka kadhaa,Mkapa ndio usiseme canada na marekani amekaa sana,JK ziara zake nje ya nchi akiwa foreign affairs minister kwa miaka kumi na miaka kumi ya urais wake ni sawa na kukaa nje miaka mitano,(siungi mkono,it was too much)

JPM alikanyaga Dar es salaam kwa mara ya kwanza mwaka 1984 alipokuwa anakuja kujaza fomu ya kujiunga na UDSM,tangu hapo hajawahi kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi mmoja Amezunguka vichochoro vyote vya Tanzania alipokuwa waziri wa ujenzi akikagua barabara,kazi aliyoiweza kuliko mawaziri wote tangu uhuru .

Back to the point,mimi nimezaliwa Dar Es Salaam na enzi za ujana wangu nilikuwa najiona mtoto wa mjini sana ila siku nilipokanyaga Manhattan mwaka 2002 nilijiona ni mshamba sana kila kitu nilikiona ni kipya na tangu siku hiyo nikajua Dar Es Salaam sio jiji bali ni mji tu.

Wazungu wanakitu wanaita exposure , huwa ni shule tosha kwa tuliosoma zamani tunajua ,mtu wa mtwara kuchaguliwa sekondari wilaya ya Ngara japo kwa upande mmoja ilichangiwa na uhaba wa shule ila ilitusaidia sana,kwa sasa kuna wanafunzi wanazaliwa ndani ya wilaya x,primary mpaka sekondari anasomea ndani ya wilaya hiyohiyo na chuo cha ualimu hapo hapo na anakuja kufundisha shule ndani ya wilaya hiyohiyo ,huyu anakosa exposure atakuwa mshamba tu.

Pia kwa waliopitia vyuo vikuu vya Tanzania mtagundua kuwa lecturers walipata elimu yao nchini bila kwenda nje ya nchi huwa wanakamata sana wanafunzi wakati wa mitihani kuliko walimu waliosomea nje.(sina uhakika kama kutumbua majipu yanhusiana na kukosa exposure )

JPM anasema anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda sasa nashangaa itakuwaje nchi ya viwanda wakati anawakimbia wazungu ambao ndio wenye technology ya viwanda,kama hadi pampas za watoto tunaagiza tukubali hatuwezi kujenga viwanda bila kuwa karibu na wazungu,awakaribishe wakae mezani waongee dili win win based business,wanatuhitaji pia bado tunawahitaji,ndio maana Nyerere na kuwatimua kote waingereza alifia kwao akukubali kufia Muhimbili

Pia JPM amekaliliwa akisema Dar ndio kioo cha Tanzania ndio maana anataka kujenga daraja toka cocobeach mpaka ocean road,hii ni kukosa exposure,nchi za watu maendeleo huwa yanakuwa balanced na pia fursa zinakuwa balanced kila sehemu kupunguza msongamano wa watu kwenye miji fulani,kuna baadhi ya nchi watu hawataki kuishi miji mikuu kwani fursa ziko kila kona,Juzi tumesikia kuwa Obama atakuwa rais wa pili wa marekani kuishi washngtone baada ya kustaafu na hii ni kwa sababu watoto wake bado wapo shule,other wise angerudi kwao chicago,JK wakati anakabidhi ikulu na kutuaga kuwa anarudi kijijini helicopter ilimpeleka Msoga mchana jioni akarudi nayo Dar.

Tanzania sio Dar tu
Pia exposure inasaidia kuimprove lugha za kigeni,hili sitaki kuliongelea sana hapa nisije kuchafua jukwaa
Na hilo la mwisho unalo dai hutaki kuliongelea sana ndio hasa target yako umezunguka weee!.
 
Back
Top Bottom